Mpenzi wangu

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
92,216
113,510
Leo boksi si kwa sana kwa hiyo nimejikalia tu hapa nikikumbuka enzi za ushababi wangu....mapitio yote niliyopitia na tajiriba ya maisha niliyonayo na jinsi ilivyoniumba hadi kufikia hapa nilipo.

Naweza kabisa kusema sasa niko muungwana na msharafu nikilinganisha na nilivyokuwa. Licha ya hivyo, hili si dhumuni la mada hii.

Dhumuni la uzi huu ni wimbo. Wimbo ambao jina limenitoka kidogo ila nakumbuka maneno mawili matatu.

"Nina mpenzi wangu Kibamba eeeh eeeh Kibamba eeeh
Mpenzi wangu Kibamba eeh Kibamba"

Hivi huu wimbo aliimba nani na ninaweza kuupata wapi? Natanguliza shukurani kwa wale watakaosaidia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom