Wakuu poleni na majukumu ya kila siku, nina mpenzi wangu tuliachana naye kwa kwa muda wa mwezi mmoja kisa aliniambia sex mpaka ndoa basi bwana mimi nikasema isiwe kesi nakamkaushia mazima sikumtafuta wala nini nashangaa siku moja usiku wa manane saa nane akanitafuta na kuniomba msamaha kwa yote aliyonifanyia na kusema kuwa anaitaji nimsamehe basi baada ya siku nne nikamjibu nikasema sawa sote ni binadamu na hakuna binadamu mkamilifu nikaamua kumsamehe nashangaa jana ananiita na kusema nimekuomba msamaha kwa sababu nimekuota umekufa nilishiwa nguvu ghafla na nikamjibu sawa kama kuna mipango ya mungu tumwachie yeye. Hili likoje mpenzi wako kukuotea umekufa?
ndugu yangu, niseme ukweli tu kuhusu ndoto, huwa ni kitu cha kweli na ni taarifa halisi. isipokuwa ni kwa zile ndoto tu ambazo zimetoka kwa Mungu nazo huwa ni dhahiri, zina mnaso wake, zina uzito wake, hautasahau na hautauliza maswali kama ni za Mungu au la kwasababu zinakupa majibu moyoni kuwa upako wa ndoto hii sio wa kibinadamu wala kishetani.
binafsi miezi miwili iliyopita niliota mama wa rafiki yangu amekufa, na mpaka sasaivi wamemaliza mwezi mmoja wamemzika. nasema ukweli wote toka moyoni, sitanii wala sishabikii kitu hapa. nilikuja kuota mtoto wa dada yangu anayeishi nami mkoa mmoja amefariki...nikagutuka nikaanza kuomba na kukemea, nilisambaratisha roho ya mauti katika ulimwengu wa roho kwa Jina la Yesu Kristo na kwa Damu ya Yesu Kristo.....yule kijana alikuwa ametoroka kwao akawa hataki hata tujue anaishi wapi, mimi niko naye mkoa mmoja akadanganya kuwa hana ndugu yeyote katika jiji hilo....matokeo yake, baada ya maombi alijileta mwenyewe akiwa ameuguaaaaa, amekondaaaa hadi nilitaka kumsahau. nilimshukuru Mungu nikajua kumbe ule ugonjwa ndio ulikuwa unaenda kumuua na kwa neema ya Mungu amepona. yupo hai hadi hivi sasa.
kuna mambo mengi sana niliota yametokea.
mwezi uliopita kuna deal moja kubwa ya hela nyingiiii nilikuwa natakiwa kupata katika shughuli zangu, tulishakamilisha kila kitu, ni issue ya kimataifa na ina pesa ndefu sana. wiki moja kabla sijaanza ile kazi/shughuli Mungu alinionyesha katika ndoto....kuwa nilikuwa nimesimama mahali samaki mmoja mkubwaaaa kupindukia, ni kama yale masangara makubwa sana zaidi ya kilo kumi yale alikuwa anakuja akiruka kwangu ili mimi nimkamate, lakini alipofika kwangu tu ghafla akageuza akarudi nyuma kwa mbio na kurukia kwa watu wawili wakamdaka. hiyo ndoto ilikuwa na upako sana na ilikuwa na uhakikisho ndani ya roho kwamba ni ya kweli. mimi baada ya kukosa yule samaki nikawa nimebakiwa na vikuku tu vingiii hao broilers wamenizunguka wengi sana na ndio ningeweza kuwadaka hao kama kitoweo changu.
niliamka usingizi ukaniishia, sikuhitaji kutafuta sana maana ya ile ndoto kwasababu Mungu alinihakikishia moyoni kwamba ILE DILI YA PESA NDEFUUU IMEONDOKA MIKONONI MWANGU KUNA WATU WAWILI WAMEISHUKUA. niliumia sana kwasababu niliuwa nimeshaanza hadi kupanga ratiba ya hizo pesa. hahahahaha, lakini moyoni nikawa nina amani kubwa sana, Mungu alinipa amani kubwa na uhakikisho kwamba Mungu ameamua iwe vile kwa mapenzi yake, nikalipokea kama lilivyo.
nimeamka, nilitakiwa katikati ya mwezi uliopita nianze ile shughuli, nikaamua kumpigia mkuu wa kitengo kile na kumwambia niendelee tu na kazi zangu au la, ajabu yake wakati tulikuwa tumepangana nianze shughuli, akaniambia tu kuwa hivi ndio nilitaka nikupigie simu, ile dili yako kuna fulani na fulani wameichukua...hahaha. ndoto yangu imetokea vilevile na rohoni Mungu akanithibitishia kuwa vile ulivyoona ndio hivi....
nimeongea mara nyingi sana na Mungu kwenye ndoto, hasa matatizo yanapotaka kutokea huwa Mungu ananionyesha kwenye ndoto. zamani nilikuwa najua labda nina matatizo, lakini ndoto zile za Kimungu huwa tofauti na ndoto za ugali...hahaha.
ninachokushauri, kama bado haujafa hadi sasaivi, piga goti, mwombe Mungu. kama haujaokoka, okoka haraka kwasababu maombi ya waovu huwa hayasikiwi mbele za Mungu, lazima upatane na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo ndio kama upatanisho Mungu atakusikia, otherwise ni neema tu ya Mungu. ukishaokoka, pambana kusambaratisha roho ya mauti, ni roho kabisa inasikia na itakimbia hautakufa, la sivyo kama hautafanya hivyo, unaweza kufa kweli. Mungu akusaidie.