Wakuu poleni na majukumu ya kila siku, nina mpenzi wangu tuliachana naye kwa kwa muda wa mwezi mmoja kisa aliniambia sex mpaka ndoa basi bwana mimi nikasema isiwe kesi nakamkaushia mazima sikumtafuta wala nini nashangaa siku moja usiku wa manane saa nane akanitafuta na kuniomba msamaha kwa yote aliyonifanyia na kusema kuwa anaitaji nimsamehe basi baada ya siku nne nikamjibu nikasema sawa sote ni binadamu na hakuna binadamu mkamilifu nikaamua kumsamehe nashangaa jana ananiita na kusema nimekuomba msamaha kwa sababu nimekuota umekufa nilishiwa nguvu ghafla na nikamjibu sawa kama kuna mipango ya mungu tumwachie yeye. Hili likoje mpenzi wako kukuotea umekufa?