Mpenzi wangu kanipatia zawadi ya mtego wa kuogea

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Nimejikuta nikijiuliza maswali mengi sana. Mida ya asubuhi wakati tunaelekea kazini tumekutana na baba mmoja akiwa anauza madodoki ya kuogea.

Mara nashangaa anaitwa na kuanza kuhojiwa ubora wa dodoki hilo. Kama masihara, huyo mwanamke kalinunua na kulitia kwenye kifuko cha shing'mia. Wakati wa kuagana ili kila mmoja ashike njia yake, binti akaamua kunikabidhi na kunambia kuwa amevutiwa nalo na anapenda nilitumie.

Ninachojiuliza:
Ameona kuwa mimi siogi kiasi cha kunipatia zawadi hiyo? Kwani hakuona zawadi nyingine tofauti na hiyo?

Nimesononeka sana aisee.
 
Back
Top Bottom