kipepeo mweusi
JF-Expert Member
- May 31, 2014
- 244
- 71
Habari wanajukwaa,
Labda nianze kwa kusema haya sasa ni mapenzi au wizi? Mnamo juzi kati siku ya jumapili tuligombana na mke wangu lakini ulikuwa ni ugomvi wa kawaida tu, kama mnavojua katika mapenzi lazima iwepo mitafaruku ya hapa na pale, tukanuniana siku nzima lakin kufikia jumatatu kila mtu akawa kama ameshapotezea hivi.
Jana kaniandalia chai vizuri, nikanywa nikaondoka zangu kazini, cha ajabu jioni narudi kazini nakuta hakuna mtu wala hakuna kitu cha aina yoyote mule ndani kwa maana nyingine (ametoroka) kabeba kila kitu kilicho chake na kisicho chake, na hapa nilipo nilienda kulala kwa rafiki yangu sijaenda kazini na sielewi nifanyenini.
Samahani mkuu huyo dada ulikuwa unaishi nae tu au ni mkeo wa ndoa?? pole kwa yaliyokukuta.