Mpenzi wangu kaniibia kila kitu, katoroka

Mpenzi wangu kaniibia kila kitu, katoroka

youngsharo

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2015
Posts
2,491
Reaction score
500
Habari wanajukwaa,

Labda nianze kwa kusema haya sasa ni mapenzi au wizi? Mnamo juzi kati siku ya jumapili tuligombana na mke wangu lakini ulikuwa ni ugomvi wa kawaida tu, kama mnavojua katika mapenzi lazima iwepo mitafaruku ya hapa na pale, tukanuniana siku nzima lakin kufikia jumatatu kila mtu akawa kama ameshapotezea hivi.

Jana kaniandalia chai vizuri, nikanywa nikaondoka zangu kazini, cha ajabu jioni narudi kazini nakuta hakuna mtu wala hakuna kitu cha aina yoyote mule ndani kwa maana nyingine (ametoroka) kabeba kila kitu kilicho chake na kisicho chake, na hapa nilipo nilienda kulala kwa rafiki yangu sijaenda kazini na sielewi nifanyenini.
 
Huyo mkeo mlikutana barabarani au mnafahamiana hadi kwa wazazi wenu? Na hivyo Vitu kavibeba kuvipeleka kwao au wapi? kama ndugu zake wamempokea na hivyo Vitu itakuwa maajabu. Anza kumtafuta kwa ndugu zake kwanza. Ila kama mlikutana kimjini mjini then pole, Anza tu upya
 
je ikwa umeoa, huyo mke hana kwao....
 
usipanic wemsubirie tu nyumbani labda kavipelekwa kwa fundi kuvitengeneza.yani wewe umeibiwa alafu unamuita mkeo siku hizi hakuwa wake ni majambazi
 
Kwan hapa siku hizi RB zinatolewa au?
 
Huyo mkeo mlikutana barabarani au mnafahamiana hadi kwa wazazi wenu? Na hivyo Vitu kavibeba kuvipeleka kwao au wapi? kama ndugu zake wamempokea na hivyo Vitu itakuwa maajabu. Anza kumtafuta kwa ndugu zake kwanza. Ila kama mlikutana kimjini mjini then pole, Anza tu upya

ndo sijajua yupo kwao ama vp
 
ha ha ha ha h, muda wangu mwingi nilikuwa kwenye Jf jukwaa la kisiasa, ni juzi tu nimechungulia kwenye hili jukwaa. Kinachonifurahisha kwenye hili jukwa ni vituko vya mitaani live. Hapa ni futuhi kwenda mbele.

serious bro.
 
HABARI ZENU WANAJUKWAA,

Labda nianze kwa kusema haya sasa ni (MAPENZI WIZI), mnamo juzi kati siku ya jumapili tuligombana na mke wangu lakini ulikuwa ni ugomvi wa kawaida tu, kama mnavojua katika mapenzi lazima iwepo mitafaruku ya hapa na pale, tukanuniana siku nzima lakin kufikia jumatatu kila mtu akawa kama ameshapotezea hivi.

Jana kaniandalia chai vizuri, nikanywa nikaondoka zangu kazini, cha ajabu jioni narudi kazini nakuta hakuna mtu wala hakuna kitu cha aina yoyote mule ndani kwa maana nyingine (ametoroka) kabeba kila kitu kilicho chake na kisicho chake, na hapa nilipo nilienda kulala kwa rafiki yangu sijaenda kazini na sielewi nifanye nini.
Shkuru Mungu hajakuwekea sumu tu, mpenzi utapata mengine na vitu untanunua vyengine.
 
usipanic wemsubirie tu nyumbani labda kavipelekwa kwa fundi kuvitengeneza.yani wewe umeibiwa alafu unamuita mkeo siku hizi hakuwa wake ni majambazi

hahahaaaaaaaa duh vitu vyote kapeleka kwa fundi!
 
Back
Top Bottom