Mpenzi wangu anapenda sana pesa

Mpenzi wangu anapenda sana pesa

dogo kubwa

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2016
Posts
798
Reaction score
695
Nimefahamiana nae miaka 9 iliyopita, wakati nafahamiana naye alikuwa na ugomvi na mchumba wake kuwa mchumba wake amezaa nje. Ni yeye alinipenda baada ya kuniona, ilikuwa kwenye social function fulani, mimi nilimuona but sikumuwazia kimapenzi wala kumuweka kichwani.

Baadae akapata mawasiliano yangu sababu kuna mtu nafahamiana naye alimpa namba zangu. Alinitega ofcourse ni mzuri kidizain na kutokana na kuwa na lifestyle la kishua by then mimi nimechoka nikaona kama zali la mentali kumpata. Nikiri wazi hajawahi kunipa hata elfu 1, but niliona zali kutokana na quality yake wakati huo hata kumiliki elfu 50 kwangu ni issue.

Sasa ikafika mahali akapata ujauzito wangu, hakutaka kuniambia but alijihudumia mwanzo mwisho mpaka siku anajifungua, niligundua mjamzito sababu nilikaa muda mrefu bila kuonana naye kutokana na nature ya majukumu yangu. Amehudumia mtoto kwa sehemu kubwa yeye.

Kuna kipindi nilijibana nikamtumia milioni mbili azifanyie biashara but mpaka leo sijapata faida hata mia, makubaliano ilikuwa tugawane faida, mtaji asiule, akakubali.

Suala ni kuwa huyu bidada amepanga mjini sasa hivi atleast ninajiweza kidogo, sema anataka nimgharamie mimi kila kitu, kodi ya nyumba, bili za umeme na maji, nimjengee, nimnunulie gari, akiugua nimtibishe, nisaidie ndugu zake n.k.

Mpaka sasa hivi nikigusia mtaji niliompa azungushe tunaanza ugomvi anasema kwanini naumizwa na hela alokula yeye na mwanangu, pia alipopanga ana ndugu zake kibao.

Nilikuwa nampenda sana zamani but nimemchoka kwa vizinga na ana maisha fulani classic anataka gharama nizilipe mimi.

Ushauri wenu wanakuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani hataki ndoa kati yenu, yeye au wewe?
Kwa sbb kutokana na umri wa uhusiano wenu na vile mmezaa kwa nini msikae pamoja? Au kuna utata

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dogo kubwa,

Nampenda sana huyo Mpenzi wako na jinsi ambavyo anakupelekesha kwani hata haya Maelezo yako tu hapa unaonekana Wewe ni Dhaifu, Hujiamini na umetawaliwa na Gubu halafu huna Kifua ( Uwezo wa Kutunza Jambo ) huku ukiwa na Viashiria vyote vya Mwanaume Mbea na Mswahili Mswahili hivi.
 
pambana au amua kadri akili yako inavyotaka. wamo kibao ndoani yanawakuta. matatizo ya aina yako.

wakizikosa wanazipokea kutoka kwa wafadhiri wanaowajua wao, ukijitutumua kuhoji utaambiwa nimetumiwa na kaka au baba!!! kwani una jingine ka kuongeza mkuu, maana alizoea maisha ya kitajiri kwao, inabidi tu uzoee au utunishe misuli uozee jela maana ai kwa wingi wa asasi za kupigania haki zao bali tulibebeshwa balaa!

lini nitasahau

'usinibabaishe, hivi unionavyo natongozwa na wenye magari yao na wenye pesa zao'

wakati huo sina hata uwezo wa kumiliki hata phoenix ya 100,000/=

Sent using Jamii Forums mobile app
 
usimhukumu, kumbuka SHARING IS CARING!

angalau huyu ametumia jukwaa hili kuweka wazi changamoto yake na hapa atapata kitu cha kujifunza nanfaraja juu na kuyaona matatizo yake kuwa ni jambo la kawaida upande mwingine. sio wale wanajifanya wana kifua cha kuyabeba, miezi kadhaa unasikia wamejitundika au kuangamiza wabaya wao kwa mapanga/sumu nao kujimaliza.

kuna kasoro ya kiufundi mahali.
Nampenda sana huyo Mpenzi wako na jinsi ambavyo anakupelekesha kwani hata haya Maelezo yako tu hapa unaonekana Wewe ni Dhaifu, Hujiamini na umetawaliwa na Gubu halafu huna Kifua ( Uwezo wa Kutunza Jambo ) huku ukiwa na Viashiria vyote vya Mwanaume Mbea na Mswahili Mswahili hivi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nampenda sana huyo Mpenzi wako na jinsi ambavyo anakupelekesha kwani hata haya Maelezo yako tu hapa unaonekana Wewe ni Dhaifu, Hujiamini na umetawaliwa na Gubu halafu huna Kifua ( Uwezo wa Kutunza Jambo ) huku ukiwa na Viashiria vyote vya Mwanaume Mbea na Mswahili Mswahili hivi.
hapa jukwaani sio pa kuonesha umwamba, namuonesha nani mimi ni mwamba, ili inisaidie nini,,,,,,,,majukwaa yana maana gani kama vifua tunavyo, halafu ujue naconsider pia nae kagharamika kidizain kutunza mimba mpaka kujifungua, mwanaume yeyote mwenye akili timamu lazima uwaze pande zote ili uwe balanced, it is true that amegharamika kidizain it is true nimempa mtaji hakuna maelezo wala faid mpaka leo, it is true ananipa mzigo mzito nimuhudumie huku siko fresh ndo najipanga,,,,,,so issue kama hii inahitaji a comprehensive judgement, sio kuonesha UANAUME
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom