Mpenzi wangu ananitukana sana!

"Nsubiri nipate kazi ndo niondoke" ....... Kumbe hata naww umetega ? .

Natania...Anakutukana akiwa katika hali ipi?? Ni chapombe?? .

Huna pa kwenda? [emoji23]... Ndo kutaka Kuendelea kuishi mjini??.

Sasa basi, ili kuondoa lawama, asije kukulaumu wakat ambao umemuacha sababu unepata kazi, ni vema ufanye maamuzi ya kuondoka katika wakat huu huu ambao Unanyanyaswa na kutukana .

Ukija ondoka sababu umepata kazi, itaonekanaga wee ni mdada usokua na Fadhila wala shukran . Na watu hawataona kua ulikua ukitukanwa.

Yes life ni gumu mno , usione mbwembwe za humu ukazitaman , life ni gumu sana , Rudi kwa wazazi mdada, Wakat huo ukipigana .
 
Dah....vumilia tu....matusi ndiyo Kodi yenyewe ya nyumba hiyo... Vipi mzigo unampa? [emoji41]
 
Pole dada angu. Anakunyanyasa sababu huna chochote kwa sasa. Ni vema ukatafuta kwingine pa kuegemea. Kwa ndugu labda..
Ningekuwa karib ningekupa hifadhi.. maana mm huwa nasafir sana. Marisa k
 
Nyumbani ni nyumbani hata kama kichakani.We umemaliza chuo gani??Tatizo mnaogopa changamoto za mlipozaliwa sio wewe hicho ni kilio cha mabinti wengi wa bush mkimaliza home hampataki vijana wa mjini wanawapokea magetoni na ndoa za mikataba
 
huyo mwanaume ana elimu gani nae? anashughilika na nini? au kapata kazi bandarini?
 
Kama wazazi wako wapo nakushauri rudi nyumbani
 
Ni kwa sababu miaka miwili hujamzalia, iko hivi, kuna mwanamke mwingine hapo anafanya yake ususe tu atie timu..humo mwanaume uliyenaye ni mvulana..bado hajawa mwanaume ki akili, kuna fukuto kubwa la hasira na majuto kuwepo kwako kwake..pengine hana chochote anachomiliki zaid ya subwoofer....agh iko hivi binaadam wote tuna mitihani, inazidiana tuu fanya utafute maisha yako, inawezekana kaanze hata na sufuri 4 na godoro mengine yatakuja hukohuko..ukishindwa, vumilia matusi na kuwa mtumwa wa ngono.
 
Kwanza nikupe pole kwa hayo unayo pitia usifikirie tu kupata kazi fikiria pia kujianzishia shughuli ndogondogo ili uweze kuendelea na kuondokana na utegemezi
 
Hivi sasa ndio muda sahihi kabisa wa wewe kuondoka,katika hali kama hiyo ngumu ndicho kipindi muafaka kwa wewe kuondoka, utajifunza mengi wewe mwenyewe lakini pia utamfunza na huyo mwenzako anayekunyanyasa, kwasababu anajua kwamba huna pa kwenda. Unaendelea kuwepo hapo kwasababu hupendi shida, lakini wakati mwingine ni bora upate shida ndio utajifunza zaidi lakini ukiendelea kuishi hapo hutajifunza, lakini hata kama kuna mtu anataka kukusaidia hajui kama unahitaji msaada maana uko kwa mtu na yaliyo ndani hakuna ayajuaye. Ukisubiri upate kazi ndipo uhame, utaongeza matatizo kwa siku zijazo kwasababu wewe hutakuwa tofauti na huyo unayeishi naye, maana atasema nimemsaidia sana lakini ona sasa amepata kazi amenikimbia na atakusumbua milele. Kimbia sasa, hama haraka sana
 
Kwa kifupi kabisa ni kwamba sasa hivi hakupendi tena,amekuchoka,ameshajua kuwa yeye ndiye mungu wako na huenda ana kademu pembeni tayari!......Sepa zako,you have to find a way against all odds!
 
Unataka kutuambia huna wazazi kabisa

Au ndugu

Ngoja akudunge mimba na makofi juu
 
Kama unampenda kwa dhati na huishi nae kwa sababu tu umekosa pa kuishi na umekataliwa na ndugu zako sikushauri kumuacha mwanaume huyo.....nakushaur utafute muda uongee nae vizur na kwa upole umuulize nini tatizo hadi amekuwa hvyo maana nilivyosoma na kuelewa inamaanisha hakuwa hvyo awali kwahyo ni vzur kumuweka chini na kumuuliza kwa upole nini chanzo cha kukutukana.....ktk mahusiano hii hatua hutokea ya wapenzi kuchokana na usipokuwa mvumilivu utaacha kila mwaka maana hakuna binadamu asiye na mapungufu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…