Ushauri unahitajika, mpenzi wangu anawasiliana na wanaume wengine

John Gregory

JF-Expert Member
Jul 14, 2019
1,060
1,957
Habarini wandugu

Kabla ya yote naomba nitangulize shukrani zangu kwa ukarimu upendo na undugu uliopo baina yetu japo wengi wetu hatufahamiani lakini tumekuwa tukisaidiana hususan kwa ushauri mzuri.

Moja kwa moja niende kwenye kile kilichonileta hapa, nimekuwa nikiishi na mpenzi wangu ambaye nikiri kuwa bado ni tineja na nimemzidi miaka mingi kidogo na nimeishi naye kwa miezi kadhaa.Siku za karibu nimekuwa nikidadisi simu yake na nimegundua anawasiliana na watu tofauti tofauti.

Kwa kifupi amekuwa akiwasiliana na wanaume tofauti tofauti na mawasiliano yao si ya kuridhisha kwani anajirahisisha kwao na wengine hata kupanga kuonana nao.Cha ajabu nikijaribu kumhoji na kumwambia kwanini anafanya hivyo? (japo kimafumbo bila yeye kujua kuwa ninafahamu anaowasiliana nao)

Anapinga kabisa na kudai ananipenda na hawezi kufanya hivyo.Mbaya zaidi siku za karibuni amepata mimba na ushahidi ninao kuwa amekutana na mwanaume mwingine siku za hatari pia katika siku hizo hizo za hatari amekuwa akikutana na mimi kwa kuwa ninaishi naye.

Kwa kifupi sina uhakika kama mimba ni yangu ( japo anasema ni yangu ) na sitokuwa tayari kulea mimba ya mwanaume mwingine au kuishi na mwanamke mwenye mtoto wa kidume mwenzangu.Kiukweli roho inaniuma sana na mpaka sasa nimebaki njia panda sijui nifanye nini.Ninaomba ushauri wenu ndugu zangu.Ahsanteni


1627022299340.png

Update 01


Nimemtimua Binti; Yupo kwao.


Update 02

Wakuu habari zenu?.Kwanza niwape pole kwa majukumu ya kila siku katika mapambano ya kuinua uchumi.

Baada ya miezi kadhaa nimeamua kuleta mrejesho wa hali ilivyo ili pamoja na mengineyo,Niweze kupata ushauri zaidi.

Kwanza baada ya kuwapa update kwamba binti nilimrudisha kwao niwajulishe tu kuwa mpaka sasa bado yupo kwa wazazi wake hakuna kilichobadilika.Baada ya binti kukataa kujishusha na kuongea ukweli wakati ushahidi wote ulikuwepo nilichukia zaidi.Nisiwachoshe sana,Ni kwamba amekubali kuwa kweli alichepuka tena katika siku ya hatari zaidi (wale mnaoelewa jinsi mizunguko ya siku za wanawake zinavyoenda nadhani mtakuwa mnaielewa day 14).Jambo moja ambalo amelia na kusisitiza sana ni kwamba walitumia kinga.Huyo jamaa pia alinipigia simu akiniaminisha kwamba ana uhakika 100% kwamba alitumia mpira na siku zote huwa anatumia mpira kwa mwanamke yeyote anayekutana naye.

Kwa maana hiyo amesisitiza kuwa anauhakika 100% kwamba mimi ndiye mhusika.Na yupo tayari hata kufanya DNA test baada ya mtoto kuzaliwa.Nikiri wazi kuwa baada ya misisitizo hiyo imebidi niwe mpole kidogo.Nilikuwa nimepanga nimtelekeze 100% mpaka mtoto atakapozaliwa,Lakini kwa sasa imebidi nianze kuhudumia.

Sasa katika harakati za kuhudumia kuulizia chakula anachokula,maendeleo ya mtoto tumboni n.k nimejikuta zile hasira nilizokuwa nazo juu yake zinaanza kunipungukia kwakweli sijui ni mbinu za wanawake,Lakini nimefanya hayo yote pia nikijaribu kumuondoa stress (Maana anaonekana kuchoka sana na kulemewa na mzigo) Jambo ambalo si zuri kwa afya ya mtoto tumboni.

Je, Mpaka hapo nipo sawa au nimekosea?
 
Ulipogundua anawasiliana na wengine kwa nini usimwambie ukweli nimegundua hiki.Eti ukamuuliza kwa mafumbo wewe ukosawa kweli kapata mimba na Ukimwi je?
Ningemueleza angeuliza nimejuaje na angegundua mbinu zangu angeomba msamaha ashum ningemsamehe then what? Angeanza tena tabia hizo kwa kujihami tayari akijua mbinu yangu kuwa huwa ninashika simu yake anaifahamu hivyo angetumia njia mbadala
 
Ningemueleza angeuliza nimejuaje na angegundua mbinu zangu angeomba msamaha ashum ningemsamehe then what? Angeanza tena tabia hizo kwa kujihami tayari akijua mbinu yangu kuwa huwa ninashika simu yake anaifahamu hivyo angetumia njia mbadala
Kwani ulivyomuuliza kimafumbo hajagundua mbinu zako hata kama akigundua unaopa kuachwa huna msimamo .
 
Back
Top Bottom