Lea mimba lea mtoto wako ndo ndugu yako huyo, mimi nilikimbiwa na daktari nikiwa na mimba ya miezi 2 huku na huku akaja kuoa mdada mwingine mtoto akiwa na miezi 8, sijawahi onana nae wala kuwasiliana na yeyote kati yao kwao kuanzia mama yake dada zake baba zake, nimepambana mpaka sasa mtoto anasoma chekechekea nalipa ada million 1.3 kwa mwaka na tunafuraha sana nikiwa na huzuni huwa ananiuliza "mama aumwa? Akiamka anasema mama napenda wewe, naenjoy sana.
Bado sijapata mwanaume kwa maisha yangu sasa hivi kila mwanaume mbaba anamuita baba, najua ipo siku nitapata mume na tutakuwa familia bora tu.
Nilipitia mengi sana kudharauliwa, kusemwa kusimangwa kisa tu nimepata nimba na mtoto kabla ndoa ila sasa hivi wao ndiyo wanaona aibu
Dada kaza moyo usitoe mimba utazaa salama ba mtoto atakua na mtakuwa na furaha na amani