Mpenzi wangu ananishauri nitoe mimba, hana uwezo wa kulea

Mpenzi wangu ananishauri nitoe mimba, hana uwezo wa kulea

Usitoe. Wengine wanatumia milions kutafuta hata mtoto mmoja wa dawa hawampati. Kwa kuwa una kazi nzuri sidhani gharama za kumtunza zitakupa shida. Kila la heri na baraka. Ila nyege kitu hatari sana 😜

Mimi nina Mika 29 ninafanya kazi nzuri tu. Ila sasa nikawa sinamtu mda mrefu nikajikuta natuliza miwasho kwa Dereva mmoja wa bajaji.

Sasa swala linakuja kuwa tumedumu kwa muda wa mwezi na Sasa nimegundua ni mjamzito wa week mbili. Kwanzia mwanzo kabisa siku ya Kwanza aliniambia usije beba mimba yangu kua hawezi kulea Saiv.

Nimemwambia juu ya ujauzito anasema nitoe yeye hataki kulea kwani anamtoto mmoja na anashindwa kuhudumia....

Je mnanishaurije?
 
Unampa moyo wako Dereva bajajii...?? Unambebea na mimba akati kakwambia hayupo tayari kuzaa bhasi fanya Hiyo mimba umejipaa tu mzee mama...
Kwani Dereva Bajaji ana shida gani? Si Ni mwanaume.. Au ulitaka niseme Manger wa bank anataka nitoe mimba..hapo ungesema Ni sawa?
 
Kama Uko dar Fanya kun pm Mimi Nina mpaka 37 Sina mtoto natafuta hata mtoto wa kusingiziwa lakini sipati, njoo unisingizie hiyo mpenzi Mimi ntalea kuliko kukiuwa kiumbe kisicho na hatia
Pole usikate tamaaa....Unaweza pata mtoto Mwenyezi Mungu ndo mtoa Riziki
 
Singo maza kama ina dhambi ni ndogo sana ukilinganisha na MUUAJI. 👊🏽👊🏽👊🏽👍🏽

1. Wewe hujui unachotaka kufanya na huo ujauzito?

2. Malengo yake yalikua kuzaa au?

3. Sikiliza moyo wako unachokitaka. Watakwambia zaa (uitwe single mom) au toa (uitwe muuaji)
Maamuzi yako mikononi mwako
 
Pole sana.
Kosa la awali ni kukutana kimwili kabla ya kukamilisha taratibu.Ni kosa ambalo dini zote na mila haliruhusu.Inahitaji taratibu ya msamaha wa Mungu wako.
Pili,jaribu kuwaza huyo unayetaka kumtoa (kukatisha uhai wake) ni binadamu kama wewe (na si ajabu atakayekuja kuwa bora zaidi yako ama yetu sote) ambaye, si ajabu ndie kiumbe pekee utakayejaliwa na (Mungu aepushe hili) labda hatapatikana mwingine tena.Je,majuto yatakayofuata wakati ama hata kama huna kitu au una kila kitu (na labda hata mume,kama sio mpenzi) halafu huna mtoto hata mmoja,utaweza kuibeba hiyo simanzi?
Nafahamu warembo wa haja kadhaa waliovuma sana enzi zao waliochoropoa mimba kama mzaha tu,hatimae wakahaha hadi kukata tamaa na watoto sio tu hawana,bali hata ndoa ama hawana/waliachika/walizivurunda au hata hazina 'ule mvuto wanaoutamani sasa kama pangekuwepo mtoto' japo wana ndoa.
Kutoa mimba ni ukatili usiomithilika.Infact,neno sahihi ni 'KUUA MWANANGU MWENYEWE NILIYEJAALIWA' kwa utashi,pesa na hiyari yangu tena kwa ubinafsi wangu na kutojali kwangu.
Kutoa mimba ni ukatili,ubinafsi,kutoona mbali na kutojali madhara ya dhambi na laana ya uuaji.Kuna siku nilimsikia mhubiri (sikuweza sikusikia aliipata wapi kama reference),akisema kuwa,binti akitoa mimba,laana zake zinaenda hadi kwa nduguze,yaani kaka zake(sikumbuki kama alitaja na wengine,alitamka 'kaka zake').Sikuwahi kusikiliza kwani nilichelewa.Ila,ilimradi linasisitiza ubaya wa hilo kosa,naona si vibaya kufikiria na hilo pia.
Umeshasema mwenyewe kuwa 'una kazi nzuri tu',hiyo haikutoshi? Kukubaliwa na huyo mwanaume kuhusu malezi au wewe kuamua kumlea lipi ni jema na bora zaidi?
Siku atakapokuwa mtu mzima na huyo mtoto akihangaika kukusaidia na kukuletea wajukuu wakupe kampani,utakumbuka kwa uchungu kuwa 'kuna siku nilijiuliza kuwa niitoe mimba ya huyu mtoto au la'.Hata akipita mbele yako wakati huo keshakuwa uhai kamili,binadamu kamili,ikikumbuka tu hata uliwaza kuwa asiwepo,utajiona mkatili sana.Sijui lakini,maana watu mioyo inatofautiana.
Kosa likishafanyika,lisifanyike kosa jingine(tena baya na kubwa zaidi) ili kulifuta au kusawazisha kosa la wali.
Huyo mtoto si ajabu ndio baraka yako ya pekee-siombei hilo,nakuombea upate wengi utakavyo.Ila,nani ajuae mipango ya Mungu?Na hata ukiitoa ukaja kupata wengine,siku akili na moyo wako vikikaa sawa,utamkumbuka na huyo uliyemtoa na kujiuliza/kujilaumu kwa mengi.Ujana mara nyingine huwa una ujinga mwingi sana uliofichika,hadi utakapopevuka zaidi.
Tuwe na huruma.Haifai hata kufikiri hili la uuaji,hasa kiumbe ambeye ni too innocent,vulnerable na wanaotaraji upendo na ulinzi toka HASA kwa wanaowaleta humu duniani,yaani wazazi au mzazi,si vinginevyo.
Kuua kiumbe ambaye alishapitishwa na Muumba kuwa awepo duniani hai,nadhani pia ni kumpinga Mungu.Kuua kiumbe ambaye si ajabu angekuja kuyafurahia mno maisha yake na kuyapenda,ni sawa na kujiua mwenyewe.Kiumbe ambaye si ajabu ataleta maana,thamani,suluhisho na faraja kwa maisha ya wengi,pamoja na kwa wazazi wake.Kiumbe ambaye si ajabu maisha yake yatakuja kuwa ya maana na thamani zaidi hata kuzidi waliomzaa.
Please,usiitoe hiyo mimba!!!
Umeandika kirefu Sana...lakini nimepata point...asante
 
Pole sana Mkuu.

Kama Uko dar Fanya kun pm Mimi Nina mpaka 37 Sina mtoto natafuta hata mtoto wa kusingiziwa lakini sipati, njoo unisingizie hiyo mpenzi Mimi ntalea kuliko kukiuwa kiumbe kisicho na hatia
 
Miaka 29 unashauriwa kutoa mimba halafu inakuingia akilini!!? Wapo wanawake wenye umri kama wako wanashinda makanisani, kwa mashekhe na kwa waganga kutafuta mtoto
Huyo dereva bajaji atakua na mtu wake au hana mpango na wewe....tumia hiyo kazi yako nzuri lea mimba......
Sawa
 
nadhani jamaa hana maamuzi ya kukwambia utoe au usitoe kwa sababu tangu mwanzo alishasema hajiwezi. wewe ilibidi ujue tangu siku hio kwamba ukibeba mimba hilo ni juu yako.

Maswali ya kujiuliza wewe mwenyewe

1. Je, unahitaji mtoto kwa sasa?
2. una uwezo wa kumlea bila usaidizi kutoka kwa baba yake?

hapo ndio utajua kama uitoe au usiitoe.
Kumbuka, uamuzi wa kuitoa au kutoitoa ni wa kwako kwasababu jamaa alishasema asihusishwe pindi utakapopata mimba.
Usimlaumu kabisa utamtendea dhambi, alishakupa tahadhali.
Amekubali kwa Sasa...tumeongea.Sasa sijui huko mbeleni. Thanks
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Ndio furaha yangu hiyo nikujaze nyembe ujae afu me nitokomee kusiko julikana. [emoji28][emoji28] Kama nakuona vile ulivyo vimba mama kijacho wetu[emoji38][emoji38][emoji38][emoji125][emoji125][emoji125]
Kilaza mwenyewe Fala wewe.na siachi ndio ndo ningekuaje kuwa Nina kizazi kifanyacho kazi Kama sio ku...tomb..ana
 
Mahusiano yana mwezi na una ujauzito wa wiki 2?? Aisee ndani ya hizo wiki 2 mshaaminiana mpaka mkapigana minyama nje minyama ndani kavu.
Ila lea tu miaka 29 mingi sana kutoa mimba kama unajimudu zaa tu dadaa.
Ndo hivyo. Anasema anambegu kali hahaha...
 
Kwani Dereva Bajaji ana shida gani? Si Ni mwanaume.. Au ulitaka niseme Manger wa bank anataka nitoe mimba..hapo ungesema Ni sawa?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Sasa dereva bajaji ukute hata bajaji sio yake...Mwenzako kajipima anachoweza ni kumwaga na kusepaa sasa Usingle mama wakujitakiaa haya pambana na hali yako.
 
Ujue hata kutoa ushauri inategemea na mshauriwa yukoje ufikiri wake.
1) Ni dereva bajaj (Probably younger than you) , na keshasema kabisa uwezo wa kulea hana na hataki kuwa na mtoto na wewe. What the hell were you doing with him in the first place??? Hivi watoto mnawachukuliaje? Like unaeza beba na kutoa tu mimba? Kwa starehe ya week mbili?

2) Wiki mbili uko na mtu ambaye anapitisha tu mda, na mimba ukabeba?

Kama maneno ya bwana wako dereva bajaj hukuyasikiliza, utakuja kutusikiliza sisi?
It's not always that we have answers
 
ukitoa mimba, umeua
Mtunze huyo mtoto atakutunza
Ukimuua huyo mtoto utanung'unika sana maishani mwako hususan siku za uzee wako
 
Pole usikate tamaaa....Unaweza pata mtoto Mwenyezi Mungu ndo mtoa Riziki
Jimix kwa huyu atakutungua tena akuachee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mabaharia wanajua kutumia matatizo ya watu kama fursa walahi
 
aya nimaisha yake hapaswi kuwaza watu watasema nini juu yake akiwasikiliza watu atakosa vyote watu hao hao wataanza mbana haolewi angekuwa na mtoto tu wakati umli umeshakata
Bai ze wei usingle mother uko mitandaoni nimeudhuria harusi nyingi tu jamaa wameoa mabinti wsliokwisha zaa
Thanks for you your kind words
 
Back
Top Bottom