Mpenzi wangu amebadilika na anataka kuniacha naombeni ushauri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpenzi wangu amebadilika na anataka kuniacha naombeni ushauri

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Jeff, Jun 27, 2011.

 1. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  wapendwa wanajf
  najua humu ndani kuna thread ambazo huwa hazichukuliwi serioes kutokana na mtoaji mada kutokuwa serious,lakini hili langu nahitaji mawazo yenu
  nina uhusiano na binti mmoja kwa muda wa miaka 4 sasa,mimi ndio niliyemtoa bikra na alikuwa ananipenda sana,tumekuwa tukisaidiana kwa kila kitu,yeye ana elimu ya form 4 nami ni graduate,mimi nilikuwa na kazi hapo awali lakini maka juzi (2009) nikawa sina kazi,lakin aliendelea kunivumilia wakati huo yeye alikuwa anareseat mtihani wa kidato cha nne na ilipofika mwaka jana nilimtafutia chuo kwa juhudi zangu akafanikiwa kupata na sasa yuko moshi anasoma certificate,na mimi bado natafuta kazi sijafanikiwa kupata mpaka leo hii,naandika habari hii nikiwa na majonzi makubwa,
  tumeendelea kuwasiliana akiwa chuoni na kumsaidia kwa mambo yote pamoja na ya kifedha,ilipofika mwezi wa 4 mwaka huu alirudi likizo nyumbani lakini mm nilisafiri hivyo sikuonana nae,aliporudi tena chuo kuanza semester ya pili alikwama fedha ya ada kwani wazazi wake walimwambia watamtumia baada ya wiki mbili na chuoni walikuwa wanahitaji ada ili afanye registration,akanioambia na kuniomba nimsaidie kwa makubaliano kuwa atanirudishia wazazi wake watakapomtumia,nami nikampa bila wasiwasi kwani nampenda na niliamini kuwa ndio atakuwa mke wangu siku za usoni,ilipofika mwezi wa tano mwaka huu akawa amebadilika kila ninapoongea nae kwenye simu amekuwa akinijibu vibaya,na kwa kiburi (just short answers) sababu ni kwamba kila tukiongea kwenye simu namgombeza kwa sababu niliona hajibu kama ilivyokuwa mwanzo na akapunguza mawasiliano na mm,yaani mpaka nimuanze na wakati mwanzo haikuwa hivyo,nilipomuuliza kwanza aliniambia yupo busy,baaae nilipombana zaidi akaniambia anafanya hivyo anaogopa tukiwa tunaongea mara kwa mara kwenye simu tunagombana kwa hiyo ameamua kupunguza mawasiliano labda ndio hatutakuwa tunagombana,
  nami nikachukia nikamwambia kama ni hivyo basi naomba nirudishie pesa nilizokupa,hapo ndio akakasirika na kunirudishishia nusu ya fedha kwa hasira kisha akaniambia tuvunje uhusiano na tubaki kama marafiki tu,sababu anasema nimemnyanyasa na pesa zangu nilizompa na anaogopa nitakuwa namnyanyasa kwenye ndoa sitakuwa namsaidia kwani hivi sasa tu nimemfanyia hivi je kwenye ndoa nitamsaidia? mimi nikamwomba msamaha,lakini hajanielewa anasema hana upendo tena kwangu kama wa mwanzo,na hivyo tubaki marafiki lakini akiwa na shida anaitafuta ili nimsaidie,baadae akasema nisubiri aongee na mama yake then akae na mimi tuongee tena ndio atajua aaume nn,kama ndio basi au tutaendelea na uhusiano wetu
  dada zake wananijua vizuri tu,na mama yake ananisikia japo hajawahi kuniona ila nimewahi kuongea nae kwenye simu na hizo pesa nilizompa za ada mama yake anajua,alipowaomba ushauri dada zake na marafiki zake walimwambia aachane na mm,bado anataka kumuuliza mama yake ndio aje kuamua,yeye bado ananitafuta kimsaada wa mambo mengine ingawa mimi nikimpigia simu anapokea lakini haonyeshi mapenzi kama mwanzo, mimi nilimwambia kama unaamua tusiwe na mahusiano basi tusiwe marafiki kwa sababu mimi itaniuma
  sasa je huyu nimchukulieje? niachane nae au nisubiri hilo jibu lake la mwisho baada ya kuongea na mama yake pamoja na mimi mwenyewe? mpaka sasa mimi bado natafuta kazi hivyo siko vizuri kifedha,naombeni ushauri wenu!
   
 2. K

  Kiduku JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 480
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hamna mapenzi ya kweli hapo maana inaonekana mpo kipesa zaidi wewe na huyo dada

  mpige chini maana pia hana msimamo, kwani mama yake inamhusu nini mapenzi yenu? kaa nae mjadili mustakabali wa mapenzi yenu isijekua unaendeshwa na wakwe baadae

  ni ushauri tuu kama vipi ipotezee
   
 3. Babuu blessed

  Babuu blessed JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 1,340
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Potezea ukuzaliwa nae,mwanamke akishapenda kuondoka ni ngumu huyo akupenda kwa dhati..
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Jun 27, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  sikiliza bwana mdogo.........wewe wakati unatoa pesa ulikuwa unakopsha au vipi?!!

  halafu mdogo wangu kaa chini, tulia tufuta kazi achana na mambo ya wanawake.....wewe mwenyewe hujajiweka vizuri, kazi hujapata lakini bado unahangaika na wanawake........achana nae huyo kaa tulia na fanya masiha kwanza..hawa watu wapo tu tena sana tu wala huna haja ya kusumbuka sana

  NB: tangu 2009 hujapata kazi??? unatafuta au umekaa kufatilia huyu dada..umesomea nini wewe? au umefungiwa kupata kzani ndani ya nchi

  komaa mtoto wa kiume
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,220
  Trophy Points: 280
  kaa chini panga maisha yako na mustakabali wako

  huyo dada limbukeni anathani certificate ndo issue.... hapo maisha anayaona kayapatia!!!

  kwani ulivyomtongoza kakaubali mama yake alihusika? lets say mama yake amwambie mrudiane, so kila mkikwaruzana mtaenda kwa mama? mkitaka ku-doo ataomba ruhusa kwa mama yake?

  kwanza anaonyesha hakutaki anachukulia mama yake kama kikingio.....

  kikubwa panga maisha yako, huyo dada akija kushtuka kuwa vidume vya chuo vinamlaghai too late,,,

  ila nikirudi upande wako , ni kweli wamgombeza hovyo? so badala ya kupata faraja anapata kero za magombezo? next time acha kukoroma koroma hovyo
   
 6. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #6
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,127
  Likes Received: 3,316
  Trophy Points: 280
  Atakuwa na mshakaji huko,.ndiye anayempa kiburi.
   
 7. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #7
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  mkuu mbona wapo wengi tuu? potezea bwanaaa!
   
 8. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #8
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Huyo mmanzi mshamba 2,kadanganyka na washkaj wa chuo anasahau alikotoka,we mpotezee bado anasumbuliwa na compan ya shule,akimalza 2 atajuta na kuanza kukusaka mwenyewe,we 2lia tafuta zako kazi maisha yaendelee.
   
 9. kichwat

  kichwat JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2011
  Joined: Mar 4, 2010
  Messages: 1,824
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hii inawakuta vijana wengi wa kiume, lakini bado hatuikubali, lakini ni kweli. Msichana unayemaliza naye Form 4, au Form 6, au hata College SI SAIZI YAKO HUYO. Kimaisha mvulana anakua taratibu kuliko msichana. Vijana mking'amua ukweli huu mambo yatakuwa rahisi. Msichana unayesoma naye when you're under 30 mara nyingi atakuacha, sababu wasichana wanatakiwa kuwa settled by around 25 - 30. Wakati mvulana unakuwa bado mchanga sana.

  Ndio, wapo wachaaaache ambao hubahatika kudumu na wapenzi wao wa shule.

  ... Haka kaushauri gharama yake ni $ 0.00 lakini katakupunguzia hasara (or even save life sometimes)
   
 10. mito

  mito JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2011
  Joined: Jun 20, 2011
  Messages: 7,613
  Likes Received: 1,993
  Trophy Points: 280
  Kifupi ni kwamba huyo demu hakupendi tena,ila inaonyesha ni wewe ndo unang'ang'ania tu. Kaishapata mwingine we achana naye tu, atakusumbua bure!
   
 11. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Pole sana mdau
  ur graduate.......na unakapenda hako kabint......lakin hakajitambui.....piga moyo konde songa mbele.....maumivu yapo lakini wewe si wa kwanza.......
   
 12. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,658
  Likes Received: 8,211
  Trophy Points: 280
  Wow...what a graduate..umesomea nini mkuu!?? nadhani huyo binti anapata aitime sana mawazoni mwako koz wewe mwenyewe huna cha kufanya! so umekuwa ukiishije tangu 2009? hizo pesa za kumkopesha unatoaga wapi!??
  U have a lot to ask urself before u even start talking abt ur gal....TAFAKARI....CHUKUA HATUA!
   
 13. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  Pole mkuu
  mapenzi ni ya watu 2......anajadili na mamake kitu gani.....hata kuolewa na wewe atamuuliza mamake........... je ikatokea mmeoana kila mara atakuwa anawasiliana na mamake kujadli maisha yenu.........kwa mtazamo huo sidhani kama anastaili kuwa mkeo
   
 14. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Umeanza kwa kusema kuwa unajua humu ndani kuna threads ambazo huwa hazichukuliwi serioes kutokana na mtoaji mada kutokuwa serious. Well, kwenye hii thread yako, hauko serious pia. Ameshakwambia kuwa hana upendo tena kwako kama wa mwanzo na mbaki marafiki tuu. Halafu unataka ushauri kama uachane nae au usubiri jibu lake la mwisho. Sasa hapo unataka tukushauri nini? Grow up man.

  Yaani kama na degree yako unashindwa hata ku make decision in a simple situation like this, then ndio maana labda unashindwa kupata kazi. Pia inaonekana kama huna prioritizing skills. Badala ya ku prioritize kutafuta kazi, unahangaika na mwanamke ambaye tayari ameshakuambia kuwa hakupendi tena. Concentrate kwenye kutafuta kazi. Kazi ni muhimu zaidi. Mambo ya mahusiano weka pembeni. Hayatakusadia na yanakupotezea muda. Kuwa kama mmiliki wa Facebook, ambaye girlfriend wake alimtema, jamaa akaitumia hiyo kama motivation ya kujiendeleza kiuchumi. Angalia alipo sasa.
   
 15. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  kaka sio kama nimekaa tu kazi natafuta ile mbaya kila siku niko mtandaoni na magazet pia,lakini sijapata ndugu,najaribu hata kuomba volunteering lakini wapi,yaani mpaka nataman kukata tamaa
  nimesoma human nutrition kutoka sua ndugu,kama vpi msaada hata wa kujitolea tu nipate experience au hata kufundisha sekondari niko tayari ndugu,kwani kwa sasa nafundisha shule za kata maths,physics and chemistry kwa kujitolea,nikipata private scholls itakuwa poa tu kwangu
  msaada wana jf
   
 16. data

  data JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 16,733
  Likes Received: 6,509
  Trophy Points: 280
  Ivi wanaume wengine mkooojeeeee... piga chini.. unalialia nin?? khaaaaaa...
   
 17. Jeff

  Jeff JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2011
  Joined: Sep 26, 2009
  Messages: 1,218
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mentor,nashukuru kwa ushauri wako,mimi ni graduate kutoka sua,nimesoma human nutrition,najitahidi sana kutafuta kazi,ofisi zingine nikiingia kuomba kujitolea tu wananiulza kuna mtu unamjua humu,nikasema hakuna,wakaniambia huwezi kupata kiurahisi nenda kajaribu ofisi nyingine,kiukweli nimechoka kwa majibu hayo,ndio maana naomba msaada kwa wanajf wenzangu,najua umu mpo wenye nafasi za juu maofisini ambao mnaweza kunisaidia hata kwa kunipa nafasi ya kujitolea tu,nahitaji msaada ndugu zangu
  hzio pesa kukweli niliziotea tu mahali flani kwa muda ndio nikaweza kumsaidia,lakini bado nina hali mbaya sana,kwa mtu anayeweza kunisaidia,my email: kunambi2003@yahoo.com
  asanteni
   
 18. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  umesema akiwa anashida anakutafuta,akiwa na raha je?


  Hongera mana umetoa bikra ingawa usichukulie kigezo cha wewe kutangaza ndoa.

  Kama anania na wewe kwanini atake ushauri kwa mama yake mzazi?
  Kwani wakati mwatongozana mama yake alihusika na jibu ulilopewa na mwanae{ex wako}

  Ushauri wangu ni kutuliza mawazo changanua mwenyewe uone mzani wa upendo umelalia/egemea wapi,mana tunaweza mshauri amuache kumbe limoyo lako bado limemdondokea uyo mpenz wako.
   
 19. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Achana nae huyo ana akili za kushikiwa. Kumpenda mtu hadi amuulize fulani. Aaaagggr..,., ameniboa kweli.
   
 20. Marahaba

  Marahaba Member

  #20
  Jun 27, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka Kumbe matukio haya yanafanana kwa baadhi ya watu , hata mimi yamenikuta , maelezo uliyoyatoa ndo hivyohivyo kwangu pia, kuwa upendo wake kwangu umekwisha, nikasema hata nikiomba msamaha hapa tukirudiana itakuwa utumwa maana ndo yaleyale twende tukaongee na mama au mjomba, nikasema tu you are not of my type, yeye yuko hapo UDSM ndo anamaliza chuo si muda mrefu mwezi wa saba 2011,nimefatilia nikagundua keshapata Mwanamme mwingine ,iikabidi nigive up, so nawe huyo anakuzuga tu kwa ushauri wangu, tafuta kazi , ukishapata Tafuta of your type
   
Loading...