Kuna mshikaji wangu yuko hapa hapa JF anasema amegundua mpenzi/mchumba wake yuko hapa JF kupitia uandishi wa comments zake. Amemtambua kutokana na uandishi wa maneno yake kwenye "text message" anazomtumia na hata maneno anayopenda kuyatumia kwenye kuongea. Je, hili linawezekana? Wewe je, umeweza kumtambua mpenzi/mume/mke/mchumba kupitia uandishi wa comments?