Mpenzi wa kweli anatafutwa

Mpenzi wa kweli anatafutwa

Malaika AD

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
496
Reaction score
316
Jamani leo na mimi nijaribu bahati yangu humu jukwaani, labda naweza vua samaki kwenye shamba la miwa, upweke huu! Mh! Kwa mlio zoea matusi na kejeli wala sivihitaji, mpite mkinyata kimya kimya mnipishe na walio serious.

Natafuta mpenzi wa kweli, mambo ya ndoa yatakuwa makubaliano.

Mimi ni dada mwenye umri wa miaka 28, elimu yangu stashahada, mkristo mcha Mungu, kazi yangu mwanariadha(mkimbiaji), naishi na wazazi wangu hapa mwanza, sina mtoto wala sijawahi kuolewa, niko tayari kuhamia mkoa wowote nitakao pata mpenzi sababu hii kazi yangu ni ya msimu, muonekano wangu - nime attach picha yangu hapo chini.

Haya sasa, wasifu wa nimtafutae;

Umri kuanzia 35+, najua wengi wao wana ndoa lakini kwa hao masingle wachache na mimi niambulie mmoja. Iwe wamechelewa kuoa, wameachika, wagane n.k mi sijali. Nahitaji mtu aliyenizidi kuanzia miaka 7. Halahala kwa wenye watoto kama saccos.

Awe na kipato cha kututosheleza, hapa niwe muwazi tu, yaani wale njaa njaa siwahitaji, kama umezoea kuhonga maelfu hapa kaa kando.

Elimu kuanzia kidato cha nne ila awe muelewa jamani, maana wenzangu na mie tusiosoma huona kila aliyesoma anaringa.

Awe mwenye uwezo wa kutekeleza majukumu yake yote haswaa kama mwanaume. Sipendi wanaume wanaotoa mwanya kwa wenzao kuwasaidia.

Muonekano wa kawaida, nataka gentleman jamani, sipendi mwanaume m-beautiful.
Awe mwenye tabia njema, watoga masikio, wavaa vipini puani, wavaa milegezo wapite mbali kabisa.

Kwa mwenye sifa aliye tayari, karibu sana.
 

Attachments

  • 1404500707728.jpg
    1404500707728.jpg
    57.1 KB · Views: 774
  • 1404500724188.jpg
    1404500724188.jpg
    44.3 KB · Views: 766
  • 1404500741115.jpg
    1404500741115.jpg
    21.3 KB · Views: 739
  • 1404500753720.jpg
    1404500753720.jpg
    41.9 KB · Views: 722
Bandiko zuri kabisaaaaaa. Ungeweka ukiwa umevaa na nguo za michezo (riadha) kabisa, anyway ngoja waje..

Sent from my phone

Sawa, nimeanza na hizo kwanza, hata hivyo mbona madaktari hamuwaambii waweke picha walizovaa makoti? Au mtu akikwambia yeye polisi ni hadi uone kavaa sare za polisi?
 
Mwanariadha na tumbo lote hilo unakimbia mita tano nini? Pia ungetupiamo picha moja ikionyesha kwa nyuma vijana wa siku hizi wanasema uzuri wa nyumba choo

Picha zote hizo bado unadai nyingine! Lol! Unakoelekea utasema niweke picha nikiwa nimevua nguo.
 
Mwanariadha na tumbo lote hilo unakimbia mita tano nini? Pia ungetupiamo picha moja ikionyesha kwa nyuma vijana wa siku hizi wanasema uzuri wa nyumba choo

kaka, kwa hii shape nyuma lazima kuwe flat...ila nisiseme sana, tungoje ageuke...
 
Uko poa kabisa, purely bantu lady, hujapiga deki uso. Hujasema utaratibu wa mawasiliano...hapa hapa hadharani au chumbani(pm)
 
Picha zote hizo bado unadai nyingine! Lol! Unakoelekea utasema niweke picha nikiwa nimevua nguo.

Kila la Heri mrembo, utampata tu mwenzio humu. Kama watu wametafuta kazi humu wamepata ndio iwe mchumba. Ukipata usisahau kurudisha feedback
 
Hizo pictures ni wewe au joking nime compare na avatar yako it means malaika wewe???
 
hutaki mtu njaa njaa eeh? vizuri sana kwani kila mtu hapendi umaskini ila age yako nakushauri chukua yeyote ambae amekuvutia pesa mtatafuta wote
 
Uko poa kabisa, purely bantu lady, hujapiga deki uso. Hujasema utaratibu wa mawasiliano...hapa hapa hadharani au chumbani(pm)

Asante wewe ulieona niko poa. Maana binadamu bwana! Fungukia popote bato
 
Last edited by a moderator:
Kila la Heri mrembo, utampata tu mwenzio humu. Kama watu wametafuta kazi humu wamepata ndio iwe mchumba. Ukipata usisahau kurudisha feedback

Sawa. Asante, naamini nitampata tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom