Mpenzi wa Harmonize amnunulia saa ya milioni 600

saa ya million 600 halafu wanatembelea mark x ya million 14 tena alipewa zawadi na diamond kwenye birthday........anyway kwa akili hizo wacha bashite aendelee kuwatawala dar
Hahahahahah na mimi nashangaa....una saa ya mil 600 unaishi nyumba ya mil 50.....
 
Hawa watu watupumzishe,mayonaise wimbo gani katoa unamhusu?siku zote ni kuiga nyimbo za baba ake ndomo nae bila kolabo na kuiga wapopo hamna kitu.
Huyo demu mnadanganywa mzungu ni mmoroko na mtaliano.
Italia,Milano sijui wapi mi huenda kula bata na blondy wa ukweli,sa ingine bila kuwalipa,respect wakiona huyu mwafrika anatunywesha hivi mbunye unapewa ukinasa unapunwa.
 
saa ya million 600 halafu wanatembelea mark x ya million 14 tena alipewa zawadi na diamond kwenye birthday........anyway kwa akili hizo wacha bashite aendelee kuwatawala dar
Ujue mara nyingi nnashanga watu wanavyo amini maneno ya wasanii.

Wengi hawajui hata maisha yao ni usanii mtupu
 
Kwa thamani yeyote ya hiyo saa, ngoja masela wamuotee! Wakileta kwangu wataniambia tu "mwana cheki mzigo wa kishua huu, kama vipi we tuachie elfu hamsini, ila sema nini mwana, hata twenty siyo mbaya wanao tukajilipue"
 
Mxiuuuuu....saa ya mil 600, while mtwara mama ake anaishi nyumba ya udongo!

Rubbish! Rubbish!
 
saa ya million 600 halafu wanatembelea mark x ya million 14 tena alipewa zawadi na diamond kwenye birthday........anyway kwa akili hizo wacha bashite aendelee kuwatawala dar
Hivi ile mark x nyeusi nilimuona Sinza kampakiza Wolper ndo hiyo hiyo hadi now?
 
Nyumba anayoishi ina gharama gani?
Hata iweje siwezi vaa saa ya mil 600. Nitaiuza kesho yake!
Kuna saa zinaitwa copies...hii inawezekana ni patek phillipe lakini imetengenezewa shenghen!
 
Harmonize ameupasua mtandao wa Instagram kwa mshangao baada ya kuweka wazi bei ya zawadi ya saa ya mkononi aliyonunuliwa na mpenzi wake, Sarah.



Kupitia kipande cha video alichoweka akiwa ughaibuni, mwanafamilia huyo wa WCB ameonesha saa aina ya Patek Philippe ambayo kwa mujibu wake imenunuliwa kwa $267,525 (sawa na shilingi milioni 603 za Tanzania).

Mwimbaji huyo ameweka picha ya inayoonesha saa hiyo yenye mng’ao wa ‘ukwasi’ na kuandika, “Put some respect on it, thanks baby @sarah__tz ❤ Google the price.”

Kwa lugha ya nyumbani Tanzania, Hamornize amemshukuru mpenzi wake Sarah kwa zawadi, ametaka anayeiona aipe heshima, lakini pia ametaka udhibitishe kwa kui-google.

Hata hivyo, alienda mbali na kusaidia kuiangalia kwenye Google ambapo ilionesha bei ya $267,525 huku nyingine ambayo ni tofauti na yake ikionesha bei ya $41,479.

Patek Philippe ni saa za adhimu na zenye gharama kubwa, awali bei ya saa zake ilikuwa kati ya $25,000 hadi $300,000. Lakini hivi karibuni, iliibuka saa ambayo ilitikisha soko, gharama yake ikitajwa kuwa $2.5 Million, kwa mujibu wa Business Insider.

Ni Harmonize pekee na Sarah ndio wanaofahamu ukweli wa bei ya saa hiyo. Kama alivyowahi kusema Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete, “akili ya mbayuwayu changanya na yako.”

GIGOLO???????????????
 
Back
Top Bottom