Mapenzi hayana formular kabisa, muda mwingine watu wanafanyiana yote hayo na wanadumu na kufikia kwenye ndoa kabisa na pengine wengine wanaishia kulia kabisa na tena wengine wanajenga pamoja wakiwa wachumba na mwisho wa siku mmoja anatapeliwa. haya mambo hayana gurantee kabisa maana unaweza kufanya hivyo kwa mumeo nae akatokomea kusiko julikana.
Pengine tujue kabisa Mapenzi ni biashara kama biashara nyingine yana faida na hasara zake na tujue kabisa kupenda ni kutake risk maana muda mwingine unaweza usiwe na uhakika kabisa mnapendana kiasi gani au unapendwa kiasi gani na hayo maswala ya kupena atm huwa yanakuja tuu, kwa hiyo ni vyema tujue tunapo amua kupenda tuna take risk tuu.
Mimi nina rafiki yangu alimsomesha msichna lakini mwisho wa siku msichana alimgeuka kabisa na kutafuta mwingine, kwa hiyo tunatakiwa tujue kabisa tunapotoa atm n.k kuna mawili either kulizwa au kutolizwa yani ni kama gambling