Mpeni pole baba Lulu........ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpeni pole baba Lulu........

Discussion in 'Jamii Photos' started by Rutashubanyuma, Apr 13, 2012.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Michael Edward Kimemeta - baba wa Lulu
   
 2. Lucas

  Lucas JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 2,452
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  na yeye ni mwana JF?
   
 3. j

  jmnamba Senior Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole kwake! Ana wakati mgumu sana.
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Baba mzazi wa Muigizaji wa kike wa filami nchini maarufu kama Lulu, ambaye anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba, ameibuka na kueleza kushtushwa sana na taarifa za kifo hicho pamoja na habari kuwa bintiye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na muigizaji huyo nguli na kuwa anahusika na kifo chake. Baba Lulu, ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimemeta(49) mzaliwa wa Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro, kaiambia Globu ya Jamii leo huko Moshi kuwa alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu wa mtoto wake Lulu,lakini hakuamini masikio yake baada ya kupata taarifa za kifo hicho, huku bintiye, anayedaiwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu, anahusika.


  Lulu alifikishwa mahakamani jana April 11, 2012 akikabiriwa na mashtaka ya mauaji ya Marehemu Steven Kanumba, ikiwa ni siku nne baada ya kifo cha msanii huyo. Alisema kuwa Elizabeth ama Lulu alizaliwa tarehe April 17,1995 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, na kwamba alimaliza elimu ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Midway mwaka jana na kamba hivi sasa ana umri wa miaka 17. Bw Kimemeta alisema kuwa ni vyema polisi kuwa makini katika uchunguzi wao kwa kuzingatia kuwa tukio hilo limejenga chuki na uhasama baina ya Lulu na ndugu, jamaa, marafiki na wapenzi wa marehemu Steven Kanumba. Alisema kuwa kilichomshtusha zaidi ni taarifa za polisi kusema kuwa kulitokea ugomvi kati ya Marehemu Steve Kanumba na Lulu,huku ikitajwa kuwa walikuwa wapenzi.


  "Hatukutegemea kama Marehemu Kanumba angeweza kuwa na mahusiano y kimapenzi na binti yetu; kwanza ndiye tuliyekuwa tukimtegemea kwa kiasi kikubwa katika kuendeleza na kukikuza kipaji alichokuwa nacho Elizabeth", alisema baba mtu. "Ninaomba Wanasheria na wanaharakati wa haki za kibinadamu kuingilia suala hili na kusaidia katika kupatikana kwa haki dhidi ya shtaka la mauaji linalomkabili binti yangu Elizabeth na pia naomba swala hili lisichukuliwe kishabiki ama kwa hisia bali haki ichukue mkondo wake"alisema.


  Alisisitiza kuwa jamii inatakiwa kutambua mazingira ya tukio hilo,ambapo chanzo kinasemekana ni ugomvi uliopelekea tafrani kwa Lulu kutuhumiwa kumsukuma Marehemu Kanumba kwa kile kinachodaiwa kuwa ulikuwa wivu wa kimapepenzi na haiyumkini hakukusidua kumuua hivyo yeye anashangaa bintiye kuhusishwa moja kwa moja na mauaji. "Ushiriki wa mwanangu kuhusu mambo ya sanaa nilikwishapata wasiwasi na mama yake mzazi alikuwa akiwasiliana na Marehemu Kanumba enzi za uihai wake ambaye alikuwa anamhakikishia usalama wa Lulu na kusema kuwa ataendele kubaki kama mwalimu…..lakini leo nasikia alikuwa ni mpenzi - nilishtushwa" alisema Kimemeta. Baba Lulu pia ameelezea kusikitishwa kwake kwa kushindwa kuhudhuria mazishi marehemu Steven Kanumba kuhofia usalama wake, na kusema mazingira yatakaporuhusu hata sita kufika nyumbani kwa marehemu Steven Kanumba na kutoa pole. Bw Kimemeta amesema kuwa anaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia ya Marehemu Steven Kanumba na kutoa mkono wa pole kwa msiba huo mkubwa ambao haukutarajiwa.Kasema kuwa Kanumba alikuwa bado ni kijana mdogo aliyeonyesha umahiri kwenye sanaa na kwamba amecha pengo kwa familia yake na Tanzania kwa ujumla.
   
 5. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Hayo ndo matokeo ya kulea kwa rimoti kontrol
  Kama kuna wa kulaumiwa kwa matatizo ya lulu huyu baba lazma awe nambari 1
   
 6. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  pia naomba swala hili lisichukuliwe kishabiki ama kwa hisia bali haki ichukue mkondo wake”alisema. NAUNGA MKONO HAPA
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Apr 13, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Pole baba Lulu.
   
 8. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  hivi tangia lini pole tunawapa wana-JF tu?.....kuna wengi matatizo yao huripotiwa humu jamvini huwa tuna utamaduni wa kuwapa pole..............au una lako jambo?
   
 9. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  hata mimi naunga mkono apewe pole mzee wa watu.......haya yanaweza kumkuta mtu yeyote yule........
   
 10. saragossa

  saragossa JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 2,141
  Likes Received: 148
  Trophy Points: 160
  Pole baba lulu!
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  hata mimi naunga mkono apewe pole mzee wa watu.......haya yanaweza kumkuta mtu yeyote yule........
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 418,988
  Trophy Points: 280
  toa pole tu maneno mengi ya nini?
   
 13. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Pole baba Lulu ngoja tusubiri sheria na haki ikitendeka.

  R.I.P the great, Mwal. WA LULU!
   
 14. Kinyerezi

  Kinyerezi JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 28, 2009
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Pole kwa kufiwa na Mwalimu wa Bintiyo:disapointed:
   
 15. T

  Twinky Senior Member

  #15
  Apr 13, 2012
  Joined: Jun 10, 2010
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Just a question. kama baba Lulu ni mwan JF naamini alikuwa akiona picha za mtoto wake huyo anayemuita mdogo
  kweli kwa mtu mzima huwezi kutafsiri tabia ya mtoto wako katika picha hizo????

  Me sioni kwa nini anashangaa kuskia kuwa alikuwa na uhusiano na Marehemu SK.!! iweje tulio nje tuskie fununu hizo na yeye mzazi awe hajui?? kweli malezi ya remote mabaya!!!!
   
 16. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  wazazi wa siku hizi hawana ibada kwa MUUMBA WAO! Malezi bila sala ni sawa sawa na LULU + JD = ????
   
 17. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #17
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana, lakini hukuonyesha juhudi yoyote kwa jamii kumkanya mwanao alivyokuwa anapamba magazeti kwa ufuska, ulevi na kutembea uchi kwa kipindi cha miaka miwili sasa. Leo mnasema ana miaka 17!!!!!!!!! si mlimsherehesha alipofika miaka 18 na kutangaza kwenye vyombo vyote vya habari kuwa mwanenu sasa amekua na ana uhuru wa kufanya atakalo, AMEFANYA SASA.
   
 18. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 430
  Trophy Points: 180
  mbona hawafanani? atakuwa kabambikiziwa huyo. pole yake lakini.
   
 19. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #19
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,108
  Likes Received: 6,583
  Trophy Points: 280
  Pole ya nini,
  wazazi wanaozaa na kuacha dunia
  iwalelee watoto wanastahili pole ya nini
  kwani magazeti hakuwahi kuyaona hata kusimuliwa hakuwahi kusikia,
  hebu asije na story zake za matonya hapa.
   
 20. J

  JUMONG Senior Member

  #20
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huyo mzee anastahili lawama zote kwa malezi mabovu aliyompa mwanaye binti ambaye hajaolewa anafanya nini kwa wanaume usiku wa manane.Nadhani wazazi wengine nao wapate fundisho katika kuwapa malezi bora vijana wao, huyo mzee anatakiwa kujilaumu yeye mwenyewe na hastahili kupewa pole hata kidogo.
   
Loading...