Ng'wanangwa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2010
- 10,827
- 4,172
Katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar leo alipoitaka NEC iache kutangaza matokeo yaliyochakachuliwa ya Urais, Willbrod Slaa, alitoboa siri kuwa Mpendazoe alipata ushindi wa kura 56,962 jimboni Segerea. Makongoro Mahanga wa CCM alipata kura 43,904.
Ushahidi wa idadi hizi za kura upo kwenye fomu za matokeo ya kura kutoka vituo vya jimbo hilo. Baada ya usalama kuchakachua matokeo, wakaja na matokeo ya kupika yanayo onesha hivi:
Makongoro Mahanga - 43,839
Fred Mpendazoe - 39,639
Huu ndio wizi wa wazi unaofanywa na CCM halafu wanasema Kikwete na chama chake wanashinda kwa kishindo!
Mimi ni msukuma orijino. Mchinga ng'ombe.
Ukiondoa 'k' nendo ishindo ni tusi kubwa tena la nguoni.
Wanawatukana. Munawapigia kura.