Segerea Na Hatma Ya Mabadiliko: Siasa Maji Taka Zisitukwamishe.
Na Ebenezer Kwayu
Jongea Tanzania
Jimbo la Segerea (Dar es Salaam) lina watia nia zaidi ya 20 wa CHADEMA mpaka sasa. Hii ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na uongozi wa chama (kamati tendaji ya Jimbo) kupitia mikutano na waandishi wa habari. Ni jimbo lenye kata 13.
Kati ya hawa watia nia 20, watano (5) ni viongozi wa Jimbo ambao ni wajumbe wa Kamati tendaji ya Jimbo. Hili nililibaini baada ya kufuatilia mwenendo wa chama Segerea kutaka kudadisi sababu za msingi za kutofanyika kwa shughuli za chama.
Kazi za chama na uendeshaji wa chama Segerea umedorora na hii imetokana na uwepo wa mgongano wa maslahi (conflict of interest) miongoni mwa viongozi wa Jimbo hili.
Kutokana na uwepo wa mgongano huu wa maslahi, kumesababisha uwepo wa makundi makuu matatu (3) ya kihasimu.
Kundi la kwanza ni lile linalonasibishwa na viongozi waliopita. Mtakumbuka kwamba baada ya chaguzi za chama za kata na mitaa, uliokuwa unafuata ni uchaguzi wa Jimbo. Lakini Makao Makuu waliengua wagombea waliokuwa wanataka kugombea tena segerea kutokana na kufeli katika ngwe yao ya kwanza ya uongozi. Aliyetaka kugombea nafasi ya Mwenyekiti ni Bw. Mchele.
Bw. Mchele alienguliwa kutokana na kuwa na uhusiano uliokuwa na sura ya hatari kwa chama kati yake na Dr Makongoro Mahanga (Mb) ambaye ndiye mbunge wa sasa wa Segerea kupitia CCM pamoja na Nimrod Mkono mbunge wa Musoma.
Tuhuma alizokuwa nazo ni kuhongwa na Dr Mahanga ili akidhoofishe chama. Lakini pia alihongwa na Nimrod Mkono ili asigombee jimbo la Musoma anakotokea na ambako mbunge wake ni Mzee Nimrod. Na katika harakati zake ndani ya chama kwa sasa, Pesa anazowahonga viongozi wa kata ili wampitishe anazitoa kwa Dr Mahanga na Mzee Nimrod Mkono.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba, Mchele ameacha ualimu alikokuwa akifundisha katika shule ya Kristo Mfalme, lakini anazo pesa za kuwahonga viongozi wetu, anayo magari mapya anayonunua mfululizo na pia nyumba amajenga. Lakini pia amejenga shule yake binafsi. Hakuna kazi wala biashara anayoifanya na hakufundisha zaidi ya miaka mitatu alipokuwa Kristo Mfalme. Wala hakuna taarifa zozote kwamba aliwahi kuokota Tanzanite, Dhahabu, almasi wala vito vingine vya thamani. Anafanya tuu hizi siasa za kuunganisha UKAWA na akina Mahanga na Nimrod.
Hisia zimeibuliwa na kumnasibisha Bw. Mchele na u-CCM kwamba anahongwa na rafiki yake Dr Makongoro Mahanga pamoja na Nimrod Mkono. Hii ni kutokana na kuwa na utajiri bila kuwa na chanzo halisi na halali cha mapato (Wealth Without Work).
Pia, Makao Makuu hawakukurupuka kumuengua huyu Bw. Mchele kwa sababu zipo tetesi (zinazoelekea kuwa ukweli) kwamba Bw. Mchele anaandaliwa na Makongoro Mahanga kugombea kupitia ACT kama hatapitishwa na UKAWA kugombea Ubunge Segerea.
Kwa kuoanisha 'dots' utapata picha kwamba huyu anatumika kudhoofisha chama na harakati za mabadilko Segerea.
Ikiwa atapitishwa na UKAWA, atasaliti, asipopata nafasi ya kusaliti, ataasi kwa kwenda ACT ili kugawa kura ambazo zingetiwa katika kapu la UKAWA.
Lakini hawa walioenguliwa ndio waliokuwa wameshasimamia chaguzi za ngazi zote za chini. Hivyo kazi ya kuwapandikiza watu watakaowasapoti ilikuwa imeshakamilika. Kwa tafasiri na kisiri ya moja kwa moja, ni kwamba hawa walioenguliwa wanayo nguvu kwa viongozi wa kata na mitaa wakiwa nje ya uongozi.
Kutokana na hali hii, viongozi wa kata na mitaa wanakahidi kwa makusudi maagizo ya uongozi uliopo kwa sasa. Wanawasikiliza walioenguliwa maana ndio waliowasimamia na pengine kuwapandikiza katika nafasi za uongozi walizonazo.
Kutokana na kasumba hii iliyojijenga na kustawi Segerea, shughuli za uendeshaji wa jimbo zimekwama.
Kundi la pili ni la viongozi waliopo madarakani kwa sasa. Katibu wa sasa (Bw. Anatropia) na Mwenyekiti wa Chama Segerea wa sasa (Bw. Kidera) hawafanyi kazi kwa pamoja. Hawaaminiani. Wote wanatafuta na kuunda mtandao wa kisiasa (polotical network) ili waweze kushinda kura za maoni. Hii imesababisha kazi na shughuli za ujenzi wa chama kusimama na kuzorota.
Lakini pia imesababisha ugomvi mkubwa na kutoelewana miongoni mwa viongozi hawa. Mathalani, katika mkutano mkuu wa kata za Vingunguti na Kiwalani, Mwenyekiti na Katibu wa chama jimbo la Segerea walionekana kugombana hadharani na kupigana mbele ya viongozi wa mitaa waliofika katika mkutano mkuu wa kata hizo uliokuwa umebeba agenda ya uchaguzi katika kata hizi. Hii ilisababisha kushindwa na kuahirisha uchaguzi na kikao kuvurugika. Mpaka ninapoandika andiko hili, chaguzi hazijafanyika katika kata hizi.
Kama hiyo haitoshi, Katibu wa sasa wa Segerea (Bw. Anatropia) ameunda na anaunda mtandao wa kikabila (tribal network aiming at political victory). Anaposimamia chaguzi katika kata kama Katibu wa Jimbo na Kiongozi wa Kamati Tendaji ya Jimbo, anahakikisha anawashawishi wapiga kura (viongozi wa wa chama wa mitaa) kuwachagua Wahaya. Katika kata ambazo uchaguzi umeshafanyika, anatumia agenda ya ukabila kuwapata wahaya wenzake katika jimbo la Segerea.
Kundi la tatu linalohasimiana na makundi mengine ni kundi la watia nia wasiokuwa na Kundi. Hili nalo ni kundi. Hawa wapo katika hawa waliobaki wasiokuwa na hila wala mauzauza ndani ya chama. Hawa wanapata changamoto moja kubwa.
Hawaruhusiwi na uongozi uliopo (Bw. Kidera na Bw. Anatropia) kufanya kazi za chama. Hawashirikishwi katika kazi yoyote kwa hofu ya kueleweka kwa wapiga kura kuliko wao, (ikitokea kazi ya chama mara moja moja).
Hawa wapo zaidi ya 15. Si viongozi wa Jimbo. Wengine katika hawa pia si viongozi kabisa ndani ya Chama.
Ninaamini hapa ndipo alipo Mbunge wa Segerea mwenye uwezo kusimama kidete dhidi ya huu mfumo wa CCM wa 'Mangi meza'. Wanaopambana na kupigana hadharani mbele ya wanachama na wananchi hawatapewa ridhaa kuongoza Segerea na kuiwakilisha mjini Dodoma.
Wakati Makao Makuu wakitoa tamko na kupuliza kipenga cha kuchukua fomu za kuwania udiwani na Ubunge katika ngazi za kata na Majimbo mbalimbali nchini kuanzia tarehe 18.05.2015 hadi tarehe 20.06.2015, Uongozi wa Jimbo la Segerea haujafanya chaguzi za viongozi wa kata katika kata Sita (6) mpaka sasa ninapoandika makala haya.
Sababu kuu za msingi ziko mbili, kwanza ni uwepo wa makundi haya ya akina Bw. Mchele, Bw. Kidera na Bw. Anatropia. Msuguano unasababisha shuguli za ujenzi wa chama kusimama. Mlolongo (bureaucracy) wa kufanya uchaguzi umefanywa mgumu (complicated) kutokana na mgongano wa maslahi.
Kutokana na kutoaminiana kwa hawa 'mafahali walio hodhi chama', Kwa sasa hakuna mjumbe wa kamati tendaji anayeruhusiwa kwenda peke yake au wawili, watatu katika kata kusimamia uchaguzi wa Viongozi kule. Wanakwenda wajumbe wote wa kamati tendaji ya jimbo. Akikosekana mmoja au wawili (bahati mbaya awe ni mtia nia), kazi zinasimama.
Mwenyekiti wa sasa wa Jimbo (Bw. Kidera) anatuhumiwa kutumia mabavu, akili ndogo na hamasa za lazima kuwaongoza viongozi wenzake wa Kamati Tendaji na Kata za Jimbo. Ugomvi usioisha katika jimbo baina ya viongozi, ngumi mkononi ni tabia ya kipekee ya Mwenyekiti wetu Bw. Kidera.
Kuthibitisha hili, katika chaguzi katika kata za Bonyokwa, Kinyerezi na Kisukuru (anakotokea Bw. Kidera), Kidera alipigana ngumi katika chaguzi hizi kutokana na mgongano wa maslahi miongoni mwa kundi lake na 'Mabwana wakubwa' wengine.
Sababu ya pili ya kushindwa (fail) au kuchelewa kwenye sura ya kushindwa (delay) kufanya chaguzi katika kata hizi sita ni Kufutwa kwa chaguzi zilizofanyika katika baadhi ya kata.
Hii ni kutokana na kambi za viongozi wa sasa kushindwa katika chaguzi hizo. Kata za Liwiti na Kiwalani (ambako ngumi zilipigwa kama nilivyoeleza awali kabisa kati ya katibu na Mwenyekiti ) ni miongoni mwa kata ambazo matokeo yake yamefutwa kutokana na kushindwa kwa kambi hizi mbili zinazohodhi kamati tendaji ya Jimbo la Segerea. Kambi iliyokuwa imeshinda ni ya Mwenyekiti wa Zamani Bw. Mchele kutokana na rushwa kuzidi akina Kidera.
Jimbo la Segera lina kata kumi na tatu (13). Katika kata hizi, ni kata saba (7) tu zimekwisha fanya chaguzi za uongozzli wa chama. Kata sita (6) hazijafanya chaguzi. Kwa tafsiri hiyo, hatuna kamati tendaji katika Kata sita. Hatuna viongozi wa kusimamia mchakato wa upatikanaji wa madiwani.katika kata sita.
Kwa kunasibisha hoja hii na hatma ya chama na matamanio yake, kitakwimu, ni kwamba 46.2% ya kata za Jimbo la Segerea haina uongozi, 53.8% ya kata za jimbo ndiyo yenye uongozi kamili wa chama. Kiulinganishi, nusu ya jimbo haina uongozi. Kwa hoja hii, hata viongozi wa Jimbo walioko hawana sifa za kikatiba (katiba ya chama) za kuendelea kuwa viongozi.
Ni vizuri sasa Kamanda Mabere Marando (Mwenyekiti Wa CHADEMA Kanda) ukajiridhisha mwenyewe kwa uozo ulioko Segerea na umazwazwa unaoendelea kufanyika. Wananchi wa Segerea wako tayari kwa mabadiliko. Wako tayari kuyafanya na kuyagharamia. Tusiwakatishe tamaa watu hawa. Tuwape kiongozi anaefaa. Tuwape mtetezi wa Maslahi, haki na matamanio yao ambaye wamekuwa wakimsubiri kwa zaidi ya nusu karne sasa.
Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki UKAWA, Ibariki CHADEMA.
Nawasilisha.
Cc:
1. Mabere Marando - Mwenyekiti Kanda
2. Dr Willbroad Slaa -Katibu Mkuu Taifa
3. Kamati Tendaji Segerea - Kwa Taarifa.