Ukisoma hapa na ukitafakari majimbo ya Dar lolote linaweza kutokea Oktoba

mpalu

JF-Expert Member
Sep 15, 2010
2,521
870


TEMEKE


Nusura jimbo la Temeke liende mikononi upinzani mwaka 2010, lakini kukosekana kwa maridhiano baina ya vyama vya upinzani kulipelekea CCM kupata ushindi huku vyama vikuu vya upinzani vikigawana kura. Abasi Mtemvu safari hii akipoteza mvuto alishinda kwa asilimia 48.21 = kura 58,339 (akishuka kwa asilimia 12 kulingana na mwaka 2005), kura za CUF zilipungua kwa kiasi kikubwa, kutoka 47,448 mwaka 2005 hadi kura 28,877 = 23.86% mwaka 2010 huku mgombea wa CUF akiwa ni Limbu Kadawi Lucas (Muasisi wa chama cha ADC na sasa Mwenyekiti aliyesimamishwa wa ACT – Tanzania). Kura za CUF ziligawika sana baada ya CHADEMA kumsimamisha Ng’hilly Dickson Amos aliyekuwa wa tatu kwa kura 27,899 = 23.06%.

Wagombea wa vyama vingine 8 walipata asilimia 2.59 ya kura zote. Tutagundua kuwa, matokeo ya jimbo la Temeke kwa mwaka 2010 yangepeleka ushindi kwa upinzani kwa sababu kura za wagombea wa CUF, CHADEMA na vyama vingine 8 zinafanya upinzani kwa ujumla kuwa na asilimia 49.5 dhidi ya 48.21% za CCM.............




KIGAMBONI

Ushindi wa CCM katika jimbo la Kigamboni mwaka 2010 ulipungua kwa asilimia 10 ukilinganisha na mwaka 2005. Dr. Faustine Ndungulile aliipa CCM kura 53,389 dhidi ya kura 25,166 za Komu Maulidah Komu wa CHADEMA na kura 24,419 za Mustapha Ismail wa CUF. Vyama hivi vitatu na asilimia za ushindi wao katika mabano ni CCM (50.07%), CHADEMA (23.06%) na CUF (22.9%). Vyama vingine 9 vilivyoshiriki kwenye uchaguzi huo vikiwemo APPT Maendeleo kilichochukua nafasi ya nne na NCCR Mageuzi kilichochukua nafasi ya 7, vilipata jumla ya kura 2695 zilizofanikisha asilimia 2.52.

KINONDONI
..

Ushindi wa CCM ulipungua kwa kasi mwaka 2010 ambapo wagombea wa CUF na CHADEMA walipata jumla ya kura 50,015 sawa na asilimia 47.88 wakati CCM chini ya Idd Azzan ikipata kura 51, 372 sawa na asilimia 49.18, kwa hiyo katika uchaguzi wa 2010 CCM iliwazidi wagombea wa CHADEMA na CUF kwa kura 1357 sawa na tofauti ya asilimia 1.3.

ILALA

Katika uchaguzi wa mwaka 2010, jimbo la Ilala lilishuhudia ukuaji wa upinzani. Mara hii idadi ya wapiga kura ilishuka na hata ushindi wa mbunge wa CCM aliyetetea kiti chake kwa mara ya pili ulikuwa mdogo. Vyama 11 viliweka wagombea ambapo CCM ikimsimamisha Azzan Zungu ilipata kura 25,940 sawa na asilimia 66.77 na CHADEMA ikaibuka katika nafasi ya pili ikiwa na kura 8,053 sawa na asilimia 20.73 huku CUF ikiwa nafasi ya tatu kwa kura 3,988 sawa na asilimia 10.27. Vyama vingine 8 vilipata jumla ya kura 472 sawa na asilimia 1.22. Uchaguzi huu ulishudia kuporomoka kwa ushindi wa Zungu kutoka asilimia 74.5 mwaka 2005 hadi 66.77 mwaka 2010.

SEGEREA

Mwaka 2010 wakati jimbo la Ukonga lilipogawanywa na Segerea kuzaliwa, Makongoro Mahanga wa CCM alikuja kugombea Segerea na alishinda kura za maoni ndani ya chama chake, safari hii ikionekana angekuwa na kazi nyepesi kwa sababu jimbo la Segerea lina kata chache tu. Uchaguzi wa mwaka 2010 ulikuwa mgumu sana kwa Makongoro Mahanga na CCM. Matokeo ya mwisho yaliyotangazwa yanaonesha alijipatia ushindi mwembamba mno wa asilimia 41.7 dhidi ya asilimia 37.49 za CHADEMA na asilimia 17.94 za CUF. Asilimia hizo zilitokana na kura 43,554 za CCM, kura 39,150 za CHADEMA na kura 18,737 za CUF, ambapo CCM ilimsimamisha Makongoro Mahanga, CHADEMA ikamuweka Fred Tungu Mpendazoe na CUF ikimsimamisha Kimangale Ayoub Musa.

Ndio kusema, kama UKAWA ingekuwepo mwaka 2010, kura za CHADEMA na CUF zingetosha kuipa UKAWA ushindi wa asilimia 55.94 na kuipita CCM kwa asilimia 14.24

UKONGA

Katika uchaguzi wa Mwaka 2010 baada ya Makongoro Mahanga kugombea Segerea, jimbo mama la Ukonga lilibaki peke yake na hivyo kufanya uchaguzi Mkuu kama lilivyo (bila kuhusisha Segerea). Jumla ya vyama 12 viliweka wagombea katika jimbo hili na mvutano mkubwa ulijitokeza kati ya CCM na CHADEMA ambapo mgombea mpya wa CCM Eugen Mwaiposa Elishiringa alijizolea kura 28,000 sawa na asilimia 53.07 ya kura zote huku Binagi James Chacha wa CHADEMA akipata kura 17,059 sawa na asilimia 32.34 ya kura zilizopigwa. Mgombea wa CUF Heko Bethuel Pori alijipatia kura 5,220 sawa na asilimia 9.89. Wagombea wengine kutoka vyama 9 walipata jumla ya kura 1,470 sawa na asilimia 2.8 ya kura zote

UBUNGO
Mwaka 2010 ulikuwa na nuru ya pekee ambapo jimbo la Ubungo liliangukia mikononi mwa CHADEMA, Mgombea wake John Mnyika alipigiwa kura 66,742 sawa na asilimia 49.56 wakati mgombea wa CCM Bi. Hawa Ng’umbi alipata kura 50,544 sawa na asilimia 37.53 na Julius Mtatiro wa CUF alipata kura 12,964 sawa na asilimia 9.63 ya kura zote.

KAWE

Katika kinyang’anyiro hicho kilichowakutanisha kina mama wawili dhidi ya mwanasiasa maarufu na nguli mhe. James Francis Mbatia wa NCCR, nyota ya Bi. Halima Mdee wa CHADEMA iling’ara na akapata ushidi wa kura 43,365 sawa na asilimia 43.17 akifuatiwa na mwanamama mwenzie Bi. Angela Kizingha wa CCM aliyepata kura 34,412 sawa na asilimia 34.26 huku James Mbatia wa NCCR na Mapeyo Shaabani wa CUF kwa pamoja wakipata kura 21,091sawa na asilimia 21, na wakati huohuo, vyama vingine 5 vilivyoweka wagombea katika uchaguzi huo vikiambulia kura 1528 sawa na asilimia 1.58 ya kura zote




source: MTATIRO facebook page
Last edited by mpalu; Today at 15:00.​
 
Back
Top Bottom