Mpendazoe aanika walioanzisha CCJ

Ndio ni ushujaaa..... Ni kama kutoka kwenye shimo la choo na kuanza kupata hewa fresh...CCM is terrible rotten!
 
mafilili hawa jamaa wanakulipa sh ngapi kwa kila post humu jf?

Suala si malipo, naaangukia upande wa uhalisia wa jambo husika. CDM bado ni kichanga kisera na mikakati, naguko lake laja muda si mrefu; mnatumia muda mwingi kuwajadili akina Nape. CDM mlianza vizuri kwa hoja zenye shibe, hatahivyo baadaye HASWA baada ya ujio wa Nape na hoja zake, mkatoka nje ya reli na kuangaza hotuba za kutaja watu badala ya hoja muafaka za kupaisha taifa kimaendeleo kwa mfano majuzi unaitisha mkutano wa hadhara Tunduru ambako wananchi wana shida lukuki, CDM walitumia robo tatu ya mkutano kuelezea namna CCJ ilivyoazishwa na kuachwa kwenye mataa na akina Nape. Zamani mkutano kama ule CDM ukitoa majibu wa wananchi namna ya kutatua tatizo la soko la korosho haswa stakabadhi ghalani HAPO wanatunduru wangewaelewa, mbaya zaidi wakaona haitoshi robo tatu ya hotuba wakamshambulia kipenzi cha wanatunduru Lipumba. HIVYO CDM MRUDI MLIKOTOKA KWENYE SIASA ZA MVUTOI KULIKO KULUMBANA NA AKINA NAPE; WANANCHI WATAWAPOTOZEA!!!
 
Kusema kweli Mpendazoe angewataja kina Nape na Sitta napema isingekuwa na political significance. Sasa ni wakati muafaka kutokana na siasa zilizopo hasa ndani ya CCM. Mbinu ya Chadema ni kuwavuruga zaidi CCM maana sasa kina Lowasa nao wamepata silaha ya kuwarudi kina Sitta na Mwakyembe. UVCCM nao wapepata silaha dhidi ya Nape amabaye tayari alishaanza kuwakoga na cheo kipya. Sasa JK anaweza "kujivua" kambi zote zinazopingana CCM bila kunyoshewa kidole na yeyote. Vita ya panzi ni furaha ya kunguru. Mpendazoe oyee!

Aiseee, Kumbe!
Hii yamaanisha kuwa CDM wanaendesha vitu vitatu kwa mkupuo; wanajiendesha wao, waiendesha ccm na wanaiendesha serikali kwa kupitia msukumo wa hoja za kitaifa. Nikiri, hili nilikuwa sijaling'amua kabisa.
 
Mpendazoe inaelekea ni mweupe kichwani.Ni mtu wa kushikwa masikio na rahisi sana kutumika.Ukimsoma vizuri Mwakyembe,utaelewa jinsi hii move ilivyokuwa
 
Chadema nimewakubali,wanafuata ule msemo usemao adui mwombee njaa.Chadema sasa wanaichakaza ccm kila kona yaani mpaka uchaguzi mkuu ujao ccm watakuwa nyang'anyang'a.Nawaonea huruma ccm maana muda wao wa kufa unakaribia kwani mpaka sasa hivi wapo chumba cha wagonjwa mahututi wa wanapumulia mashine.
 
Mheshimiwa Raisi wetu JK SASA ndio muda muafaka wa kuondoa magamba yote yaliokifikisha chama chetu hapo kilipo , KAMBI ZOTE MBILI ZINAZOKIVURUGA CHAMA wanastahili kutimuliwa kwa kulea makundi kama ifuatavyo:

Lowasa na kundi lake ,Sitta na kundi lake naamini CDM watakuwa wamekosa cha kuongea kwenye hayo maandamano yao yasiyokuwa na kichwa wala miguu
Sasa Kikwete akiyaondoa makundi hayo CCM itabaki na nani Dr.Sheni.
 
JK mungu anampenda sana kwani moja ya makundi yaliyokifikisha ccm hapa ilipo ni kundi la Sitta na Lowassa . Ni wakati muafaka sasa kuyafutilia mbali haya makundi kwani kila kundi ni hatari kwa uhai wa Chama. Naamini CDM WATAKOSA cha kuongea kwenye haya maamdamano yasiyokuwa na kichwa wala miguu
Nauliza ayafutilie mbali nani abaki CCM? kuyatoa haya makundi ni sawa na mwenye ukimwi kubadili damu yote akitegemea viini vitakwisha lakini ndiyo anakaribisha kifo.
 
Baada ya Kada mwandamizi wa CDM Fred Mpendazoea kuanika siri za vigogo wa CCM Zinazowahusisha na mipango ya kuwahi kukigeuka chama chao na kuanzisiha ccj, jana Fred Mpendazoea aliwataja wahariri na waandishi wa habari ambao walikuwa ni waasisi wakuu wa CCJ,waandishi waliotajwa na Mpendazoea na vyombo vya habari wanavyotoka ni Ramadhani Semtawa(Mwananchi) ,Muhingo Rweymamu(Habari Corporation), Mayage S Mayage (Habari Corporation) .
Amesisitiza kuwa ndio walikuwa waasisi wakuu wa CCJ

Kwakweli mimi binafsi ni msomaji mzuri sana wa gazeti la mwananchi, lakini habari zinazoandikwa na huyu mkulu huwa zinashangaza.

Ahsante sana Mpendazoe kwa kutujulisha ukweli wa kiwavi ndani ya gazeti la mwananchi, hao wengine wa habari corporation tulikuwa tunawafahamu rangi zao siku nyingi.
 
RIP na Upupu wako,unapotaka kumumng'oa adui huwezi weka mambo bayana na hata sababu ya kutosajiliwa CCJ ilikuwa ni zengwe na worry ya CCM dhidi ya CCJ na Mpendazoe anasema lengo ilikuwa waje waungane na CDM ilikuing'oa CCM sasa unaposema alikuwa msiri na hata akiona CDM kama mambo hayaendi sawa anaweza kuanzisha movement za mabadiliok kupitia chama kingine amabcho ki-mtazamo wake kitakuwa na malengo sawa na anavyoamini na hii ni kwa mtu yeyote makini sio Mpendazoe tu!

Ukipenda zoa zoa!!!!:dance::dance::dance:
Haaaa! CDM inapaswa kuwa makini wasipokee wanasiasa uchwara (makapi) why! kada anayehama chama kimoja kwenda kingine hapo pana jambo,unamkumbuka Lyatonga???? kwa nn mtikila anakufa na DP yake??? Hayo anayosema kwa nn hakusema kabla,cdm lazima kuwatazama kwa macho mekundu hawa, wanataka chip-popularity!! wataharibu reputation ya cdm?yaonekana hata Dovutwa akija cdm itampokea???:A S 103:

Je wajua kinachompata mkimbizi anayehamahama kambi ovyo ovyo !!!!!:pound::pound::pound:
 
Suala si malipo, naaangukia upande wa uhalisia wa jambo husika. CDM bado ni kichanga kisera na mikakati, naguko lake laja muda si mrefu; mnatumia muda mwingi kuwajadili akina Nape. CDM mlianza vizuri kwa hoja zenye shibe, hatahivyo baadaye HASWA baada ya ujio wa Nape na hoja zake, mkatoka nje ya reli na kuangaza hotuba za kutaja watu badala ya hoja muafaka za kupaisha taifa kimaendeleo kwa mfano majuzi unaitisha mkutano wa hadhara Tunduru ambako wananchi wana shida lukuki, CDM walitumia robo tatu ya mkutano kuelezea namna CCJ ilivyoazishwa na kuachwa kwenye mataa na akina Nape. Zamani mkutano kama ule CDM ukitoa majibu wa wananchi namna ya kutatua tatizo la soko la korosho haswa stakabadhi ghalani HAPO wanatunduru wangewaelewa, mbaya zaidi wakaona haitoshi robo tatu ya hotuba wakamshambulia kipenzi cha wanatunduru Lipumba. HIVYO CDM MRUDI MLIKOTOKA KWENYE SIASA ZA MVUTOI KULIKO KULUMBANA NA AKINA NAPE; WANANCHI WATAWAPOTOZEA!!!

my friend that is POLITICAL SCIENCE! kwa taarifa yako CDM inakubalika mpaka MBINGUNI
 
Hii move ya CDM inaweza isieleweke kwasasa ila amin amin nawambia CCM wakimaliza kujivua gamba la mafisadi (kama wataweza) kinachofuata ni kujivua gamba la wasaliti (CCM-J) former CCJ. Ngoja tuone...!
 
Miundobinu ya ki-intellijensia itawamaliza cdm take note!!! Hao wanaohamia ni sawa nyuki je mnawabusu na kukumbatia!! Tzm huo ni muundombinu wa chombo ndani ya cdm??? wanajikusanya marando,shibuda,safari,mpenda zoa itakapoanza conflict of interest and option!!! wake up !!!! Msipoteze dira kwa kutokuwa makini! Malumbano si siasa pevu kwenu!!

MSIWE DODOK!!!!! Know who you are!!!:smow:
 
Haitatokea.Unadhani Kikwete/CCM walikuwa hawawafahamu hao jamaa wa CCJ?
 
Miundobinu ya ki-intellijensia itawamaliza cdm take note!!! Hao wanaohamia ni sawa nyuki je mnawabusu na kukumbatia!! Tzm huo ni muundombinu wa chombo ndani ya cdm??? wanajikusanya marando,shibuda,safari,mpenda zoa itakapoanza conflict of interest and option!!! wake up !!!! Msipoteze dira kwa kutokuwa makini! Malumbano si siasa pevu kwenu!!

MSIWE DODOK!!!!! Know who you are!!!:smow:

Nyuki hapigwi busu huna hoja wewe
 
Kama CCJ ingesajiliwa kwa kuwa haikusajiliwa ndio maana kaingia CDM, yeye ni mtu makini kwani aliamua kuacha madaraka na kuamua kusimamia ukweli, CCM wakamwibia kura ili kumkomesha lakini mwisho wa ubaya aibu! Siku si nyingi CCM watajuta kwa dhuluma zao
 
*Yumo pia Mbunge Victor Mwambalaswa
*Watajwa kuwa ndiyo waanzilishi wa CCJ
*Mwingine alibana fedha za pango, samani
*Nape adaiwa kuwa ndiye mtunzi wa Katiba
Na Mwandishi Wetu, Njombe
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendeleza mashambulizi dhidi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na safari hii kimewataja vigogo wanne kinaodai walishiriki kuanzisha Chama Cha Jamii (CCJ).
Mmoja wa makada wa Chadema, Fred Mpendazoe, ndiye aliyevishwa dhima ya kuwataja vigogo hao. Alitaja majina yao katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Njombe, jana.
Waliotajwa kwamba walihusika kuanzisha CCJ ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta; Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa (CCM); na Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye.
Alisema yeye alikuwa pamoja na viongozi hao wakati wa kuanzishwa kwa CCJ, na walikubaliana kuwa kwa pamoja waihame CCM.
Hata hivyo, kwa kile alichokiita kuwa ni unafiki wa viongozi hao, alitelekezwa na wenzake hao na kujikuta akijitangaza yeye peke yake kuwa ni mwanachama wa CCJ.
Wakati akihamia CCJ, Mpendazoe alikuwa Mbunge wa Kishapu mkoani Shinyanga kupitia CCM. Kwa kuhamia CCJ, alipoteza ubunge.
"CCM wanafiki, ndani ya CCM ni unafiki, hawa watu walianzisha chama kingine, sasa wengine ni wabunge, wengine mawaziri na wengine viongozi ndani ya CCM, ni wanafiki.
"Tulikubaliana tuhame wote, lakini kwa sababu ni wanafiki, hawakuondoka kama mimi," alisema na kushangiliwa.
Aliongeza, "Nape anajifanyaje mzalendo wakati alianzisha chama kingine?"
Alisema mmoja wa viongozi hao aligoma kujiunga CCJ, lakini akabaki na fungu nono la fedha zilizokuwa zimetolewa na wafadhili kwa ajili ya kuendeshea chama.
Alisema fedha hizo zilikuwa maalumu kwa ajili ya kulipia kodi ya pango la ofisi na ununuzi wa samani. Hakutaja kiasi cha fedha kilichotafunwa na kigogo huyo.
Alirejea kauli aliyoitoa hivi karibuni kwa kusema kwamba Nape ndiye aliyejihusisha na ukusanyaji katiba za vyama mbalimbali barani Afrika ili kupata katiba ya CCJ iliyo bora zaidi.
Nape anadaiwa kwamba baada ya kushindwa kwenye kura za maoni katika Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam, alikwenda Chadema kuomba apewe nafasi ya kuwania nafasi hiyo kupitia chama hicho cha upinzani.
Mwanasheria na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando, wiki iliyopita alisema kwamba chama hicho baada ya kutafakari, kiliona Nape hana sifa za kumzidi John Mnyika, aliyekuwa amepitishwa kuwania ubunge na hatimaye kushinda.
Kwa upande wake, Nape alikanusha madai hayo na kusema kwamba Chadema ndiyo waliokuwa wa kwanza kumfuata ajiunge nao baada ya kushindwa kwake kwenye kura za maoni.
Tangu awali, kulikuwapo maelezo ya wazi mitaani kwamba Sitta na Mwakyembe ni miongoni mwa waanzilishi wa CCJ. Hata hivyo, viongozi hao mara kadhaa walinukuliwa wakipuuza madai hayo.
Wakati CCJ inaanzishwa, Sitta alikuwa Mbunge wa Urambo Mashariki na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Dk. Mwakyembe alikuwa Mbunge wa Kyela; ilhali Mwambalaswa alikuwa Mbunge wa Lupa. Wote bado wanashikilia nafasi za ubunge kwenye majimbo yao.
Aidha, Sitta na Mwakyembe wakiwa bungeni walikuwa miongoni mwa kundi lililojipambanua kama wapambanaji wa ufisadi wakitiwa nguvu na wabunge kama Mpendazoe.
MTANZANIA lilikuwa gazeti la awali kabisa kuandika kuwa CCJ kilikuwa chama kilichokuwa kimeasisiwa na vigogo kutoka ndani ya CCM. Kuandikwa kwa habari hizo kulielezwa na wachunguzi wa mambo kuwa ndiko kulikotibua mipango ya vigogo wengi kujitangaza hadharani.
 
UOTE=nngu007;1981872]

*Yumo pia Mbunge Victor Mwambalaswa
*Watajwa kuwa ndiyo waanzilishi wa CCJ
*Mwingine alibana fedha za pango, samani
*Nape adaiwa kuwa ndiye mtunzi wa Katiba

Na Mwandishi Wetu, Njombe
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendeleza mashambulizi dhidi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na safari hii kimewataja vigogo wanne kinaodai walishiriki kuanzisha Chama Cha Jamii (CCJ).
Mmoja wa makada wa Chadema, Fred Mpendazoe, ndiye aliyevishwa dhima ya kuwataja vigogo hao. Alitaja majina yao katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Njombe, jana.
Waliotajwa kwamba walihusika kuanzisha CCJ ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta; Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaswa (CCM); na Katibu wa Uenezi na Itikadi wa CCM, Nape Nnauye.
Alisema yeye alikuwa pamoja na viongozi hao wakati wa kuanzishwa kwa CCJ, na walikubaliana kuwa kwa pamoja waihame CCM.
Hata hivyo, kwa kile alichokiita kuwa ni unafiki wa viongozi hao, alitelekezwa na wenzake hao na kujikuta akijitangaza yeye peke yake kuwa ni mwanachama wa CCJ.
Wakati akihamia CCJ, Mpendazoe alikuwa Mbunge wa Kishapu mkoani Shinyanga kupitia CCM. Kwa kuhamia CCJ, alipoteza ubunge.
CCM wanafiki, ndani ya CCM ni unafiki, hawa watu walianzisha chama kingine, sasa wengine ni wabunge, wengine mawaziri na wengine viongozi ndani ya CCM, ni wanafiki.
Tulikubaliana tuhame wote, lakini kwa sababu ni wanafiki, hawakuondoka kama mimi, alisema na kushangiliwa.
Aliongeza, Nape anajifanyaje mzalendo wakati alianzisha chama kingine?
Alisema mmoja wa viongozi hao aligoma kujiunga CCJ, lakini akabaki na fungu nono la fedha zilizokuwa zimetolewa na wafadhili kwa ajili ya kuendeshea chama.
Alisema fedha hizo zilikuwa maalumu kwa ajili ya kulipia kodi ya pango la ofisi na ununuzi wa samani. Hakutaja kiasi cha fedha kilichotafunwa na kigogo huyo.
Alirejea kauli aliyoitoa hivi karibuni kwa kusema kwamba Nape ndiye aliyejihusisha na ukusanyaji katiba za vyama mbalimbali barani Afrika ili kupata katiba ya CCJ iliyo bora zaidi.
Nape anadaiwa kwamba baada ya kushindwa kwenye kura za maoni katika Jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam, alikwenda Chadema kuomba apewe nafasi ya kuwania nafasi hiyo kupitia chama hicho cha upinzani.
Mwanasheria na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Mabere Marando, wiki iliyopita alisema kwamba chama hicho baada ya kutafakari, kiliona Nape hana sifa za kumzidi John Mnyika, aliyekuwa amepitishwa kuwania ubunge na hatimaye kushinda.
Kwa upande wake, Nape alikanusha madai hayo na kusema kwamba Chadema ndiyo waliokuwa wa kwanza kumfuata ajiunge nao baada ya kushindwa kwake kwenye kura za maoni.
Tangu awali, kulikuwapo maelezo ya wazi mitaani kwamba Sitta na Mwakyembe ni miongoni mwa waanzilishi wa CCJ. Hata hivyo, viongozi hao mara kadhaa walinukuliwa wakipuuza madai hayo.
Wakati CCJ inaanzishwa, Sitta alikuwa Mbunge wa Urambo Mashariki na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Dk. Mwakyembe alikuwa Mbunge wa Kyela; ilhali Mwambalaswa alikuwa Mbunge wa Lupa. Wote bado wanashikilia nafasi za ubunge kwenye majimbo yao.
Aidha, Sitta na Mwakyembe wakiwa bungeni walikuwa miongoni mwa kundi lililojipambanua kama wapambanaji wa ufisadi wakitiwa nguvu na wabunge kama Mpendazoe.
MTANZANIA lilikuwa gazeti la awali kabisa kuandika kuwa CCJ kilikuwa chama kilichokuwa kimeasisiwa na vigogo kutoka ndani ya CCM. Kuandikwa kwa habari hizo kulielezwa na wachunguzi wa mambo kuwa ndiko kulikotibua mipango ya vigogo wengi kujitangaza hadharani.[/QUOTE]
WANAFIKI SANA HAO,WANA NIDHAMU YA UOGA-NA UCHU WA MADARAKA.WALIJIFANYA WAPIGANAJI LEO WAMEPIGWA PLASTA MIDOGO.
 
Inawezekana serikali na CCM walikuwa na tetesi ya watu wanaoanzisha Chama cha CCJ. Huenda mpango huo ulipojulikana, ndio maana Kikwete akampa Cheo cha UDC Nape Mnauye ili kumrithisha na hivyo kuvunja nguvu za uanzishwaji wa Chama hicho kilichofutwa. Pia anaonekana ni kijana mwenye ushawishi mkubwa. Pia mizengwe ya kumwondoa Samweli Sitta kwenye Uspika ni jitihada nyingine za kutompa nafasi ya ushawishi aliokuwa nao kwa umma na kuishia kumpa Uwaziri na Mwakiembe ili wawe busy na mambo ya serikali na kuwafumba midomo.
Hayo ni mawazo yangu na tafsiri yangu kwa yanayojilia baada ya Mpendazoni kutoboa siri.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom