Mpendazoe aanika walioanzisha CCJ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpendazoe aanika walioanzisha CCJ

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tores, May 17, 2011.

 1. Tores

  Tores JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 425
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 45
  [​IMG]

  KADA wa Chadema, Fred Mpendazoe amewataja mawaziri wawili wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, mbunge mmoja wa CCM na makada wengine wawili wa chama hicho tawala kuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa katika harakati za kukihama na kujiunga na CCJ.

  Mpendazoe ambaye alikuwa kada wa kwanza wa CCM kuhamia CCJ wakati huo akiwa Mbunge wa Kishapu, aliwataja waanzilishi hao wa CCJ kuwa ni pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri mmoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

  Kwa mujibu wa Mpendazoe, katika kundi hilo pia wamo kada wa Jumuia ya Umoja wa Vijana wa CCM na mbunge mmoja kutoka Mkoa wa Mbeya. Hatukuandika majina ya baadhi ya viongozi waliotajwa kwa sababu hatukufanikiwa kuwapata kujibu tuhuma hizo.


  Hata hivyo, Sitta alipipogiwa simu alisema asingeweza kuzungumza lolote kuhusu madai hayo akisema anasubiri kusoma alichosema Mpendazoe.

  Mpendazoe aliwataja makada hao jana wakati akihutubia umati uliokusanyika kwenye Viwanja vya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Njombe Mjini katika mkutano wa hadhara wa Chadema.


  "Nilipoondoka CCM mimi nilikuwa ni mmoja wa waanzilishi wa CCJ, lakini wengine walikuwa hawajulikani na leo nitawataja hao wengine kwa kuwa CCM inajidai kujivua gamba ili kuwadanganya wananchi," alisema Mpendazoe.

  Alisema hao aliowataja ndiyo waliotaka kukihama CCM, lakini walibaki si kwa ajili ya maslahi ya Taifa, bali ni kwa maslahi yao binafsi.

  "Sitta na (makada wengine) wameingia katika Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, lakini ni wasaliti na Serikali ya CCM ya sasa haiwezi kuwasaidia Watanzania," alisema na kuongeza:


  "Wamevaa ngozi ya kondoo kwa kupinga ufisadi kwa maslahi yao, lakini leo bado wako pale."

  Akizungumza katika mkutano huo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema viongozi wa CCM ni wanafiki na ndiyo maana, hawaelewi wanachokifanya zaidi ya kuwadanganya wananchi.

  Aliitaka serikali kuacha ubabaishaji na kuchukua hatua zinazoweza kuwaletea wananchi maendeleo na kuliinua Taifa.


  Dk Slaa alitumia nafasi hiyo kumshambulia Spika wa Bunge, Anne Makinda. Aliwahoji wakazi wa Njombe waliohudhuria mkutano huo kama uspika wake unawasaidia chochote na wao wakajibu kwa kupiga kilele: "Hakuna chochote."

  "Nilipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, niliwahi kukagua Njombe na miradi yenu nikagundua kuwa hakuna maendeleo yoyote ikiwamo kituo cha basi cha Njombe ambacho hakifai," alisema Dk Slaa.


  Alisema kutokana na kuendelea kumpigia kura kwa muda mrefu, wananchi hao wataendelea kunyanyasika na familia ya mbunge wao itaendelea kuneemeka kwa kutumia mgongo wao.

  Mukama: Chadema kiache ubabaishaji


  Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilson Mukama amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuacha kile alichodai kuwadanganya wananchi kwamba CCM kujivua gamba si kitu akisema hatua hiyo imefikiwa kukiimarisha chama baada ya kutambua kuwa bila hivyo nchi itayumba.

  Mukama alisema hayo kwa nyakati tofauti juzi na jana katika Kijiji cha Kibara, wilayani Bunda na katika Kijiji cha Kaburabura, wilayani Musoma katika mikutano ya hadhara, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nane mkoani Mara.

  Alisema CCM kimetumia dhana hiyo ya kujivua gamba ili kiweze kurudi kwenye misingi imara, ikiwa ni pamoja na kufanya mabadiliko makubwa, hali ambayo itakiweka kwenye mstari unaotakiwa ambao lengo lake ni kuhakikisha kuwa wananchi wanapata maendeleo na huduma zote muhimu.


  Alisema anawashangaa wapinzani wanaotumia muda mrefu kujadili falsafa ya kujivua gamba na kuhoji uwezo wao katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

  Alisema amesikitishwa na kauli ya viongozi wa Chadema kwamba kuna uwezekano Rais Kikwete kuondoka madarakani kabla ya 2015 kwa kutolea mfano wa Waziri Mkuu wa Japan aliyeondolewa madarakani.


  Alifafanua kuwa viongozi wa Chadema wanatakiwa kufanya uchunguzi kabla ya kutoa matamko kwa maelezo kuwa Waziri Mkuu wa Japan hawezi kufananishwa na Rais Jakaya Kikwete kwa vile aliwekwa madarakani na Bunge wakati Rais alichaguliwa na wananchi.

  Alisema kuwa, hata Mwalimu Julius Nyerere enzi za uhai wake aliwahi kutamka kuwa, bila CCM ya kweli nchi itayumba na kwamba ndiyo maana chama hicho kimeamua kutumia dhana hiyo ya kujivua gamba ili kiweze kuwa imara na kinachoweza kusimamia maendeleo ya wananchi.


  "Tunakiweka katika misingi ya kukiimarisha ili kiwe chombo imara ambacho kweli kinaweza kusimamia maendeleo katika maeneo yetu tunayoishi. Sasa hawa Chadema wameichukua dhana hiyo ya kujivua gamba visivyo kabisa," alisema.


  Alisema hiyo inatokana na viongozi wa Chadema kuwa na tabia ya kurukia mambo bila kuyafanyia uchunguzi na kwamba wameichukua dhana hiyo visivyo na kuendelea kuwarubuni wananchi ili wakichukie CCM na serikali yao... "Hawa wanataka kwenda Ikulu kwa maneno ya udanganyifu kabisa na maandamano yasiyokuwa na msingi wowote."


  Pia alisema kuwa CCM haiwezi kufa kama upinzani wanavyoendelea kuwaambia wananchi, kwani ni chama kikubwa, taasisi na si kampuni ya kibiashara.

  Aidha, Mukama amekiponda Chadema ambacho kimekuwa kikidai kwamba CCM imekumbatia wafanyabiashara na kueleza kuwa Chadema ndicho kinayofanya hivyo."Sasa watu wanaokumbatia sera ambazo mwalimu alikuwa anazipinga, eti ndio wanakwenda kwenye kaburi pale wanasema tunakuomba leo utusikilize tuweze kutawala nchi hii kidogo," alisema.


  Alisema CCM kina matajiri wachache ambao wanataka kukitumia kwa ajili ya kujinufaisha na kuonya kuwa wafanyabiashara ambao maadili yao hayaendani na chama chao wataondolewa na kuwekwa pembeni mara moja.


  Amewataka wakuu wa wilaya nchini na viongozi wa CCM, kusimama imara na kuhakikisha fedha za miradi mbalimbali zinazoletwa na Serikali katika halmashauri husika, zinafanya kazi iliyokusudiwa na si kuishia kwenye mikono ya wajanja wachache.


  Alisema kuwa ni lazima wakuu wa wilaya pamoja na viongozi wa chama hicho watekeleze wajibu wao ipasavyo wa kusimamia fedha za Serikali zinazopelekwa kwenye halmashauri.Habari hii imeandaliwa na Boniface Meena, Njombe; Ahmed Makongo na Christopher Maregesi, Bunda na Beldina Nyakeke, Musoma Vijijini.
   
 2. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Lisemwalo lipo kama halipo basi laja
   
 3. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Mmhu! Tutasikia mengi mwaka huu
   
 4. Kajuni

  Kajuni JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2011
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 45
  Just window shopping.....
   
 5. M

  Marytina JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Nape!jiwe lisiloweza kuvunja yai
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ndio kwanza May hadi ije ifike December watu watakuwa wameparangana mpaka basi
   
 7. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mukama ni lini mtachukua hatua ya kuwaondoa wenye magamba si kila siku mnaimba tu eti waondolewa tuambieni lini????? acheni propaganda hizo
   
 8. k

  kabombe JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 15,635
  Likes Received: 8,596
  Trophy Points: 280
  Wakati ule alibembelezwa awataje akagoma,kwa sasa ni wrong time.Ni sawa na hadithi za kufikirika.Mi namuona sawa tu huyo Nape.Je CCJ ingeandikishwa angekua CDM?
   
 9. M

  Mwana Mnyonge JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 346
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Mpendazoe amewalipua spika aliyepita samwel sitta na mbunge wa kyela naibu waziri herrison mwakyembe kuwa ndio waanzilishi wa ccj

  source, magazeti ya leo naomba kuwasilisha
   
 10. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #10
  May 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  gazeti gani mimi mbona sijaona?
   
 11. Mlengo wa Kati

  Mlengo wa Kati JF-Expert Member

  #11
  May 17, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 2,733
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mpendazoe aliwahi kuulizwa kama yeye ni mwanzilishi wa CCJ akasema hapana,leo anasema yeye ni miongoni mwa Wanzilishi! Hopeless kabisa!
   
 12. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #12
  May 17, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ni ngumu kuamini, kuanzisha chama kwa malengo ya muda mfupi sio rahisi.
   
 13. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #13
  May 17, 2011
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  napita nitarudi
   
 14. A

  AlamaZA NYAKATI JF-Expert Member

  #14
  May 17, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 274
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ccm jibuni hoja kuwa akina nape. sita na mwakyembe si wasaliti kwa kuandaa mipango ya kuhama ccm????
   
 15. Charles Mtekateka

  Charles Mtekateka Verified User

  #15
  May 17, 2011
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 310
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Pata nakala ya leo ya MWANANCHI na NIPASHE!
   
 16. T

  The Priest JF-Expert Member

  #16
  May 17, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hawa wanasiasa wananichanganya hata siwaelewi..huyu mpendazoe nae anakurupuka sana.
   
 17. M

  Mwana Mnyonge JF-Expert Member

  #17
  May 17, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 346
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  gazeti la mwananchi mtanzania na tanzania daima
   
 18. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #18
  May 17, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kujivua gamba ni dhana?
   
 19. I

  Idofi JF-Expert Member

  #19
  May 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 1,542
  Likes Received: 820
  Trophy Points: 280
  CCJ hoyee
   
 20. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #20
  May 17, 2011
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Acha kulinganisha mbingu na dunia, Mpendazoe yeye alionesha kwa vitendo kwamba alifanya yale aliyokua anayaamini kwa kuondoka CCM na kuacha ubunge wake. Hao wengine ni wanafiki tu baada ya kuahidiwa vyeo wakagoma kutoka walikua mavuvuzela tu wanatafuta nafasi kwa kujifanya kwamba wanapinga ufisadi kumbe hakuna kitu.

  Hu ndio muda wakuwaanika wanafiki ili umma ujue wapiganaji wa kweli ni wapi na wanaopigania matumbo yao ni wapi? Go Mpenda, go waumbue
   
Loading...