MPASUKO mkubwa CCM, Juhudi za Kimataifa zinahitajika kukinusuru!

Sikio la kufa halisikii dawa! Kama falme zilivyoinuka na kuanguka, anguka kuu la ccm limekaribia! Chama kimekiuka miiko, kimewasahau wakulima na wafanyakazi, kimekumbatia mafisadi, na kinazima kila njia ya sauti ya wanyonge kusikika. Huwezi kujenga nyumba imara yenye msingi dhaifu!
Umehitimisha vizuri juu ya usaliti wa ccm kwa wakulima na wafanyakazi. Usaliti huu ulianzia baada ya chama kuwaweka pembeni wenye chama na kununuliwa na wafanyabiashara wenye kutaka kulinda maslahi yao.

Shida iliyo mbele yetu ni hii, kumnyang'anya tonge la ugali anayekula huleta patashika ya hapa na pale iwezekana hata mapigano. Hawa watu wanataka kuendelea kula ugali wao huku watu wengine wakiendelea kuwa watazamaji!

Watazamaji walio wengi sana, nao walishachoka kuwa watazamaji.
 
Uzuri wa Lowasa anajua kucheza na mbongo za magamba! Muda si mrefu atawaformat vichwa vyao na watasahau yote yaliyopita maana watayaita yaliyopita si ndwele.
Na watakapo yaita kuwa si ndwele m4c itakuwa imezibua shampeni na kizibo kinadondokea magogoni.

Si walitoa Azimio la Bagamoyo kwamba rais ajaye hatatoka kaskazini?
 
Mpasuko wa CCM kweli unahitaji usuluhishi wa PLO au Frelimo? Mnapoandika uzushi angalia unachoandika sio FRERIMO ni FRELIMO

Chama
Gongo la mboto DSM

Mkuu chama tutasikia mengi kuelekea uchaguzi mkuu bahati nzuri JF ni bahari inapokea kila kitu.
 
Last edited by a moderator:
Si walitoa Azimio la Bagamoyo kwamba rais ajaye hatatoka kaskazini?

Hilo azimio la Bagamoyo ndilo lilo asisi kundi la vijana nililolitaja hapo, na lilipewa baraka zote toka kwa mwenyekiti na likaahidiwa usaidizi,
 
I do not claim to know every member of the Nyerere family. But I assume wewe upo katika familia ya Nyerere? Huu mpasuko wa Lowassa ,Sita na Membe,na sijui nani mwingine;kwa vile CCM wanafanya mambo yao kisiri,kwa nini tusisubiri kuona uchaguzi wa CCM chairman baadaye mwaka huu?
 
Hali ndani ya ccm imezidi kuwa mbaya na ambayo haijawahi kutokea tangu kuundwa kwa chama hiki tangu mwaka 1977,

WAHAFIDHINA ndani ya ccm wameapa kuwa hawapo tayari kuona ccm ikishindwa Uchaguzi ujao, na wapo tayari kufia miguuni kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tz,

Taarifa za ndani na zakuaminika zinasema mpasuko wenye kutishia hata usalama wa nchi yetu,umeanzaa baada ya Lowassa kulazimishwa na wanausalama kuhudhuria UGAWAJI wa ng'ombe pale Monduli ulioratibiwa na kusimamiwa na Rais Jakaya Kikwete!

Kimsingi inasemekana Lowasa alishaapa kutokaa meza moja na JK, hivyo kitendo cha kulazimishwa kuwepo na kuamuliwa kutoa kauli ya kumsifu jk imemkera sana yeye na wanamtandao wake ndani ya ccm na wamepanga kufanya UASI mkubwa ndai ya CHAMA na ikibidi wanasema (nje ya chama)!

Wakati hilo likijiri kambi ya Samweli Sita nayo imechukizwa sana na hatua ya JK kukaribiana na Lowasa kwani wanasema kitendo cha JK kuwa (maadui) kilikuwa kikiwasaidia wao kujijenga kisiasa na kutimiza malengo yao ya Urais 2015

Hawa nao wanatafakari hatua za kuchukua na inatajwa kuna vikao vya siri vimekuwa vikifanyika Tabora na Masaki vikiratibiwa na wanamtandao wa Sitta!

Kundi lingine ni la Waziri Membe,

Kwanza Membe amekasirishwa sana kuona wanaccm wanamchafua huku mwenyekiti jk akiacha tu hizo rafu bila kupuliza kipyenga, amefika mbali na kusema sasa anajibu mapigo,

Wakati kundi la mwishoo ni la vijana, likiongozwa na Januari Makamba, Emanuel Nchimbi, Nape Nauye nk

Hawa wamestushwa sana na mwenyekiti kuwageuka nakuanza kuwa karibu na Lowasa wakati alishawaahidi kuwa sasa ni zamu ya vijana,

Hili nalo linajiapiza kuwa bora chama kife lakini sio kuongozwa na wazee kwakuwa wameongoza kwa miaka 50 lakini nchi inakuwa kwa kurudi nyuma,

Wakati kundi hili likisema kwa manung'uniko, linaonekana kama linasalitiana kwakuwa baadhi yao wameanza kupingana na kudharauliana wao kwa wao, na wengi wakimtupia lawama Januari na Nape kwa wamekuwa wakijipendekeza kwa Mwenyeti badala ya kujenga umoja wao!

Wadadisi wa siasa za ccm wanasema kuwa hali iliyopo haiwezi kutatulika bila juhudi za vyama marafiki vya nje, kama ANC afrika Kusini, PLO cha Palestina, Frelimo cha Msumbiji,nk

Haya ndugu zangu mungu aepushilie mbali Chama hiki kife bila kurusha miguu maana kitatuingiza kwenye matatizo makubwa!

Topic fed by: figments of your own imagination + inputs from the grape vine = Pure speculation without measurable outcomes!

Rating: 3 on a scale of 10
 
lowasa kiboko ukimuona kanisani azania front kama mlokole vile kumbe.......

ndani ya ccm hakunaga kama lowasa,,,,wamchezee waangukie pua,,,,cheza na lowasa wewe,,,wakimtosa tu,,wengine hata ubunge hawapati,,nijuacho,,sita na membe wanajiandaa kuwa viongozi wa kambi rasimi ya upinzani bungeni,,,,lowasa mkiti wa ccm,,,isiyo na dola,,,,
 
Mkuu,

Hoja nyepesi sana hiyo, haiwezi kusababisha mpasuko unaousema. CCM inajipanga sasa hivi, ndo maana wapinzani kwa nje mnakikuza hata kidogo kinachotokea chamani. poleni sana

Kenge huwa hasikii mpaka umtandike hadi damu zimtoke maskioni.
Endelea kujidanganya.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wadadisi wa siasa za ccm wanasema kuwa hali iliyopo haiwezi kutatulika bila juhudi za vyama marafiki vya nje, kama ANC afrika Kusini, PLO cha Palestina, Frelimo cha Msumbiji,nk

Haya ndugu zangu mungu aepushilie mbali Chama hiki kife bila kurusha miguu maana kitatuingiza kwenye matatizo makubwa!

Kote ulikoandika sina tatizo, isipokuwa hapa katika RED

1; ANC wao wenyewe ndani kwa ndani wana mvutano mkubwa na kuna kikundi kinaitwa ABZ (Anyone But Zuma) ambacho kiko against Zuma kupata mhula wa pili wa kuongoza na kinamtapa Cyril Ramaphosa ambaye ni tajiri milionea ama Kgalema Motlante ambaye ni makamu wa zuma ndio washike nchi. Mgogoro wao ni mkubwa sana huku Zuma naye akiwa anapigania mhula wake wa pili ambao uko mashakani. Hawawezi kushindwa kuokoa kwao waweze kuja kuiokoa CCM na mpasuko huku nao wakiwa na mpasuko mkubwa zaidi.

2; PLO ni chama cha wanaharakati zaidi ambao hawana uzoefu na siasa za kidemokrasia kama Tanzania. Itakuwa ni maajabu kwa wanaharakati hao kuonekana wanaweza kuja kusuluhisha mgogoro wa ndani ya CCM huku wakiwa na mitazamo miwili tofauti licha ya urafiki wao.

3; Frelimo huko kwao Msumbiji wamo katika matatizo makubwa sana na wakimlaumu Chisano (ambaye sisi TZ tunamheshimu) kuwa ameiacha nchi katika hali mbaya na chama kushindwa kuwasaidia wananchi. Hali yake Msumbiji sio shwari hata kidogo na wananchi wa huko wanaamini huenda hata RENAMO wakawa ni bora kuliko Frelimo (amini usiamini ndivyo hali ilivyo Msumbiji).

MY TAKE:
CCM ni kama iko ICU na inapumulia mashine. Two options; Au kuiacha mashine iwe ndio msaada wake maisha yote au kuizima mashine ili mgonjwa afe na kuanza kutafuta mbadala wake
 
320581_163430573738117_158108290937012_315590_985909421_n.jpg
 
I do not claim to know every member of the Nyerere family. But I assume wewe upo katika familia ya Nyerere? Huu mpasuko wa Lowassa ,Sita na Membe,na sijui nani mwingine;kwa vile CCM wanafanya mambo yao kisiri,kwa nini tusisubiri kuona uchaguzi wa CCM chairman baadaye mwaka huu?
Wewe huna lolote kuna kipindi ambacho ulikuja na thread ya kuwaponda wahindi halafu mwishoni wakakuhonga ukaanza kuwaomba mods wafute hiyo thread sikuamini kabisa halafu avatar yako unaonyesha wewe ni mzee wa makamo lakini huaminiki
 
mleta habari anataka tu kupotosha watu, anayoyasema hayana mtiririko tulio utegemea, mimi nilitegemea kusikia kundi la Lowassa limefanikiwa kumtia nyavuni swaiba wao ili amfagilie njia mzee wa monduli!

zaidi ya hayo nimewahi kuona thread nyingi zikidai Lowassa anamiliki nusu ya usalama wa taifa kwa hivyo basi hapa aliyepaswa kulalamika kuto tendewa haki ni rais na makundi mengine nikimaanisha kuwa usalama wa taifa umempangia rais shughuli ambayo ingeweza fanywa na diwani wa monduli!
 
Hizi hadithi ni wenye akili za kuku ndio wanazishabikia,mtu mwenye akili timamu anaziona ni shigongo material. CCM ni nchi jamani sio chama tena.
 
Hizi hadithi ni wenye akili za kuku ndio wanazishabikia,mtu mwenye akili timamu anaziona ni shigongo material. CCM ni nchi jamani sio chama tena.

Duuuuuh yani unapenda chama mpaka unasahau mstakabali wa taifa lako mkuu?

Nani kakwambia ccm ni nchi? Tema mate chini kijana tyuuuuuuuupu!

Haya chama kinakufa, je na nchi itakufa?
 
Wewe huna lolote kuna kipindi ambacho ulikuja na thread ya kuwaponda wahindi halafu mwishoni wakakuhonga ukaanza kuwaomba mods wafute hiyo thread sikuamini kabisa halafu avatar yako unaonyesha wewe ni mzee wa makamo lakini huaminiki

Hehee mkuu taratibu, ni kaka yangu huyo, ila tunatofautiana tu mitazamo ya kisiasa!
 
Back
Top Bottom