MPASUKO mkubwa CCM, Juhudi za Kimataifa zinahitajika kukinusuru!

Duuuuuh yani unapenda chama mpaka unasahau mstakabali wa taifa lako mkuu?

Nani kakwambia ccm ni nchi? Tema mate chini kijana tyuuuuuuuupu!

Haya chama kinakufa, je na nchi itakufa?
CCM haitakufa kama unavyoota wewe, bila ccm hakuna nchi. CCM ndio Tanzania,ndio system na ndio pumzi ya hii nchi. CCM ikisimama basi nchi inasimama,na wewe unasimama. Sijui umeelewa? Kama ungekua ni nyerere wa kweli basi ungeelewa hili.
 
changu kcheko! adui muombee njaa :alien:
 
........jamani Lowassa ni Jembe hata kama hamtaki, Sitta mnafiki hatuwezi kumpa nchi, Membe mzee wa joka la mdimu anayemtegemea Jack Zoka, pamoja na malezi ya ndani ya TISS hatufai......tunamhitaji mtu ambaye akiongea anasikika, akisema, anasomeka, huyu ni Lowassa, na kwa nature ya nchi hii iliyojaa sanaa, jibu ni Lowassa, samahni niliowakera ni maoni yangu haya.
 
Hakuna lo lote, huu ni mwono (uzushi?) wa muanzishaji wa hii thread. Binafsi sielewi nia yake.
 
CCM haitakufa kama unavyoota wewe, bila ccm hakuna nchi. CCM ndio Tanzania,ndio system na ndio pumzi ya hii nchi. CCM ikisimama basi nchi inasimama,na wewe unasimama. Sijui umeelewa? Kama ungekua ni nyerere wa kweli basi ungeelewa hili.
Daaaaah hivi kweli unaongea yanakutoka moyoni au kinywani haya unayoonge?

Nikupe pole kwakuwa hujui utendalo na usemalo,

Kubishana kwa hoja na mtu mwenye mawazo yako ni kufilisika na ni Uasi kwa Taifa langu linalohitaji Ukombozi toka kwa mkoloni mweusi ambae ni hatari kuliko mkoloni wa kale yule Mzungu wa pua ndefu!

Ila uponyaji ukaribu kwako,na naamini imani yako itakuponya!

Macho yako ya nyama yatakuwa shuhuda mkuu kuiona Tanzania Mpya!
 
Hali ndani ya ccm imezidi kuwa mbaya na ambayo haijawahi kutokea tangu kuundwa kwa chama hiki tangu mwaka 1977,

WAHAFIDHINA ndani ya ccm wameapa kuwa hawapo tayari kuona ccm ikishindwa Uchaguzi ujao, na wapo tayari kufia miguuni kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tz,

Taarifa za ndani na zakuaminika zinasema mpasuko wenye kutishia hata usalama wa nchi yetu,umeanzaa baada ya Lowassa kulazimishwa na wanausalama kuhudhuria UGAWAJI wa ng'ombe pale Monduli ulioratibiwa na kusimamiwa na Rais Jakaya Kikwete!

Kimsingi inasemekana Lowasa alishaapa kutokaa meza moja na JK, hivyo kitendo cha kulazimishwa kuwepo na kuamuliwa kutoa kauli ya kumsifu jk imemkera sana yeye na wanamtandao wake ndani ya ccm na wamepanga kufanya UASI mkubwa ndai ya CHAMA na ikibidi wanasema (nje ya chama)!

Wakati hilo likijiri kambi ya Samweli Sita nayo imechukizwa sana na hatua ya JK kukaribiana na Lowasa kwani wanasema kitendo cha JK kuwa (maadui) kilikuwa kikiwasaidia wao kujijenga kisiasa na kutimiza malengo yao ya Urais 2015

Hawa nao wanatafakari hatua za kuchukua na inatajwa kuna vikao vya siri vimekuwa vikifanyika Tabora na Masaki vikiratibiwa na wanamtandao wa Sitta!

Kundi lingine ni la Waziri Membe,

Kwanza Membe amekasirishwa sana kuona wanaccm wanamchafua huku mwenyekiti jk akiacha tu hizo rafu bila kupuliza kipyenga, amefika mbali na kusema sasa anajibu mapigo,

Wakati kundi la mwishoo ni la vijana, likiongozwa na Januari Makamba, Emanuel Nchimbi, Nape Nauye nk

Hawa wamestushwa sana na mwenyekiti kuwageuka nakuanza kuwa karibu na Lowasa wakati alishawaahidi kuwa sasa ni zamu ya vijana,

Hili nalo linajiapiza kuwa bora chama kife lakini sio kuongozwa na wazee kwakuwa wameongoza kwa miaka 50 lakini nchi inakuwa kwa kurudi nyuma,

Wakati kundi hili likisema kwa manung'uniko, linaonekana kama linasalitiana kwakuwa baadhi yao wameanza kupingana na kudharauliana wao kwa wao, na wengi wakimtupia lawama Januari na Nape kwa wamekuwa wakijipendekeza kwa Mwenyeti badala ya kujenga umoja wao!

Wadadisi wa siasa za ccm wanasema kuwa hali iliyopo haiwezi kutatulika bila juhudi za vyama marafiki vya nje, kama ANC afrika Kusini, PLO cha Palestina, Frelimo cha Msumbiji,nk

Haya ndugu zangu mungu aepushilie mbali Chama hiki kife bila kurusha miguu maana kitatuingiza kwenye matatizo makubwa!

Juhudi za kimataifa zinahitajika kuinusuru CCM? Mimi nilidhania CCM au chama chochote kile kinatakiwa kujinusuru chenyewe kupitia sanduku la kura. Sasa hao wa kukinusuru kutoka nje ya nchi watasaidiaje CCM? Sanduku la Kura? Silaha? Fedha?
Frelimo, ANC, PLO ilikuwa ni vyama vya ukombozi kama ilivyokuwa TANU; PLO bado ipo katika juhudi hizo; ANC na Frelimo bado ni wachanga sana katika harakati za kuondokana na udhalimu wa makaburu ambao ulikuwa umedhaminiwa na mataifa makubwa ya nje kama ureno, marekani n.k; CCM ni chama cha mapinduzi, ​watanzania wanayasubiri mapinduzi haya and time is running out.
 
Hali ndani ya ccm imezidi kuwa mbaya na ambayo haijawahi kutokea tangu kuundwa kwa chama hiki tangu mwaka 1977,

WAHAFIDHINA ndani ya ccm wameapa kuwa hawapo tayari kuona ccm ikishindwa Uchaguzi ujao, na wapo tayari kufia miguuni kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tz,

Taarifa za ndani na zakuaminika zinasema mpasuko wenye kutishia hata usalama wa nchi yetu,umeanzaa baada ya Lowassa kulazimishwa na wanausalama kuhudhuria UGAWAJI wa ng'ombe pale Monduli ulioratibiwa na kusimamiwa na Rais Jakaya Kikwete!

Kimsingi inasemekana Lowasa alishaapa kutokaa meza moja na JK, hivyo kitendo cha kulazimishwa kuwepo na kuamuliwa kutoa kauli ya kumsifu jk imemkera sana yeye na wanamtandao wake ndani ya ccm na wamepanga kufanya UASI mkubwa ndai ya CHAMA na ikibidi wanasema (nje ya chama)!

Wakati hilo likijiri kambi ya Samweli Sita nayo imechukizwa sana na hatua ya JK kukaribiana na Lowasa kwani wanasema kitendo cha JK kuwa (maadui) kilikuwa kikiwasaidia wao kujijenga kisiasa na kutimiza malengo yao ya Urais 2015

Hawa nao wanatafakari hatua za kuchukua na inatajwa kuna vikao vya siri vimekuwa vikifanyika Tabora na Masaki vikiratibiwa na wanamtandao wa Sitta!

Kundi lingine ni la Waziri Membe,

Kwanza Membe amekasirishwa sana kuona wanaccm wanamchafua huku mwenyekiti jk akiacha tu hizo rafu bila kupuliza kipyenga, amefika mbali na kusema sasa anajibu mapigo,

Wakati kundi la mwishoo ni la vijana, likiongozwa na Januari Makamba, Emanuel Nchimbi, Nape Nauye nk

Hawa wamestushwa sana na mwenyekiti kuwageuka nakuanza kuwa karibu na Lowasa wakati alishawaahidi kuwa sasa ni zamu ya vijana,

Hili nalo linajiapiza kuwa bora chama kife lakini sio kuongozwa na wazee kwakuwa wameongoza kwa miaka 50 lakini nchi inakuwa kwa kurudi nyuma,

Wakati kundi hili likisema kwa manung'uniko, linaonekana kama linasalitiana kwakuwa baadhi yao wameanza kupingana na kudharauliana wao kwa wao, na wengi wakimtupia lawama Januari na Nape kwa wamekuwa wakijipendekeza kwa Mwenyeti badala ya kujenga umoja wao!

Wadadisi wa siasa za ccm wanasema kuwa hali iliyopo haiwezi kutatulika bila juhudi za vyama marafiki vya nje, kama ANC afrika Kusini, PLO cha Palestina, Frelimo cha Msumbiji,nk

Haya ndugu zangu mungu aepushilie mbali Chama hiki kife bila kurusha miguu maana kitatuingiza kwenye matatizo makubwa!
Vipi ule mpasuko wa kundi la dk slaa na genge la mboe umefikia hatua gani sasa???
 
Watabanaaaa...mwishowe wataachia. Hawana mbinu nyingine zaidi ya ufisadi, mauaji, kufungia magazeti na mengine yote ya uovu!
 
........jamani Lowassa ni Jembe hata kama hamtaki, Sitta mnafiki hatuwezi kumpa nchi, Membe mzee wa joka la mdimu anayemtegemea Jack Zoka, pamoja na malezi ya ndani ya TISS hatufai......tunamhitaji mtu ambaye akiongea anasikika, akisema, anasomeka, huyu ni Lowassa, na kwa nature ya nchi hii iliyojaa sanaa, jibu ni Lowassa, samahni niliowakera ni maoni yangu haya.

uko huru kusema unachokiamini ndugu
 
Hii mada mbona imekaa kiumbeya umbeya?
 
Yetu macho tuone watakavyokorogana na hayo makundi yao. kwanini wasianzishe makundi ya kushughulikia migomo. kundi la lowasa madaktari, la sitta walimu, la membe kupunguza safari za jk nadhani yangetusaidia sana
 
Back
Top Bottom