Hapana hii ni ya uhakika kabisa kutoka kwa mshuri wa chadema bwana kitila mkumbo ndio alievunja ukimya huu,si habari ya kufikirika kama zile za kina membe,lowassa na sitta kwamba wanautaka urais.
Mshauri mkuu wa chadema ndugu, Kitila Mkumbo alitembelea Uingereza katika miji ya London na Readings kuanzia tarehe 5 Machi na 6 Machi 2012 na kuondoka tarehe 10 Machi, 2012.
Miongoni mwa mambo aliyotueleza ni kuwepo kwa mpasuko wa nani anasitahiri kubeba/kupeperusha bendera ya chadema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kati ya Freeman Mbowe na Dk. Slaa. Mkumbo anasema kuna kambi mbili zinazopingana ndani ya chadema kuhusu suala hilo.
Wanaomuunga mkono Dk. Slaa wanasema kwamba ni mtu anayejua kujenga hoja, ana mvuto, wananchi wanamwamini kuliko Mbowe lakini pia kwamba Dk. Slaa alishinda uchaguzi mkuu wa 2010 kabla ya kuchakachuliwa. Kwa sababu hiyo akipewa nafasi tena 2015 na chadema ikisimamia vyema uchaguzi huo Dk. Slaa anaweza kuwa Rais ajaye.
Kambi ya mbowe inasema kwamba alitumia asilimia 72 ya pesa yake katika kufanikisha kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010, wapo wanaodai chama kirudi mikononi mwa Mbowe kwa sababu hivi sasa ameimarika zaidi kwa ajili ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu ujao. My take: Kuendeleza huo mpasuko kutaisaidia ushindi wa CCM katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Wadau nimeleta kwenu tusaidiane namna ya kutafuta ufumbuzi wa mpasuko wa kambi mbili hizi ili chadema kiendelee kuwa chama kikuu cha upinzani na pengine kushika dola mwaka 2015. Source: Nilikuwa Uingereza miongoni mwa wafuasi wa chadema tuliohudhuria kikao cha kamanda wetu Kitila.
Tatizo wana CHADEMA walio wengi bado wanabeza kuwepo kwa mpasuko huo, afadhali wewe KIM KARDASH umekubali ukweli na kutoa mapendekezo yako. Kama ulivyosema, tumezoea kuona vyama vya upinzani vikiibuka na kuzama kila kunapokucha na mifano mizuri ni hiyo uliyoitoa. Tofauti hizo zinazoleta mpasuko zisipo rekebishwa mapema hii CDM nayo itabaki historia kama ilivyokuwa NCCR Mageuzi ya Mrema.
Mkuu wewe ndiye uliyekuwa London na Dr. Mkumbo wakati anasema hayo maneno?
Hakuna ubishi kwamba chadema ndio chama kikuu cha upinzani angalau kwa sasa nafasi ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na cuf ambao nao waliirithi kutoka kwa NCCR-MAGEUZI ile ya Mrema na Marando ambae kwa sasa yuko chadema huku Mrema yeye akiwa na chama "chake" siku hizi.
Lakini katika hali ya kusikitisha taarifa kutoka chanzo cha kuaminika(mshauri mkuu wa chadema)zinaeleza kwamba ndani ya chedema kuna mpasuka mkubwa kuhusu nani anapswa kuandaliwa kugombea urai kati ya mwenyekiti mbowe na katibu dr slaa.Ama hakika hii si habari njema sana kwa wapenda demokrasia na mabadiliko kiujumla.
Ushauri wangu ili kunusuru hali hii ya mpasuko isizidi kusambaa,Mbowe na slaa wake pembeni,hii itawavunja nguvu wapambe wao,watakuwa hawana tena kinachowatofautisha na pia itwapa muda mzuri mwenyekiti na katibu wake kushiriki mchakato huru wa kuitafutia chadema mgombea akaekidhi matarajio ya chama hicho ambayo siamini kama ni just kuwwa chama kikuu cha upinzani tu.
Mi naanza kuonyesha njia,majina haya sita kati yao anaweza kuipeperusha vyema bendera ya chadema kwenye urais.
1:Kitila Mkumbo(dr)
2:Zitto Kabwe
3:Halima Mdee
4:Abdallah Safari(prof)
5:Godbless Lema
6:Tundu Lisu
Nawasilisha.
Ndugu yangu hivi huyo namba 5 kweli ana sifa za kugombea urais kweli au umeamua kuwaliwaza wana Chadema.

kitila mkumbo-msahuri mkuu wa chadema,sio mwanahalisi.Recycled!
Mbona hamuweki source reliable?...?
Weka habari hiyo hapa kama alivyosema..Weka link!kitila mkumbo-msahuri mkuu wa chadema,sio mwanahalisi.
Hapana hii ni ya uhakika kabisa kutoka kwa mshuri wa chadema bwana kitila mkumbo ndio alievunja ukimya huu,si habari ya kufikirika kama zile za kina membe,lowassa na sitta kwamba wanautaka urais.
Kwenye nyekundu hapo, ni mzigo kwa chama hivi sasa. Wakazi wa Arusha wanajuuuta kumchagua. matukio ya uharibifu yamezidi jijini hapa, Watalii wengi hivi sasa hawaendi tena kuhofia usalama wao na sasa wengi wanakwenga mikoa ya morogoro, kigoma na kwingine. Watu wenye busara zao jijini Arusha tunaona kama tumevuliwa nguo kutokana na watu wote wa jiji hili kuonekana kama ni wahuni tu. Ni zaidi ya mwaka mmoja tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu, lakini muda wote huo Mbunge huyo amekuwa akilumbana tu na Meya wa JIJI bila sababu yoyote ya msingi. Hakuna ambalo vijana wamekwishalipata pamoja na kwamba ndiyo waliompa umaarufu huo.
mshauri mkuu wa chadema ndugu, kitila mkumbo alitembelea uingereza katika miji ya london na readings kuanzia tarehe 5 machi na 6 machi 2012 na kuondoka tarehe 10 machi, 2012.
miongoni mwa mambo aliyotueleza ni kuwepo kwa mpasuko wa nani anasitahiri kubeba/kupeperusha bendera ya chadema katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kati ya freeman mbowe na dk. Slaa. mkumbo anasema kuna kambi mbili zinazopingana ndani ya chadema kuhusu suala hilo.
wanaomuunga mkono dk. Slaa wanasema kwamba ni mtu anayejua kujenga hoja, ana mvuto, wananchi wanamwamini kuliko mbowe lakini pia kwamba dk. Slaa alishinda uchaguzi mkuu wa 2010 kabla ya kuchakachuliwa. Kwa sababu hiyo akipewa nafasi tena 2015 na chadema ikisimamia vyema uchaguzi huo dk. Slaa anaweza kuwa rais ajaye.
kambi ya mbowe inasema kwamba alitumia asilimia 72 ya pesa yake katika kufanikisha kampeni za uchaguzi wa mwaka 2010, wapo wanaodai chama kirudi mikononi mwa mbowe kwa sababu hivi sasa ameimarika zaidi kwa ajili ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao. my take: Kuendeleza huo mpasuko kutaisaidia ushindi wa ccm katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
wadau nimeleta kwenu tusaidiane namna ya kutafuta ufumbuzi wa mpasuko wa kambi mbili hizi ili chadema kiendelee kuwa chama kikuu cha upinzani na pengine kushika dola mwaka 2015. source: Nilikuwa uingereza miongoni mwa wafuasi wa chadema tuliohudhuria kikao cha kamanda wetu kitila.
Mkuu tofauti ndio uhai wa chama. Chama kimeishakomaa hivyo kila mtu ndani ya Chama anaamini akipewa kupeperusha bendera ya Chama basi chama kitambeba. Ikulu ni tamu mzee kila mtu anataka awepo pale.
kitila mkumbo-msahuri mkuu wa chadema,sio mwanahalisi.