Mpasuko CCM: Watofautiana juu ya Serikali mbili

Mpasuko CCM: Watofautiana juu ya Serikali mbili

Mimi ni mwana-CHADEMA, lakini napenda serikali moja (nina hoja zake, wala si gharama za kuendesha kama wengine wanavyodai), ikishindikana moja basi walau zibaki mbili halafu Katiba ya Zanzibar ikarekebishwe
Mkuu wangu; wewe ndio mtz mwenzangu haswa!
Yaani tumeshindwa kuwazuia kuvunja katiba, tutawaamuru wavunje mstaafu uliopatikana(katiba)?
Jamaa wako safarini, wanaelekea uhuru kamili; nyuma mwiko!
 
Suala hili la muundo wa Muungano ni la kihistoria Tume za Jaji Kisanga na Jaji Nyalali ambazo baada ya kuchukua maoni ya Watanzania zilipendekeza kuwepo kwa Serikali tatu, na pia tunakumbuka mijadala ya mwalimu Nyerere miaka ya 1993/1994 na kundi la G55 ambapo wabunge na viongozi wengi wa CCM walitaka aina hii ya Muungano (Federation) tunakumbuka kina Malecela, Kolimba, Jumbe, Njelu Kisaka n.k. Ulipelekea uoga wa kufikishwa bungeni kwa mjadala huo kwa hofu kuwa Bunge lingegawanyika.
Mimi naona kutofautiana ndani ya CCM ni suala la kihistoria, naamini bado wapo mashujaa watakao tete hoja hii bila uoga wowote kama walivyofanya kina Kisaka.
 
Kwenye muungano Tanganyika iko wapi jamani? mbona Zanzibar bado ipo jamani? inakuaje mbunge wa mkunazini anakuwa mjumbe wa kamati ya hesabu za serikali za mitaa ambalo si jambo la muungano?
 
Kasome ilani ya CDM using'ang'ane na kujiaminisha kwa upuuzi au uzembe wa kufuatilia usiyoyajua. Hoja ya chadema kutaka serikali 3 ipo kwenye ilani ya chama na ndiyo imetumika kujinadi ktk uchaguzi wa 2010. Sera hii pia imebebwa na CUF japo imebadilishwa na msimamo wa cuf zanzibar baada ya mchakato wa katiba.
Mkuu unajichanganya - Inaelekea hujui tofauti ya SERA na HOJA, Kumbe kwako wewe kwenye ilani vyama vinatangaza hoja na sio sera! Pole sana.

Ilani inaainisha maeneo ya vipaumbele vitakavyozingatiwa chama kikipata nafasi ya kuunda serikali. Kifupi hii inakuwa taarifa tu kwa wananchi na si mjadala, ila wanaweza kukubali au kukataa kwenye box la kura.

Hoja inajadiliwa. Bungeni hujadiliwa hoja hadi kufikia muafaka hata kwa kura. Bunge la katiba lina wabunge kwa sasa tayari kujadili hoja zilizomo kwenye rasimu ya pili ya katiba.

Kama CHADEMA walisema serikali tatu kwenye ilani yao 2010 hiyo haikuwa hoja, bali ilikuwa sera yao kama wakiingia madarakani. Kilichoko mezani sasa hv ni HOJA ya Tume ya kurekebisha Katiba kuwa Wananchi wanataka serikali 3 na ninasisitiza kuwa hiyo haijaletwa na CDM iliijadiliwe.

USIPOTOSHE kwa CCM wenye kuitakia mema nchi hii waanze kuona hii ni hoja na mambo ya CHADEMA. Haya ni mambo ya kitaifa zaidi sio kila kitu mnawaza CDM.
 
Dodoma. Baadhi ya wabunge wa CCM ambao ni wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wamepinga msimamo wa chama hicho unaowataka kutetea muundo wa Serikali mbili katika mijadala ya Bunge hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, wamesema hawaoni mantiki ya msimamo huo, kwa kuwa Katiba inayotengenezwa ni ya wananchi.

Habari kutoka katika kikao cha ndani cha CCM kilichofanyika juzi kati ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya na wabunge wa CCM, baadhi ya wabunge waliweka wazi msimamo wao wa kutaka Serikali tatu.

“Wapo wengi hawakubaliani na msimamo wa CCM wa kutaka watetee Serikali mbili na wanashikilia msimamo wa Serikali tatu, ambao ndiyo msimamo wa wananchi wao,” alisema mmoja wa wabunge aliyekaririwa kutoka katika kikao hicho.

Habari zilizovuja kutoka katika kikao hicho, miongoni mwa walioeleza msomamo huo ni Alphaxard Kangi Lugola wa Mwibara, ni miongoni mwa waliokuwa na msimamo mkali kuhusu jambo hilo.

Lugola alipohojiwa jana, alishikilia msimamo wake wa kutaka Serikali tatu akisema anafanya hivyo ili kulinda masilahi ya wananchi anaowawakilisha.

“Mimi kama Kangi Lugola kama mjumbe ninayesimamia walionituma, nataka Serikali tatu… Hapa kuna mambo mawili, msimamo wa chama na msimamo wa mimi kama mwakilishi,” alisema.

Lugola aliongeza, “Msimamo huu nitautoa pia kwenye Bunge la Katiba na nitajenga hoja halafu Bunge kama chombo kitaweka mizania, ni muundo upi wa Serikali upite.”

Inadaiwa Christopher Ole Sendeka wa Simanjiro alikwenda mbali zaidi na kumweleza Rais Kikwete kwamba hakuna dhambi kubwa aliyotenda kama kuruhusu Zanzibar kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa mujibu wa habari hizo, Sendeka alisema matatizo yote yanayoibuka sasa kuhusu muundo wa Serikali, yanatokana na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ambayo yalivunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 ndiyo yaliyosababisha Zanzibar kutambuliwa kama nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuruhusu Rais wa Zanzibar kuwa na uwezo wa kuigawa mipaka ya Zanzibar, jukumu ambalo ni la Rais wa Muungano.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo jana, Sendeka, alikataa kueleza lolote akisema kikao hicho kilikuwa ni cha faragha.

Mbunge mmoja kutoka Kanda ya Ziwa ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe, aliliambia gazeti hili kuwa kwa uchache, theluthi mbili ya wabunge wa CCM wanataka Serikali tatu.

“Subirini muone moto utakaowaka bungeni siku tutakapofika kwenye hicho kipengele cha Muungano, nadhani halitatosha, tumeamua kusimama na wananchi siyo msimamo wa CCM,” alidokeza.

Mjumbe huyo alisema yeye ataeleza wazi kuwa haungi mkono muundo wa Serikali ya CCM unaotaka Serikali mbili na kwamba yuko tayari kukabiliana na adhabu yoyote kama CCM itaona amefanya makosa.

Mbunge wa Beatrice Shelukindo wa Kilindi ambaye pia ni mjumbe wa Bunge hilo, alisema awali alikuwa muumini wa Serikali tatu lakini baada ya kuelimishwa, amebadili msimamo huo.

“Ni kweli wapo wana CCM wanataka Serikali tatu, hata mimi nilikuwa huko lakini baada ya kuelimishwa nakubali muundo wa Serikali mbili pale tu kero za Muungano zitakapotatuliwa,” alisema.

Alitoa mfano wa mbunge kutoka Zanzibar kuwekwa katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) wakati mambo yanayofanywa na kamati hiyo kwa asilimia 100 yanahusu upande wa Bara pekee.

Mbunge mwingine kutoka Kanda ya Ziwa ambaye naye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema ni usaliti kwa CCM kuwachagulia Watanzania aina ya Muungano baada ya kutoa maoni yao kuhusu jambo hilo.

“Mimi binafsi nataka Serikali mbili lakini siungi mkono kitendo cha chama changu kuweka msimamo wa pamoja na kutaka uwe ndiyo msimamo wa taifa kwani Katiba ni mali ya wananchi,” alisema na kuongeza:

Mgawanyiko huo wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, umekuja siku moja baada ya CCM kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kutangaza msimamo wa CCM kama taasisi kuwa ni muundo wa Serikali mbili na imewataka wajumbe wake kusimamia msimamo huo wakati wa mijadala bungeni.

Hata hivyo, Zainab Kawawa alitaka wajumbe wa Bunge la Katiba watakaokwenda kinyume na msimamo wa chama, wanyang’anywe kadi

source : mwananchi.co.tz
Huyo Lugola katumwa na akina nani anaowawakilisha labda katumwa na Mke wake na baba Mkwe wake kwani nilipita jimboni humo nikashangaa kwa Nini Lugola hawatafutii Maendeleo wananchi wake badala yake anakamia mambo yenye masilahi yake mwenyewe na si wananchi wake.
 
Dodoma. Baadhi ya wabunge wa CCM ambao ni wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wamepinga msimamo wa chama hicho unaowataka kutetea muundo wa Serikali mbili katika mijadala ya Bunge hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, wamesema hawaoni mantiki ya msimamo huo, kwa kuwa Katiba inayotengenezwa ni ya wananchi.

Habari kutoka katika kikao cha ndani cha CCM kilichofanyika juzi kati ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya na wabunge wa CCM, baadhi ya wabunge waliweka wazi msimamo wao wa kutaka Serikali tatu.

“Wapo wengi hawakubaliani na msimamo wa CCM wa kutaka watetee Serikali mbili na wanashikilia msimamo wa Serikali tatu, ambao ndiyo msimamo wa wananchi wao,” alisema mmoja wa wabunge aliyekaririwa kutoka katika kikao hicho.

Habari zilizovuja kutoka katika kikao hicho, miongoni mwa walioeleza msomamo huo ni Alphaxard Kangi Lugola wa Mwibara, ni miongoni mwa waliokuwa na msimamo mkali kuhusu jambo hilo.

Lugola alipohojiwa jana, alishikilia msimamo wake wa kutaka Serikali tatu akisema anafanya hivyo ili kulinda masilahi ya wananchi anaowawakilisha.

“Mimi kama Kangi Lugola kama mjumbe ninayesimamia walionituma, nataka Serikali tatu… Hapa kuna mambo mawili, msimamo wa chama na msimamo wa mimi kama mwakilishi,” alisema.

Lugola aliongeza, “Msimamo huu nitautoa pia kwenye Bunge la Katiba na nitajenga hoja halafu Bunge kama chombo kitaweka mizania, ni muundo upi wa Serikali upite.”

Inadaiwa Christopher Ole Sendeka wa Simanjiro alikwenda mbali zaidi na kumweleza Rais Kikwete kwamba hakuna dhambi kubwa aliyotenda kama kuruhusu Zanzibar kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa mujibu wa habari hizo, Sendeka alisema matatizo yote yanayoibuka sasa kuhusu muundo wa Serikali, yanatokana na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ambayo yalivunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 ndiyo yaliyosababisha Zanzibar kutambuliwa kama nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuruhusu Rais wa Zanzibar kuwa na uwezo wa kuigawa mipaka ya Zanzibar, jukumu ambalo ni la Rais wa Muungano.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo jana, Sendeka, alikataa kueleza lolote akisema kikao hicho kilikuwa ni cha faragha.

G55 wamefia wapi? Wakishindwa uitumia hii nafasi ambapo wingi wa wananchi wapo nyuma yao kwa kutaka serikali 3 basi na wanyamaze milele.
.
 
Wajumbe waelimishwe maana ya bunge la katiba
 
Wajumbe wa katiba wa wilya wengi walikuwa CCM, mbona hawakutetea maslahi ya CCM ?

CCM wengi hawakubaliani na serikali mbili.

Wabara ni wajinga nini, unapewa fursa ya kurejesha Tanganyika halafu unaleta mizengwe
 
tutaona nini kitafanyika kukwepa serikali tatu ambazo ni kweli wanaCCM pia wanazihitaji
 
Iwe iwavyo, wale waliodai katiba mpya wasipoipata katiba mpya bado wataendelea kudai katiba mpya tu. Ni ukweli usiopingika kuwa vyama vya siasa huzaliwa na hufa ila taifa limekuwepo hata majina yabadilishwe bado litakuwa katika mipaka ileile. Hoja yangu hapa ni kuwa kama katiba haitajadiliwa katika mijadala huru, na kupatika katiba ya wananchi basi tujue wazi kuwa madai ya katiba mpya hataishia hapo.
CCM wakitumia wingi wao kalazimisha katiba wanayoitaka basi wajue wazi watakapoondoka madarakani wataondoka na katiba waliyoiunda. Huo ndio ukweli tumeona hayo kule Misri kuwa katiba ya Morsi na chama chake cha Muslim brotherhood waliyoilazimishia Wamisri imeshatupwa jalalani. Na sasa wanakatiba mpya.
 
Hivi CCM ina wanachama wangapi mpaka wawachagulie wananchi katiba wanayoitaka wao? Tusitoke kwenye hoja ya msingi hapa, hii ni katiba ya Tanzania ambayo ina wenye vyama na wasio na vyama, believers and non believers, nasikitika kwanza politicians ndio wamejipachika jukumu na kieleele cha kujifanya ndio wanajua kila kitu!
 
Kinachosababisha watu kutaka mabadiliko ya sasa ni malalamiko ya kuhusu kero za Muungano, na kuona serikali 3 ndio suluhisho la kumaliza malalamiko, kama CCM wanaona watatua kero hizo ni sawa, lakini watanzania hawataki kusikia tena neno kero za muungano.
 
Huko sasa ndio kukosa nidhamu, walichaguliwa kupitia chama gani leo waweze kuwa tofauti na msimamo wa chama kilichowasimamisha kuwawakilisha hao wananchi, halafu hayo madai yao wamehitimisha vipi wakati nina uhakika hakuna hata mmbunge mmoja kati yao aliyewahi kufanya kikao jimboni mwake hili haweze hata kutetea huo msimamo wa wananchi.
 
Kwa kweli Watanzania hatutaki tena kero za Muungano. Tunataka ukinunua gari Zanzibar million5 hatutaki kulipishwa tena Kodi na TRA ya huku, kwa kuwa Zanzibar ni Tanzania pia. Hii ni kero.
 
Huko sasa ndio kukosa nidhamu, walichaguliwa kupitia chama gani leo waweze kuwa tofauti na msimamo wa chama kilichowasimamisha kuwawakilisha hao wananchi, halafu hayo madai yao wamehitimisha vipi wakati nina uhakika hakuna hata mmbunge mmoja kati yao aliyewahi kufanya kikao jimboni mwake hili haweze hata kutetea huo msimamo wa wananchi.

Political damage ni Kubwa hapo kwa wabunge wa CCM mfumo wa kuwa na directives /misimamo ya chama Ina madhara yake na 2015 sio mbali
 
Mimi ni mwana-CHADEMA, lakini napenda serikali moja (nina hoja zake, wala si gharama za kuendesha kama wengine wanavyodai), ikishindikana moja basi walau zibaki mbili halafu Katiba ya Zanzibar ikarekebishwe
Jabulani, unaota Utopia, katiba ya Zanzibar hairekebishwi kupunguza chochote. Tumeiwekea lock hakuna mtu yeyote atakaeweza kuibadilisha bila Kura ya Maoni. Upooo!

Serikali yako moja ni hiyo ya nyumbani kwako!
 
Last edited by a moderator:
Sisi wananchi tulishapendekeza maoni yetu vyama vilishapeleka maoni yao then rasim ikatoka na mapendekezo ya wananchi leo yabadilishwe kwa sababu tuu ccm hawayakubali ni kweli?

hayo mawazo ya selikari tatu ni mawazo ya mtu na mwananchi mwingine anayeona mufumo selikari mbili unafaa sasa kitu cha kushangaza nakujiuliza nikwanini huyu anaye taka mufumo wa selikari tatu aonekane yeye diyo wa maana au mtanzania kuliko mimi ninayeunga mkono mfumo selikari mbili?
 
Political damage ni Kubwa hapo kwa wabunge wa CCM mfumo wa kuwa na directives /misimamo ya chama Ina madhara yake na 2015 sio mbali
Tatizo sio chama hapo, tatizo ni hao wanachama on this instance. Hakuna chama kisichokuwa na misimamo duniani, na ukienda kwenye liberal democracies whereby votes are largely bought by firm part party lines between left and right. Hapo zikija sera ambazo zimekaa ki-conservative kuna baadhi ya wabunge hawato kubaliana nazo (either morally or due to self beliefs), same applies to other parties with strong view-points.

Hata vyama vyenye mlengo wa socialism vinabishana (how far to intervene) hivyo si wanachama wote wanakubaliana. Hizo ndio sababu vyama vya siasa vinaweka whips to make sure those at the top and representing people through their parties are always in toe with major party lines.

Mara chache sana utasikia wabunge wakitoa kauli tofauti na viongozi wao nadhani kwanza wanatakiwa kuandika barua na wapate baraka za juu kabla ya kutofautiana na sera za chama vilevile mfano kama UK kabla ya kupoteza kura ya chama bungeni lazima upate mmbunge wa upinzani mwenye msimamo na serikali hili usipige kura, vinginevyo ukipoteza kura ya chama kijinga sidhani kama watakuacha hivihivi wanawaita 'rebels' viongozi wa namna hiyo.

Ndio maana nakwambia hawa jamaa wamekosa nidhamu.
 
Back
Top Bottom