Mpasuko CCM: Watofautiana juu ya Serikali mbili

Mpasuko CCM: Watofautiana juu ya Serikali mbili

Ni Ni Mzanzibar(ambae ananufaika na serikali mbili) au Mtanzania bara MWENDAWAZIMU pekee anaweza kukubaliana na muundo wa serikali MBILI!

Anayekubaliana na serikali TATU ana HEKIMA!

Na anayekubaliana na serikali MOJA ni MZALENDO wa kweli!

Katiba mpya bila serikali ya watu wa Tanganyika,bunge la katiba ni sawa na kupoteza muda wake bure!
 
Naona CHADEMA mmejipanga kushinda hoja ya serikali tatu kwa namna yoyote ile, CCM wako smart sana, hawawezi kuja na msimamo ambao wengine hawakubaliani nao. Halafu serikali tatu hapingwi na wana-CCM pekee, juzi nimemsikia Cardinary PENGO akisema serikali tatu, hakuna muungano, na makundi mbalimbali pia hawaungani na hoja hii ya CHADEMA.
We ni mwehu.... Hoja ya serikali tatu sio hoja ya CHADEMA kama unavyotaka kuaminisha watu, hii ni hoja ya Tume ya mabadiliko ya Katiba,ambayo imewekwa kwenye rasimu ijadiliwe, baada ya Tume kuwahoji Wananchi na kuonekana wengi wanataka Serikali Tatu (61% ya waliohojiwa) Chadema kama Taasisi wametoa tu msimamo wao kwenye hoja hii kama wewe unavyotoa wa kwako serikali mbili, sasa sijui na wewe tuseme na tuite hii ni hoja yako unavyotaka serikali mbili?Tunajua lengo lako chafu kuwaaminisha wasio na vyama na CCM wenye nia safi kuwa haya ni mambo ya serikari 3 ni CHADEMA kumbe yapo kitaifa zaidi na si kichama. Muwe mnafikiria kabla ya kuposti, unaposti nini ujiulize!
 
Wabunge wa CCM wasipo kuwa macho na chama chao watajikuta chama kinawachagulia hadi wake wa kuwaoa na wanaume wa kulewa nao.
 
CCM wakijibu haya maswali (1. kwanini kwetu ni kwao na kwao kwao, 2. Kwanini serikali yetu ni yao na serikali yao ni yao?), basi nami nitakuwa muumini wa serikali mbili.
 
Naona CHADEMA mmejipanga kushinda hoja ya serikali tatu kwa namna yoyote ile, CCM wako smart sana, hawawezi kuja na msimamo ambao wengine hawakubaliani nao. Halafu serikali tatu hapingwi na wana-CCM pekee, juzi nimemsikia Cardinary PENGO akisema serikali tatu, hakuna muungano, na makundi mbalimbali pia hawaungani na hoja hii ya CHADEMA.

pengo hana nguvu kuliko wananchi
 
Kama asilimia zote 61 za wananchi waliotaka serekali 3 ni CHADEMA basi jiandaeni kuikabidhi nchi CHADEMA.
 
Nimekuwa nikisikia CHADEMA wakisemwa kwa uminyaji wa demoklasia kwa kutokubali mawazo ya baadhi ya wanachama wao wanaokwenda kinyume na misimamo ya chama. Je CCM nao hawaoni kama kumlazimisha mtu kuwa muumini wa serikali mbili kinyume na mtazamo wake ni kuminya democrasia? Au inakuwa hivyo tu endapo wahusika ni CHADEMA?
 
Naona CHADEMA mmejipanga kushinda hoja ya serikali tatu kwa namna yoyote ile, CCM wako smart sana, hawawezi kuja na msimamo ambao wengine hawakubaliani nao. Halafu serikali tatu hapingwi na wana-CCM pekee, juzi nimemsikia Cardinary PENGO akisema serikali tatu, hakuna muungano, na makundi mbalimbali pia hawaungani na hoja hii ya CHADEMA.

Nikurekebishe,hoja ya serikali tatu sio ya CHADEMA,bali ni matokeo ya maoni ya wananchi yaliyokusanywa na tume ya jaji Warioba ambapo 64% wamependekeza muundo wa serikali tatu. CHADEMA wana support msimamo huu wa tume sababu ni matakwa ya wananchi wengi.
 
Demokrasia ya Tanzania inakizungumkuti sana hivi iweje mbunge atoe maoni hafu aseme jina lake lisiandikwe kwani anaogopa nini ikiwa maoni hayo ametumwa na wananchi wake? Wanasiasa haswa wa CCM huwa ni waoga kutoa maoni hadharani yanayotofautiana na chama chao hata kama watakuwa wametumwa na wananchi wao.

Dodoma. Baadhi ya wabunge wa CCM ambao ni wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wamepinga msimamo wa chama hicho unaowataka kutetea muundo wa Serikali mbili katika mijadala ya Bunge hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, wamesema hawaoni mantiki ya msimamo huo, kwa kuwa Katiba inayotengenezwa ni ya wananchi.

Habari kutoka katika kikao cha ndani cha CCM kilichofanyika juzi kati ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya na wabunge wa CCM, baadhi ya wabunge waliweka wazi msimamo wao wa kutaka Serikali tatu.

“Wapo wengi hawakubaliani na msimamo wa CCM wa kutaka watetee Serikali mbili na wanashikilia msimamo wa Serikali tatu, ambao ndiyo msimamo wa wananchi wao,” alisema mmoja wa wabunge aliyekaririwa kutoka katika kikao hicho.

Habari zilizovuja kutoka katika kikao hicho, miongoni mwa walioeleza msomamo huo ni Alphaxard Kangi Lugola wa Mwibara, ni miongoni mwa waliokuwa na msimamo mkali kuhusu jambo hilo.

Lugola alipohojiwa jana, alishikilia msimamo wake wa kutaka Serikali tatu akisema anafanya hivyo ili kulinda masilahi ya wananchi anaowawakilisha.

“Mimi kama Kangi Lugola kama mjumbe ninayesimamia walionituma, nataka Serikali tatu… Hapa kuna mambo mawili, msimamo wa chama na msimamo wa mimi kama mwakilishi,” alisema.

Lugola aliongeza, “Msimamo huu nitautoa pia kwenye Bunge la Katiba na nitajenga hoja halafu Bunge kama chombo kitaweka mizania, ni muundo upi wa Serikali upite.”

Inadaiwa Christopher Ole Sendeka wa Simanjiro alikwenda mbali zaidi na kumweleza Rais Kikwete kwamba hakuna dhambi kubwa aliyotenda kama kuruhusu Zanzibar kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa mujibu wa habari hizo, Sendeka alisema matatizo yote yanayoibuka sasa kuhusu muundo wa Serikali, yanatokana na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ambayo yalivunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 ndiyo yaliyosababisha Zanzibar kutambuliwa kama nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuruhusu Rais wa Zanzibar kuwa na uwezo wa kuigawa mipaka ya Zanzibar, jukumu ambalo ni la Rais wa Muungano.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo jana, Sendeka, alikataa kueleza lolote akisema kikao hicho kilikuwa ni cha faragha.

Mbunge mmoja kutoka Kanda ya Ziwa ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe, aliliambia gazeti hili kuwa kwa uchache, theluthi mbili ya wabunge wa CCM wanataka Serikali tatu.

“Subirini muone moto utakaowaka bungeni siku tutakapofika kwenye hicho kipengele cha Muungano, nadhani halitatosha, tumeamua kusimama na wananchi siyo msimamo wa CCM,” alidokeza.

Mjumbe huyo alisema yeye ataeleza wazi kuwa haungi mkono muundo wa Serikali ya CCM unaotaka Serikali mbili na kwamba yuko tayari kukabiliana na adhabu yoyote kama CCM itaona amefanya makosa.

Mbunge wa Beatrice Shelukindo wa Kilindi ambaye pia ni mjumbe wa Bunge hilo, alisema awali alikuwa muumini wa Serikali tatu lakini baada ya kuelimishwa, amebadili msimamo huo.

“Ni kweli wapo wana CCM wanataka Serikali tatu, hata mimi nilikuwa huko lakini baada ya kuelimishwa nakubali muundo wa Serikali mbili pale tu kero za Muungano zitakapotatuliwa,” alisema.

Alitoa mfano wa mbunge kutoka Zanzibar kuwekwa katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) wakati mambo yanayofanywa na kamati hiyo kwa asilimia 100 yanahusu upande wa Bara pekee.

Mbunge mwingine kutoka Kanda ya Ziwa ambaye naye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema ni usaliti kwa CCM kuwachagulia Watanzania aina ya Muungano baada ya kutoa maoni yao kuhusu jambo hilo.

“Mimi binafsi nataka Serikali mbili lakini siungi mkono kitendo cha chama changu kuweka msimamo wa pamoja na kutaka uwe ndiyo msimamo wa taifa kwani Katiba ni mali ya wananchi,” alisema na kuongeza:

Mgawanyiko huo wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, umekuja siku moja baada ya CCM kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kutangaza msimamo wa CCM kama taasisi kuwa ni muundo wa Serikali mbili na imewataka wajumbe wake kusimamia msimamo huo wakati wa mijadala bungeni.

Hata hivyo, Zainab Kawawa alitaka wajumbe wa Bunge la Katiba watakaokwenda kinyume na msimamo wa chama, wanyang’anywe kadi

source : mwananchi.co.tz
 
Ntakuwa Muasi wa kwanza wa Taifa hili Kama CCM watachakachua maoni ya wananchi wanaotaka serikali tatu na kuweka maon yao ya kipumbavu eti serikali mbili. TANGANYIKA KWANZA..
 
We ni mwehu.... Hoja ya serikali tatu sio hoja ya CHADEMA kama unavyotaka kuaminisha watu, hii ni hoja ya Tume ya mabadiliko ya Katiba,ambayo imewekwa kwenye rasimu ijadiliwe, baada ya Tume kuwahoji Wananchi na kuonekana wengi wanataka Serikali Tatu (61% ya waliohojiwa) Chadema kama Taasisi wametoa tu msimamo wao kwenye hoja hii kama wewe unavyotoa wa kwako serikali mbili, sasa sijui na wewe tuseme na tuite hii ni hoja yako unavyotaka serikali mbili?Tunajua lengo lako chafu kuwaaminisha wasio na vyama na CCM wenye nia safi kuwa haya ni mambo ya serikari 3 ni CHADEMA kumbe yapo kitaifa zaidi na si kichama. Muwe mnafikiria kabla ya kuposti, unaposti nini ujiulize!

Kasome ilani ya CDM using'ang'ane na kujiaminisha kwa upuuzi au uzembe wa kufuatilia usiyoyajua. Hoja ya chadema kutaka serikali 3 ipo kwenye ilani ya chama na ndiyo imetumika kujinadi ktk uchaguzi wa 2010. Sera hii pia imebebwa na CUF japo imebadilishwa na msimamo wa cuf zanzibar baada ya mchakato wa katiba.
 
Mimi ni mwana-CHADEMA, lakini napenda serikali moja (nina hoja zake, wala si gharama za kuendesha kama wengine wanavyodai), ikishindikana moja basi walau zibaki mbili halafu Katiba ya Zanzibar ikarekebishwe

Je wazanzibari wako tayari kubadili katiba yao?Naamini hawa waliosema serikali tatu wana akili sana.Kwanza walitaka kuficha aibu ya Rais aliyeruhusu kuvunjwa kwa katiba ya JMT.Pili waliona jinsi wazanzibari walivyokuwa na msimamo mkali dhidi ya muungano huu na kama utakumbuka ile rasimu ya sheria ya kwanza ya mabadiliko ya katiba ilikataza kujadiliwa kwa suala la muungano lakini waliichana chana hadharani licha ya kwamba tayari wazanzibari walikwisha jipa mamlaka ya nchi kamili kinyume na katiba ya JMT.Tatu hofu ya kuvunjika muunngano wa serikali 3 ni ya kufikirika na hivyo haina mashiko kwani hata sasa kwenye serikali mbili tayari wazanzibari wamesha vunja na sasa wao wanajitambulisha kama wazenji na sio waTZ

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Ni vema tukawa tunajadili hili jambo bila kuingiza ITIKADI. Hili swala la serikali 3 siyo la CHADEMA, bali zaidi ya 61% ya waliotoa maoni. Inamaana hayo maoni yalitolewa kwa kufata ITIKADI? Na je, hawa wabunge wengine wa CCM wanaounga mkono serikali 3 kinyume na azimio la chama chao ni CHADEMA hao? Ni vema tukatumia hoja kujadili hili bila kujali ni msimamo wa chama gani. KATIBA tunayoipigania siyo ya chama chochote, bali ni ya wananchi wote wa TANZANIA.

63% wanaunga hoja ya serikali 3, CCM wanasema ni hoja ya CHADEMA kwa hiyo pamoja na CCM kuchezea mabaraza ya katiba bado wanaonekana hoja yao ni dhaifu mno hivyo CCM hawana ushawishi wa demokrasia bali wamebaki madarakani kwa nguvu ya dola, hawaoni kuwa CHADEMA huwa wanashinda kila chaguzi ila wanachakachuliwa? jana tu madudu yamejidhihirisha katika uchaguzi wa m/kiti wa muda zaidi ya kura 20 zimeonekana kuzidi ili mtu wao apite kwa urahisi. Ama kweli CCM IKO ICU.
 
Naona CHADEMA mmejipanga kushinda hoja ya serikali tatu kwa namna yoyote ile, CCM wako smart sana, hawawezi kuja na msimamo ambao wengine hawakubaliani nao. Halafu serikali tatu hapingwi na wana-CCM pekee, juzi nimemsikia Cardinary PENGO akisema serikali tatu, hakuna muungano, na makundi mbalimbali pia hawaungani na hoja hii ya CHADEMA.

Endelea kuonesha jinsi CDM inavyowanyika usingizi...Hivi hii ni hoja yao eehh....Nadhani jina lako limechangia uwezo wako wa kufikiri kuwa chini kiasi hiki...halafu unajidanganya kuwa eti wabunge wote wa CCm wanaweza kuungana na kukubaliana kwenye hili? Unatumia kitu gani kufikiri Cybercrime? Hata wazanzibari watakubaliana na wewe katika hili? Too low, naona hoja ya CCM ikipigwa chini kwa anguko la aina yake.
 
Last edited by a moderator:
Lugola alipohojiwa jana, alishikilia msimamo wake wa kutaka Serikali tatu akisema anafanya hivyo ili kulinda masilahi ya wananchi anaowawakilisha.

“Mimi kama Kangi Lugola kama mjumbe ninayesimamia walionituma, nataka Serikali tatu… Hapa kuna mambo mawili, msimamo wa chama na msimamo wa mimi kama mwakilishi,” alisema.
Inaingia akilini.
 
Angalau kwa hili la katiba CCM iwaache wabunge wake wawakilishe maoni ya wapiga kura wao....
 
We unayesema CCM inawasomi wengi ina mana usomi wao ndo wana hati miliki yakutuchagulia sisi wananchi serikali wanayoitaka wao kwani CCM ndo wameiumba Tanzania au wamewazaa watanzania? KUsoma sio hoja unaweza kusoma ukawa na digrii nyingi lakini ukatoka bila kuelimika. Aidha umeenda kukua au kusoma English course. Kama hao wasomi wanahoja walete huo mkataba wa muungano unasemaje yani Aticle of union hakuna hata kipengele kimoja kinachosema serikali mbili. kwenye Katiba yao ya chama ndo kuna muungano wa vyama viwili. ASP na TANU ambayo ndo CCM.
 
Back
Top Bottom