Mpasuko CCM: Watofautiana juu ya Serikali mbili

Mpasuko CCM: Watofautiana juu ya Serikali mbili

Serikali ni2 tu hatuna haja ya serikali nyingi kama 2 zinatushinda tuongeze matatizo mengine tena!!chamsingi ni kuweka mikakati madhubuti ili kutatua matatizo ya muungano,wapinzani wanataka serikali 3 kwa lengo la kupata upenyo wa madaraka,lakini hicho kitu hakipo na hakitawezekana naomba viongozi wa ccm kuwa mbunge yeyote wa ccm anaye saliti msimano huu wa chama akuchukuliwe hatua kali za kinidhamu,by katibu hamasa na chipukizi Rungwe
 
Serikali ni2 tu hatuna haja ya serikali nyingi kama 2 zinatushinda tuongeze matatizo mengine tena!!chamsingi ni kuweka mikakati madhubuti ili kutatua matatizo ya muungano,wapinzani wanataka serikali 3 kwa lengo la kupata upenyo wa madaraka,lakini hicho kitu hakipo na hakitawezekana naomba viongozi wa ccm kuwa mbunge yeyote wa ccm anaye saliti msimano huu wa chama akuchukuliwe hatua kali za kinidhamu,by katibu hamasa na chipukizi Rungwe

Serikali tatu ni kuimyonga znz
Na tanganyika haifaidiki lolote.
Bora kifanyike kitu kitaalam
Muungano uli kuja kwa nguvu ya nje so ni wakati wa kuuchambua kisayansi
 
Mimi binafsi nilipenda tuwe na serikali moja lakini Zanzibar tayari wamerekebisha Katiba yao na kujitangazia kuwa Nchi yenye serikali yake, rais wake na mamlaka yake, sasa inakuwaje Tanganyika isiwepo pia?

Ni kweli kabisa!! Nampongeza Mheshimiwa Kange Lugola kwa kuliona hili... Haiwezekani wewe Mbunge udharau maoni ya wananchi unaowaongo!. Ole-Sendeka kasema kweli,, kama CCM wanataka Serikali mbili kwanini walikubali Zanzibar kufanya mabadiliko makubwa ya kujitangazia utawala wao na kuvunja Katiba ya Muungano..

Nitawaweka kwenye maombi yangu Wabunge wote watakaotetea maslahi ya wananchi kwenye mchakato huu
 
Naona vurugu kwa sababu ya maslahi ya ccm! wananchi tunataka kama tulivyopendekeza sasa kama chama ni zaidi yetu tutaona! lakini nawatahadharisha viongozi wa juu angalieni sana gharama za katiba hii maana msije mkajikuta tunakataa katika kura za maoni na pesa zetu kama walipa kodi zikapotea bure
 
Naona CHADEMA mmejipanga kushinda hoja ya serikali tatu kwa namna yoyote ile, CCM wako smart sana, hawawezi kuja na msimamo ambao wengine hawakubaliani nao. Halafu serikali tatu hapingwi na wana-CCM pekee, juzi nimemsikia Cardinary PENGO akisema serikali tatu, hakuna muungano, na makundi mbalimbali pia hawaungani na hoja hii ya CHADEMA.

mbona mnaihusihsa cdm na serikali 3 mbona cuf hamisemi? cdm cdm cdm kumbe inawakosesha usingizi eheeeeee!
 
ccm wasipende kuwabuluza wananchi vile wanavyotaka wao,kwanza mungano una mapungufu mengi sana yawezekana wao wananufaika sana na huo mungano wa serikali mbili,mfano kuonyesha huu muungano ni kisanii ni hakuna hata raisi mmoja aliyewahi kufanya ziara ya kukagua maendeleo zanzibar,kama kuna mtu ana kumbukumbu naomba atujuze.
 
Kama kutakua na JMT muungano lazima uwe na serikali tatu. Kama zanz wamejitoa basi hapo sawa.
 
mleta mada mwenyewe kaiweka na kusema mkuu, ni wazi ni uzushi tu na wala hakuna mbunge wa CCM anaweza kuwa kinyume na hoja ya serikali mbili, serikali mbili ndiyo muhimili wa Muungano kama kweli tunahitaji kuendelea kujiita watanzania.


Tafadhali Nijibu suali langu : washirika wa muungano ni Zanzibar na Tanganyika au na Tanzania ? Serikali ya mshiriki mmoja ya ZANZIBAR ipo ya mshiriki wa pili iwapi ???
 
mleta mada mwenyewe kaiweka na kusema mkuu, ni wazi ni uzushi tu na wala hakuna mbunge wa CCM anaweza kuwa kinyume na hoja ya serikali mbili, serikali mbili ndiyo muhimili wa Muungano kama kweli tunahitaji kuendelea kujiita watanzania.

Siyo kweli mkuu. Tumia fikra ulizopewa na Mungu japo kidogo, acha ushabiki! Katiba ya mwaka 10 ya Zanzibar ni halali au si halali? Ukinijibu, nitarudi ili tuelimishane, mimi niridhike na wewe uridhike!
 
siyo swala la mbunge mkuu, CCM wana wasomi wazuri sana, wanajua athari za serikali tatu kama ambavyo makundi mengine wakiwemo wanazuoni wanaungana na CCM kuilaani hoja ya serikali tatu kwa vile haina mashiko katika mstakabali wa umoja, undugu ulioasisiwa na viongozi watangulizi wa taifa hili teule la Mungu. Inawezekana kabisa Mwandishi wa habari aliwahoji wana-CCM wafu kama akina MBOWE na weingine waliokumbatia kadi za CCM huku wakiwa upinzani.

SIO SWALA LA CCM KUWA NA WASOMI WENGI ,SUALA NI KUJA NA HOJA ,WARIOBA KAJA NA HOJA NZITO KUHUSU SERIKALI TATU ,CCM WASILETE UBISHI TU NA KUTUMIA WINGI WAO BUNGENI ,WAJE NA HOJA ,NA WATAMBUE USOMI WAO HAUWEZI KUWA JUU YA MAWAZO NA MTAZAMO WA WANANCHI WALIO WENGI ,HALAFU HAMPATI USINGIZI KILA SIKU KABLA HAMJABEZA WAPINZANI ,NA WEWE NGOJA NIKUPE MAKAVU YAKO INAWEZEKANA KABISA HUNA TAARIFA KUWA ULE MRADI WA B7 PALE LUMUMBA HAUPO TENA ,HIVYO WE KAZANA KUPOST UTUMBO UKITEGEMEA B7 IMEKULA KWAKO MJOMBA.:smile-big::loco:
 
Mbunge yeyote asiyetaka serikali 3 asithubutu hata kujisumbua kuchukua fomu 2015 , KUKATAA SERIKALI 3 NI KUJIFUTA UBUNGE !
 
Serikali ni2 tu hatuna haja ya serikali nyingi kama 2 zinatushinda tuongeze matatizo mengine tena!!chamsingi ni kuweka mikakati madhubuti ili kutatua matatizo ya muungano,wapinzani wanataka serikali 3 kwa lengo la kupata upenyo wa madaraka,lakini hicho kitu hakipo na hakitawezekana naomba viongozi wa ccm kuwa mbunge yeyote wa ccm anaye saliti msimano huu wa chama akuchukuliwe hatua kali za kinidhamu,by katibu hamasa na chipukizi Rungwe

kama UNATAKA KUMPONZA MBUNGE WAKO , MWAMBIE APINGE SERIKALI 3 , HAKIKA HUO NDIYO UTAKUWA MWISHO WAKE KUWA MBUNGE .
 
Mie nimefadhaishwa mno na 'eti' wasomi waliokutana hivi juzi na kusema serikali moja. Hivi tume ya katiba si ilipokea maoni yao? Kama sio kutumwa basi ni tatizo kubwa nchin. Kioja kingine ni kuwa kama wasomi hawaelekezi nguvu zao katika elimu kana kwamba hii iliyopo ndio bora kwao!!!!!!!!!
 
na bado wataendelea kuchafuana na kukandamizana na kulaana wenyewe kwa wenyewe
sisi cdm yetu amacho tu tukiwaangalia ili baadaye tuje kushika nafasi za juu
Dodoma. Baadhi ya wabunge wa CCM ambao ni wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, wamepinga msimamo wa chama hicho unaowataka kutetea muundo wa Serikali mbili katika mijadala ya Bunge hilo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, wamesema hawaoni mantiki ya msimamo huo, kwa kuwa Katiba inayotengenezwa ni ya wananchi.

Habari kutoka katika kikao cha ndani cha CCM kilichofanyika juzi kati ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya na wabunge wa CCM, baadhi ya wabunge waliweka wazi msimamo wao wa kutaka Serikali tatu.

“Wapo wengi hawakubaliani na msimamo wa CCM wa kutaka watetee Serikali mbili na wanashikilia msimamo wa Serikali tatu, ambao ndiyo msimamo wa wananchi wao,” alisema mmoja wa wabunge aliyekaririwa kutoka katika kikao hicho.

Habari zilizovuja kutoka katika kikao hicho, miongoni mwa walioeleza msomamo huo ni Alphaxard Kangi Lugola wa Mwibara, ni miongoni mwa waliokuwa na msimamo mkali kuhusu jambo hilo.

Lugola alipohojiwa jana, alishikilia msimamo wake wa kutaka Serikali tatu akisema anafanya hivyo ili kulinda masilahi ya wananchi anaowawakilisha.

“Mimi kama Kangi Lugola kama mjumbe ninayesimamia walionituma, nataka Serikali tatu… Hapa kuna mambo mawili, msimamo wa chama na msimamo wa mimi kama mwakilishi,” alisema.

Lugola aliongeza, “Msimamo huu nitautoa pia kwenye Bunge la Katiba na nitajenga hoja halafu Bunge kama chombo kitaweka mizania, ni muundo upi wa Serikali upite.”

Inadaiwa Christopher Ole Sendeka wa Simanjiro alikwenda mbali zaidi na kumweleza Rais Kikwete kwamba hakuna dhambi kubwa aliyotenda kama kuruhusu Zanzibar kuvunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa mujibu wa habari hizo, Sendeka alisema matatizo yote yanayoibuka sasa kuhusu muundo wa Serikali, yanatokana na marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ambayo yalivunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 2010 ndiyo yaliyosababisha Zanzibar kutambuliwa kama nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuruhusu Rais wa Zanzibar kuwa na uwezo wa kuigawa mipaka ya Zanzibar, jukumu ambalo ni la Rais wa Muungano.

Alipoulizwa kuhusu madai hayo jana, Sendeka, alikataa kueleza lolote akisema kikao hicho kilikuwa ni cha faragha.

Mbunge mmoja kutoka Kanda ya Ziwa ambaye hata hivyo hakutaka jina lake litajwe, aliliambia gazeti hili kuwa kwa uchache, theluthi mbili ya wabunge wa CCM wanataka Serikali tatu.

“Subirini muone moto utakaowaka bungeni siku tutakapofika kwenye hicho kipengele cha Muungano, nadhani halitatosha, tumeamua kusimama na wananchi siyo msimamo wa CCM,” alidokeza.

Mjumbe huyo alisema yeye ataeleza wazi kuwa haungi mkono muundo wa Serikali ya CCM unaotaka Serikali mbili na kwamba yuko tayari kukabiliana na adhabu yoyote kama CCM itaona amefanya makosa.

Mbunge wa Beatrice Shelukindo wa Kilindi ambaye pia ni mjumbe wa Bunge hilo, alisema awali alikuwa muumini wa Serikali tatu lakini baada ya kuelimishwa, amebadili msimamo huo.

“Ni kweli wapo wana CCM wanataka Serikali tatu, hata mimi nilikuwa huko lakini baada ya kuelimishwa nakubali muundo wa Serikali mbili pale tu kero za Muungano zitakapotatuliwa,” alisema.

Alitoa mfano wa mbunge kutoka Zanzibar kuwekwa katika Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Serikali za Mitaa (LAAC) wakati mambo yanayofanywa na kamati hiyo kwa asilimia 100 yanahusu upande wa Bara pekee.

Mbunge mwingine kutoka Kanda ya Ziwa ambaye naye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema ni usaliti kwa CCM kuwachagulia Watanzania aina ya Muungano baada ya kutoa maoni yao kuhusu jambo hilo.

“Mimi binafsi nataka Serikali mbili lakini siungi mkono kitendo cha chama changu kuweka msimamo wa pamoja na kutaka uwe ndiyo msimamo wa taifa kwani Katiba ni mali ya wananchi,” alisema na kuongeza:

Mgawanyiko huo wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, umekuja siku moja baada ya CCM kupitia kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye kutangaza msimamo wa CCM kama taasisi kuwa ni muundo wa Serikali mbili na imewataka wajumbe wake kusimamia msimamo huo wakati wa mijadala bungeni.

Hata hivyo, Zainab Kawawa alitaka wajumbe wa Bunge la Katiba watakaokwenda kinyume na msimamo wa chama, wanyang’anywe kadi


source : mwananchi.co.tz
 
mleta mada mwenyewe kaiweka na kusema mkuu, ni wazi ni uzushi tu na wala hakuna mbunge wa CCM anaweza kuwa kinyume na hoja ya serikali mbili, serikali mbili ndiyo muhimili wa Muungano kama kweli tunahitaji kuendelea kujiita watanzania.

Wewe acha kuwa kama cockroach. ulivyo kilaza et hujui kama Zanzibar ni nchi huru, ambayo kwa uhuru huo, unaitaka Tanganyika iliyo huru pia ili tupate mlinganyo sawia. Sasa ili Tanzania iwe Tanzania, lazima nchi ya Tanganyika iwe na kila kitu chake na tukutane kwenye Muungano na Zanzibar kila mmoja akiwa na uhuru kamili. Kwa hiyo sasa, serikali ya Tanganyika + Serikali ya Zanzibar = Serikali ya Muungano wa Tanzania = serikali tatu na siyo vinginevyo. Muhimu watu kama wewe msiwe mnajichoresha kwa kuonesha ujinga wenu kwenu hili jamvi. Kama hujui unajitahidi kuuliza na si kubwabwaja mineno kama muuza K.

VIVA TANGANYIKA
 
Back
Top Bottom