Polisi wazuia msafara wa mgombea ubunge wa CHADEMA

Polisi wazuia msafara wa mgombea ubunge wa CHADEMA

babalao 2

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
5,426
Reaction score
3,309
1392636363852.jpg

Polisi mkoani Iringa wakiwa wameuzuia msafara wa mgombea ubunge jimbo la Kalenga, Bi Grace Tendega kupitia CHADEMA kwa madai hawakuwa na kibali cha kufanya maandamano hayo ya magari hapa ni eneo la lango la mji Samora ambapo msafara huo ulikuwa ukitokea maeneo ya Ndiuka kuelekea kwa msimamizi wa uchaguzi ili kuchukua fomu.
 
Kwa mwendo huu wa vikwazo tutafika kweli?
 
Polisi wa Iringa wana Laaana ya Mwangosi, baada ya Kamuhanda kupandishwa cheo kila RPC anataka kusimamia mauaji ili apandishwe cheo
 
hatuwashangai mwenyekiti wa CCM katangaza vita wenye haki nchi hii ni wana CCM Geofrey Mgimwa atakapo kwenda kuchukua fomu mwenyekiti katibu mkuu makamu mwenyekiti katibu mwenezi mbunge wa isimani wote watamsindikiza na hakutakuwa na katazo lolote mwenyekiti unayaona uliyotanga tbccm
 
Wanajiamlia tu nunua waendesha boda boda kwa buku ten ten afu wanajikuta wanataka ushind,hahaha
 
tamko la mkuu wa kaya limetoka juzi tu leo utekelezaji umeanza.....yaani hizo juhudi zingekua kwy kukamata wauza madawa wa kulevya nchi hii isingekua ghala la madawa ya kulevya.
 
Mumesahau kama amri imetolewa juzi tu? wapigwe tu, unyonge basi.!
 
Safi sana, hongera sana jeshi letu la polisi, kazi iendelee
 
View attachment 139770

Polisi mkoani Iringa wakiwa wameuzuia msafara wa mgombea ubunge jimbo la Kalenga, Bi Grace Tendega kupitia CHADEMA kwa madai hawakuwa na kibali cha kufanya maandamano hayo ya magari hapa ni eneo la lango la mji Samora ambapo msafara huo ulikuwa ukitokea maeneo ya Ndiuka kuelekea kwa msimamizi wa uchaguzi ili kuchukua fomu.
Hata Dar kuna foleni kumbe unahitaji kibali ?
 
Kikwete atangaze hali ya hatari tujue moja kuliko kucontrol movement za watanzania kwa kisingizio cha kibali wangapi leo wametoka kalenga kwenda iringa mjini iweje hao wapewe kibano kikwete the hague inamgoja
 
Back
Top Bottom