Mpango wa kumtangaza Mwl. Nyerere Mtakatifu kuratibiwa na Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mchakato wa kumtangaza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuwa Mtakatifu ulioanzishwa na Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Musoma mkoani Mara nchini Tanzania umehamishiwa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Akizungumza leo Jumatatu Oktoba 14, 2019 wakati wa ibada maalum ya kumwombea Mwalimu Nyerere aliyefariki Oktoba 14, 1999, Paroko wa Kanisa Katoliki Parokia ya Butiama, Padre Daniel Inc amesema uratibu wa mchakato huo umehamishiwa chini ya Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC).

"Kwa kigezo kwamba Mwalimu Nyerere alikuwa kiongozi wa Kitaifa mchakato wa kumkangaza kuwa Mtakatifu sasa utasimamiwa na Baraza la Maaskofu badala Jimbo Kuu la Musoma kama ilivyokuwa awali," amesema Padre Inc

Kuhusu kuhamishiwa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padre Inc amesema "Kutokana na Mwalimu Nyerere kuishi na kusali Jimbo Kuu la Dar es Salaam kwa kipindi kirefu, mchakato wa kumtangaza kuwa Mtakatifu pia umehamishiwa huko."

Amewasihi waumini wa Kanisa Katoliki kufanya maombi kwa ajili ya Mwalimu Nyerere na kutangaza miujiza inayotokea wakati wa maombi hayo kama njia ya kufanikisha mchakato wa kumtangaza mwasisi huyo wa Taifa kuwa Mtakatifu.
 
Mimi huku siko kwanza, mpaka atangazwe mtakatifu maisha yake ya duniani yalikuwa ya kujitolea kwa wengine na ameacha mfano wa kuigwa.

Baada ya kifo chake ametenda muujiza. Mfano mgonjwa wa gonjwa sugu kupona kwa jina lake.

Baba Mtakatifu John Paul II ameshaponyesha watu cancer na yuko kwenye mchakato wa kutangazwa.
 
Mtakatifu kwenye hiyo dini Yao. Sisi tunamtambua ni mtu mchafu na mbaya kuliko Marais wote waliotangulia na motoni ndio makazi yake.. Allah umchome moto uunguzao kwelikweli
 
Wazungu bhana!! Haya mambo wameturithisha,ni wao waliotupoka Uhuru,wakatesa Babu zetu huku wakipenyeza dini zao,Leo kwa kupitia dini Yao wamfanye nyerere kuwa mtakatifu!! Au ndo tuseme lile jiwe kuu lililokataliwa na waashi leo limekuwa jiwe kuu la pembeni!! Hahaha waafrika bado tunaelea kwenye viganja vya mtu mweupe.
 
"Binadamu Ata Kama Ulikuwa Bora Kiasi Gani Ila Sikubaliani Na Ili Swala Kuitwa Mtakatifu Hapana Sizani Kama Ni Sahihi"

Nyerere Ni Babu Yetu Lakini Sikubaliani Na Ili Mwenye Heri Inatosha Na Mambo Aliyoyafanya Hakuna Asiyeyajua Tumuache Mzee Apumzike.

Kuna Siku Na Jiwe Atahitaji Kufanyiwa Ivyo Ili Awe Kama Nyerere"
 
Barikiwa sana Mkuu kumbe mara nyingine huwa na akili ee
Mimi huku siko kwanza, mpaka atangazwe mtakatifu maisha yake ya duniani yalikuwa ya kujitolea kwa wengine na ameacha mfano wa kuigwa.

Baada ya kifo chake ametenda muujiza. Mfano mgonjwa wa gonjwa sugu kupona kwa jina lake.

Baba Mtakatifu John Paul II ameshaponyesha watu cancer na yuko kwenye mchakato wa kutangazwa.
 
Acha urongo Tanzania hakuna mtakatifu hata moja ambaye ametangazwa

Wapo wawili tu ambao wapo kwenye daraja la kutangazwa

Nyerere mmoja wapo na mwingine mwanamama jina limenitoka
Kwahy saiv mtamwomba Nyerere..
Kanisa Katoliki saiv wanagawa Utakatifu kama Karanga tuu. Kuna mtu kafariki miaka mingi imepita, Kalimwa Utakatifu jana chap tu.

Sio ajabu wakaja kumpa Jiwe Utakatifu.

Mt. Yosefu, utuombeee

Mt. Mwlm Nyerere utuombee.
 
Utashangaa wewe na kizazi chako Ndio mtateseka

Kwasababu Nyerere anapendwa na 99% ya watanzania
Kumbuka maombi ya wachache hayana nguvu
Mtakatifu kwenye hiyo dini Yao. Sisi tunamtambua ni mtu mchafu na mbaya kuliko Marais wote waliotangulia na motoni ndio makazi yake.. Allah umchome moto uunguzao kwelikweli
 
Back
Top Bottom