Mpango wa kuanza ujenzi SGR Mijini wakati kipande cha Dodoma- Mwanza kinasuasua, nani ameubariki?

Mpango wa kuanza ujenzi SGR Mijini wakati kipande cha Dodoma- Mwanza kinasuasua, nani ameubariki?

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
161
Reaction score
200
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa taarifa kuwa hivi karibuni litaanza ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) katika miji, hususan Dar es Salaam, kama sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Serikali yenye lengo la kupunguza changamoto za usafiri mijini.

Baada ya kusoma taarifa hii, nimekuwa nikitafakari masuala kadhaa. Bila shaka natambua umuhimu wa treni za kisasa katika maeneo ya mijini, hasa Dar es Salaam ambako changamoto za usafiri ni kubwa.

Hata hivyo, swali linalojitokeza ni iwapo Serikali imejipanga ipasavyo kutekeleza mradi huu kwa wakati, ilhali bado kuna taarifa za kusuasua kwa ujenzi wa miundombinu ya SGR katika maeneo yaliyopewa kipaumbele, hususan kipande cha kutoka Dodoma hadi Mwanza.

Kumekuwepo na kasi ndogo ya utekelezaji wa mradi huo, hali inayozua maswali ya msingi: kwa nini vipande vilivyoanza kujengwa havikamilishwi kwanza ili vianze kutumika, badala ya Serikali kujiongezea mzigo wa miradi mipya, wakati ufanisi wa utekelezaji wa mpango uliopo unaonekana kuwa wa kusuasua?

Huenda maswali haya yasingekuwepo kama mradi ungekuwa ukitekelezwa kwa kasi inayostahili.

Hivyo, ni halali kujiuliza kama kweli kama Taifa tumejipanga vyema katika kusimamia miradi mikubwa kama hii, au kama miradi hiyo imekuwa ikifungua mianya ya uzembe na upotevu wa rasilimali.

Kama Taifa, tunapaswa kuwa na mipango thabiti ya uwekezaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo, badala ya kukimbilia miradi mingi kwa wakati mmoja ilhali uwezo wetu wa usimamizi wa miradi hiyo kwa pamoja bado ni mdogo.

Ni vyema TRC na Serikali kwa ujumla wakatafakari upya kabla ya kuanza ujenzi wa SGR katika maeneo mapya. Ni muhimu kujiuliza: kasi ya ujenzi wa SGR katika maeneo ambayo ujenzi tayari umeanza ikoje? Ikiwa kasi hiyo hiyo itatumika katika maeneo mengine, hali itakuwaje? Je, kweli tumejipanga kwa ufanisi katika usimamizi wa miradi hii mikubwa?
 
Ulaji. Siku hiz pesa ziko kwenye kuanzisha miradi mipya.

Waulize TRC kwa nini treni za ghorofa zimepark, kipande cha kuingia bandarini mbona kinasuasua, na maswali kibao kama lot 3,4 nk

Hawawi wawazi sana. Na serikali ni kama imewaignore, yaani sio kipaumbele chao.


Hii nchi inaumiza kichwa sana
 
Back
Top Bottom