Mpango uliovuruga mbwembwe za EX-Girlfriend

Kabla hujapata hasira na kuona huu ni utoto, hii ni social forum tu.

Watu wapo tofauti, soma kilichoandikwa na endelea na majukumu yako, watu hawafanani, kila mmoja ana mtazamo wake.

Ni katika mahusiano watu wanauana, kwa sababu hawajui kuwa kuna maisha baada ya kuachana.

Ni katika mahusiano unafunga ndoa leo lakini wiki moja baadaye upo na mchepuko

Ni katika mahusiano mke wa mtu anatoka na mlinzi wa getini

Ni katika mahusiano mume anatoka na housegirl

Halafu mwisho hizi ni stori tu jamaa ameamua ku-share. Inawezekana ikawa kweli ama ni fiction tu.
 

Ndugu umenikumbusha miaka minne iliyopita nikiwa naishi maeneo ya mbezi beach pale makonde. Kuna binti alikuja kuishi kwa aunt yake baada ya kuhitimu masomo yake ya chuo kikuu. Baada ya kumuona na kujua alipokuwa akiishi nilianza kumfatilia kwa karibu kwa muda mrefu usiopungua miezi tisa hivi. Ukweli alikuwa ni mzuri aliyeumbika na kujaaliwa neema za Allah kama wengi mjuavyo dada zangu wa kichaga walivyo. Kwa wakati wote huo sikuweza kuambulia chochote zaidi ya namba yake na simu na ahadi nyingi alizokuwa akinipatia pasipo utekelezaji. Ukweli nilikata tamaa na kuamua kumpotezea na kujisemea moyoni ‘sizitaki mbichi hizi’ hali moyoni nikiwa naendelea kufedheheka kumkosa mrembo huyu. Kuna binti mmoja nipo naye ofisi moja hapa town, huyu binti ana mchanganyiko wa kinyarwanda na uhaya ndani yake. Ni binti mmoja matata mnoo, aliyepanda hewani na shingo kama twiga wa Serengeti. Hapo kiunoni mpaka kwenye nyonga zake ndio usiseme. Nadhani wengi mnajua vile watoto wenye uasilia wa Kagame walivyo. Sasa hiyo siku huyu bintia kaniomba muda wa lunch nimsindikize kariakoo ili akanunue nguo zake na zawadi kwa ajili ya mama yake. Basi tukiwa kwenye mizunguko yetu kule madukani kariakoo; Hamad!!!!! Si nikamuona yule binti wa kichaga aliyewahi kunisumbua kwa muda mrefu pasipo mafanikio yoyote. Kwa ule muda yeye alikuwa hajaniona kwa kuwa nilikuwa mbali kidogo na lile duka alilokuwamo. Na kwa muda mfupi niliweza kubaini alikuwa akifanya kazi kwenye lile duka sababu alikuwa akiwahudumia wateja waliofika dukani pale kununua nguo. Bila ya kupoteza muda ilibidi nimhadithie tu kwa ufupi yule dada rafiki yangu ambaye aliniomba nimsindikize Kkoo. Alicheka sana na kuniambia twende pale pale dukani kwake then mengine niachie mimi. Tulipofika pale dukani kwake nami nikajifanya kama nimemsahau yule dada wa kichaga huku tukiendelea kuchagua nguo. Yule dada wa kitusi akaanza manjonjo yake pale dukani, mara kaniwekea mkono begani, kidogo kaniita baby, ili mradi tu kumkera yule mrembo wa kichaga. Na kiukweli yule binti wa kichaga hakuwa anamfikia hata robo ya uzuri mtoto wa kitusi. Gafla akatoka nje ya duka na kuaga anaenda kutafuta chakula cha mchana sababu hakuweza kuvumilia mbwembwe alizofanyiwa na mtoto wa Kagame. Ndio nikaamini wanawake wengi wanatesekaga na kuumia sana pale anapokuletea mapozi na kukudharau halafu siku akuone upo na mwanamke mkali, mzuri zaidi yake pasipo kujua hata kama yule mwanamke anaweza akawa ni mpemzi wako ama sio. Basi baada ya siku kadhaa yule binti wa kichaga akanitumia text za kejeli ‘hivi kuamua kunilitea yule mpenzi wako dukani ili uniumize au nini?’ Mimi nikamjibu hapana wala halikuwa lengo langu na pia sikuwa najua pale ni dukani kwenu. Basi akawa anaendelea kunitext na kunipigia simu mara kwa mara mradi aje kubaini ni vitu gani yule mwenzake (mtusi wa Kagame) alikuwa anafaidi nini kutoka kwangu. Kama ilivyo ada yetu wajuba hatunaga mambo ya ngonjera ngonjera. Siku moja nikamwambia weekend nitatembelea mbezi beach na wife (yule mdada wa kitusi), ila nitafika usiku wa saa tatu. Yeye hakujua lengo la mimi kumuambia nitafika mbezi usiku ni nini. Hatimaye, Siku ya jmosi ikafika. Simkumtafuta mpaka ilipofika saa mbili na nusu hivi usiku akanitext ‘mhh naona mwenzangu ndio kakukamata maana sio kwa kunichunia huko’ nikamjibu ‘nipo naye hapa napanga jinsi ya kumtoroka chap nije kwako’ kabla hajajibu nikamchota akili yake na kumwambia ‘ kwanini tusionane siku nyingine nikiwa na muda wa kutosha,? Yeye akasisitiza lazima niende kumuona hata kama ni dakika moja tu. Pale anapoishi kuna bonde kubwa la maji ambalo linapitisha maji kutoka goba juu mpaka kule baharini. Nikambia nitafika mpk pale ila sitaenda na gari ili wife asije kushtuka kama nimemtoroka akapata mashaka juu yangu. Kwenye text nikamtania ‘nilipokuja dukani kwako na wife niliona bikini zikiuzwa hivyo usisahu kuvaa mojawapo ya bikini’ nilijua hii text itampa ashki kwa namna moja au nyingine na pia ajue kuwa nilienda pale kwa kazi moja TU! Akanijibu ‘nyooo, bikini akuvalie mkeo unayemnunuliaga, siku utakayoninunulia ndio nitavaa’ Basi mjuba nikamwambia ‘ok usjali luv, nikifika hapo nitakupima nijue unavaa size gani’ Kabla sijaituma hii text akatuma text ‘Jamani hufiki tuuu, wakifunga geti hutoniona tena,’. Nikamjibu ndio nakaribia kufika kwenye bonde hapo anza kutoka ndani na usije umenivalia jeans kama unaenda dukani kwako, vaa kama vile unavyoendaga kulala chumbani kwako! Baada ya dakika kumi nilikuwa nimeshafika pale kwenye lile korongo la mto na kumjulisha kuwa nimeshafika. Huwezi amini mtoto alitoka nje ya geti akiwa amevaa night dress na kujifunga kanga kifuani. Yaliyojiri pale ni hatari tupu. Kwa wanaojua mambo ya Jungle Love wanaweza nielewa nini namaanisha. Nashukuru Mungu nimekuwa baba kwa ajili yake siku aliponizalia mtoto handsome.
 
Mkuu wewe sasa ndio umemuelewa mtoa mada.
Wanawake huwa wanatufanyia kusudi sana ila sasa ukimfanyia yeye lazima aonyeshe unyonge.
Hongera mkuu.
 

This is deadly, na ndivyo mabaharia hufanya sio kulia lia kama wakina Aslay na nyimbo zao
 
Hii kali sana. Hongera sana
 
vipi umemuoa?
 
Nilipofika katikati ya story tu nikajua mbeleni lazima huyo x akuletee uipige tena, ni wajinga sana wanawake
 
Hii ilifaa kuwa kwenye ule uzi wa kula tunda kimasihala
 
Dah hii stori yako imenukumbusha miaka kadhaa nyuma. Kuna binti nilikuwa namfuatilia, mtoto mmoja matata sana huyu nlikuwa nasali naye kanisani. Nishamtoa sana out maeneo mbalimbali plus vizinga vya hapa na pale lakini hataki kukubali ombi langu. Baada ya muda nikajiona bwege maana binti alikuwa ananiendesha anavyotaka.
Nikaamua kuendelea na maisha mengine,naye pia akapiga kimya kama hakuna kilichotokea. Baada ya muda idara ya vijana ikaandaa safari ya kwenda kutembea kwenye moja ya mbuga za wanyama hapa bongo. Wakati najiandaa kuchanga kwa ajili ya safari, nikaongea na dada mmoja ambaye ni wa dhehebu moja lakini anasali katika kanisa lingine jirani (Yaani mfano ni kama kanisa Katoliki Msimbazi na Kanisa Katoliki Magomeni). Binti akawa na interest za kwenda, hivyo ikabidi nimlipie pia.
Siku ya safari ndani ya Isuzu Journey nikiwa na mgeni wangu tukapanda na kuchagua siti ya watu wawili.
Safari nzima ilikuwa tuna ukaribu sana, ikiwemo kula chakula pamoja, tunagawana earphones, vicheko vingi kwenye gari na mambo mengineyo. Tulikuwa kama wapenzi na safari ilikuwa nzuri sana.
Niliweza kusoma huzuni machoni kwa yule binti mwingine kwa uwazi kabisa.
Baada ya safari alinitafuta mwenyewe na mimi nikajifanya nipo bize mwisho akatuma meseji, ‘’ yaani unanitongoza huku una mwanamke mwingine?’’ nikamjibu ’’ wewe si ulizingua’’ kwa kustaajabu akaandika ‘’mimi mbona nilikuwa nishakukubalia’’.

Kilichoendelea hapo ni historia.
 
Nzuri sana hii... Itanisaidia one day
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…