Mpanda: Wakazi wa Mpanda watakiwa kukithamini Chuo cha VETA Mpanda

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,815
11,991
Wakazi na wazawa Mkoa wa Katavi wametakiwa kuwasomesha vijana wao katika chuo cha Ufundi Stadi VETA Mpanda ili mkoa upate wataalamu watakaochochea shughuli za kiuchumi katika mkoa huo.

Maoni hayo yametolewa na Frank Atanas na Jesca Wambali ambao ni baadhi ya wazawa wa Katavi ambao wameiasa jamii kuondokana na mtazamo hasi wa kutoamini na kuheshimu kozi zinatotolewa katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA Mpanda.

Joshua Matagane ni mkuu wa chuo cha ufundi stadi VETA Mpanda amesema vijana wanaotoka Katavi ni 34 kati ya 122 ambao wamehitimu katika chuo hicho.

Geofrey Mwashitete ni Katibu Tawala Manispaa ya Mpanda ametumia muda huo kutoa rai wa wanachi wa mkoa huo kuhakikisha wanatumia chuo hicho katika kusoma kozi mbalimbali.

VETA Mpanda ni baadhi ya vyuo bora vya ufundi stadi hapa nchi ambao wahitimu wake wanajiriwa katika viwanda na taasisi za kiufundi mbalimbali hapa nchini na kilianzishwa tangu Mwaka 1983.
 
Back
Top Bottom