Chuo cha Veta Dodoma kifanyiwe uchunguzi

Ibanda1

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
705
1,092
Niwajulie hali wanajamvi

Kama kichwa cha habari kinavyochokoza mada. Nianze kwa kutoa pongezi kwa serikali kwa juhudi za kuwezesha elimu ya ujuzi kwa vitendo kupitia vyuo vya VETA ambao umesaidia vijana/mabinti wengi kujiajiri, ila kwa hili linaloendelea kwenye chuo cha VETA Dodoma halikubaliki ni ubabaishaji,wizi, ubadhilifu na ukiukwaji wa dhana na malengo ya chuo.

Mchongo uko hivi, Veta wanatoa mafunzo ya ujuzi kwa vitendo katika kada mbalimbali na hii ni programme maalumu ya serikali ili kuwawezesha vijana kupata ujuzi na kujiajiri hivyo serikali hutoa ruzuku ili kufanya gharama za kumudu mafunzo ziwe rafiki. Wanafunzi wa kutwa wanachangia Ada kiasi cha Tsh 60,000 na wanaokaa bweni ni Tsh 120,000 kwa mwaka.

Hawa jamaa walikuja na wazo zuri sana la mafunzo maalumu ya muda mfupi (Short course programme) ya miezi mitatu tu ila kilichonichosha ni Kiasi cha Ada ambayo imekuwa kubwa sana lakini hilo halikuwa jambo la kushangaza sana kwani niliamini ni kwa sababu wakufunzi wanatumia muda wa ziada kuendesha haya mafunzo basi watakuwa wanademand overtime.

Jambo lililozua ukakasi ni namna wakufunzi wanavyoratibu hayo mafunzo, nimepokea malalamiko kwa baadhi ya wanafunzi wanaosoma course ya food production ambayo ada yake ni almost 500k kwa miezi mitatu, unaambiwa hawana syllabus wala ratiba hivyo itategemea mwalimu ameamkaje siku hiyo, kila siku wanajifunza kupika wali samaki na ni miezi miwili sasa imepita tangu waanze course na wamebakiwa na mwezi mmoja tu kuhutimu mafunzo, mwanfunzi anatumwa akatafute order ya chakula mtaani kitu ambacho ni tofauti kabisa na jambo waliloendea kusomea. Walipojaribu kuhoji wanaambiwa kama kuna vyakula hukujifunza muhula huu basi unakaribishwa tena kujiunga na mafunzo kwenye mhula mwingine na inatakiwa tena ulipie 500k.

Chuo kinaendesha hii biashara ya kihuni ili kijipatia fedha ambayo haifanani na thamani ya taaluma wanayoitoa. Mkuu wa chuo hizi taarifa anazo lakini hakuna hatua amechukua tuona serikali iliangalia hili jambo chuo cha VETA Dodoma kuna uozo mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom