Wafanyabiashara wadogo katika Soko la Kilimahewa, linalotumiwa na machinga wadogo, wameathirika baada ya vitu vyao kubomolewa kwa madai ya kutengeneza mitaro.
Tukio hilo limeibua maswali kuhusu namna zoezi hilo lilivyotekelezwa na athari zake kwa wafanyabiashara wanaotegemea biashara hizo kujipatia kipato cha kila siku.
Je, wafanyabiashara walipewa taarifa ya mapema kabla ya kubomolewa kwa vitu vyao JIBU hapana.
Wakina mama wanaangaika huku na kule kuokoa mali zao kwani ndio msingi mkuu wa maisha yao.