Dar es Salaam: Machinga wa Karume waandamana kuelekea ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wasema hawana imani na Viongozi. Mabomu ya machozi yarindima

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
4,821
2,000
Wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga wa soko la Karume (Mchikichini) wameandamana hadi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kushinikiza kiongozi huyo atoe tamko la kuwaruhusu waendelee kufanya shughuli zao kwenye soko hilo.

Wafanyabiashara hao wameandamana leo Jumatatu Januari 17, 2022 ambapo walikuwa wanaimba "Tunataka Soko letu" wakiwa wamezingira geti la ofisi hiyo, ikiwa ni siku moja imepita tangu soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana.

Wakizungumza katika tukio hilo, baadhi ya wafanyabishara hao wamesema wanafanya hivyo baada ya kukosa imani na maamuzi yaliyochukuliwa na viongozi hao huku wakionyesha kusikitishwa kwao na kitendo cha wenzao kuvunjiwa mabanda yao waliyojenga usiku wa kuamkia leo na jeshi la polisi.

Silvanus Mwakipesile amesema Mkuu wa Mkoa aliwaahidi leo saa 2:00 asubuhi angefika kwenye soko hilo kuwaona na kuwapa muongozo lakini wanashangaa kabla ya kiongozi huyo kwenda kuna watu wamevunjiwa mabanda yao na sehemu hiyo kuwekwa chini ya ulinzi mkali ukisimamiwa na Jeshi la Polisi.

"Tumekosa imani na viongozi jana alisema anakuja lakini hadi sasa hatujamuona na chakushangaza waliojenga vibanda vyao wamebomolewa, sisi hatuwezi kuwasubiri wao maisha yetu magumu watuache tujenge wenyewe ili tuendelee kufanya kazi zetu," amesema

"Siku zilizotolewa kwa ajili ya kufanya uchunguzi ni nyingi tunataka tuachwe tujenge mabanda wakati uchunguzi ukiendelea na si kubaki hivihivi tutakula Nini na tunawatoto wanatakiwa kwenda shule,"amesema Saida Mohamed

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Ng'wilabuzu Ludigija amewaomba wafanyabishara hao kuwa wavumilivu na kufuata utaratibu uliotangazwa na Serikali kwamba waiachie kamati ifanye kazi kwa siku saba na kutoa ripoti badala ya kuandamana kutaka kushindana na Serikali.

"Mnatakiwa kujiongeza pamoja na kwamba mnadai haki lakini lazima mfuate utaratibu Jana Waziri tuiachie Kamati ifanye kazi na walete ripoti tunaomba kuweni na subira,"amesema.

Jana baada ya soko hilo kuungua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla aliwataka wafanyabiasha wa soko hilo kuwa watulivu huku akiahidi kuundwa kamati ambayo itachunguza chanzo cha moto huo kwa siku 14 akipiga marufuku shughuli zozote kuendelea wakati wa uchunguzi huo.

Muda mfupi baada ya RC Makalla kutoa tamko hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Innocent Bashungwa aliagiza kamati hiyo kufanya uchunguzi kwa siku saba badala ya 14.

UPDATES
POLISI WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUWATAWANYA MACHINGA WALIOANDAMANA
Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya Wafanyabiashara wa soko la Karume (Mchikichini) ambao wameandamana na kufunga barabara karibu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakishinikiza kuruhusiwa kuendelea na biashara katika soko hilo lililoungua

Wafanyabiashara hao maarufu walifunga Barabara kwa kutumia mawe na magogo katika makutano ya Uhuru na Kawawa, Ilala Boma wakimtaka RC Amos Makalla atoe tamko la kuwaruhusu waendelee kufanya shughuli zao kwenye soko hilo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa ameagiza Kamati iliyoundwa kufanya uchunguzi wa Moto uliotokea kwa siku saba.

Chanzo;- Mwananchi
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
10,457
2,000
Hii serikali imepoteza uaminifu kwa wananchi mapema sana, serikali haina huruma kabisa, watu wameunguliwa vibanda vyao wanajenga upya bado wanawavunjia tena?!

Na huyu Mkuu wa wilaya Ilala anaendeleza tamaduni ya kijinga, wasubiri nini wakati hawajui kula yao itatoka wapi? basi wagawieni mishahara yenu na marupurupu sio hizo ahadi hewa mnazowapa. Watu wanaungua Dsm jua kali nyie mko ofisi zenye AC mnawaambia wawe na subira?

Sasa naamini kuna uwezekano mkubwa serikali ikawa inahusika na haya matukio ya moto unaounguza masoko ya nchi hii usiku tu, hawa hawawezi kujichunguza ndio maana huwa hawatoi majibu ya ripoti za tume wanazounda, hawa ni corrupt.

Nawaunga mkono machinga kwa hatua walizochukua kudai haki yao sababu zote walizotoa ni za msingi kabisa, kama makundi mengine yangekuwa na uthubutu huo, nina hakika CCM ingebaki historia nchi hii.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
38,048
2,000
Wanadeserve wanachokipata kwa kuwa wakati CCM inapora chaguzi walikenua meno.

Watulia hivyo hivyo sindano iingie vizuri hadi watakapopata akili ya kuikataa CCM na mambo yake yote.

Nashukuru sana Mungu kuwa leo wamepelekewa askari wa kikosi cha mbwa ambao wameenda kubomoa vile vibanda vyao ambavyo walikuwa wameshaanza kuvijenga jana.
 
Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
3,976
2,000
Machinga wameandamana kwa mkuu wa mkoa Amos Makalla kushinikiza waachiwe eneo lao waendelee na biashara zao. Lakini hawajafanikiwa na hivyo kuanza kupigwa mabomu ya machozi ili waondoke eneo hilo.

Poleni sana wamachinga wote wa Karume, sasa ni wazi hamna chenu hapo. Ila binafsi nawaonea huruma sana, maana wamepoteza mitaji yao na eneo limeenda.
Poleni sana

=======

Wafanyabiashara ndogondogo maarufu machinga wa soko la Karume (Mchikichini) wameandamana hadi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla kushinikiza kiongozi huyo atoe tamko la kuwaruhusu waendelee kufanya shughuli zao kwenye soko hilo.

Machinga hao wameandamana leo Jumatatu Januari 17, 2022 ambapo walikuwa wanaimba "Tunataka Soko letu" wakiwa wamezingira geti la ofisi hiyo, ikiwa ni siku moja imepita tangu soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia jana.

POLISI WATUMIA MABOMU YA MACHOZI KUWATAWANYA MACHINGA WALIOANDAMANA

Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya Wafanyabiashara wa soko la Karume (Mchikichini) ambao wameandamana na kufunga barabara karibu na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wakishinikiza kuruhusiwa kuendelea na biashara katika soko hilo lililoungua

Wafanyabiashara hao maarufu walifunga Barabara kwa kutumia mawe na magogo katika makutano ya Uhuru na Kawawa, Ilala Boma wakimtaka RC Amos Makalla atoe tamko la kuwaruhusu waendelee kufanya shughuli zao kwenye soko hilo

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Innocent Bashungwa ameagiza Kamati iliyoundwa kufanya uchunguzi wa Moto uliotokea kwa siku saba.
 
Malimi Jr

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,103
2,000
Tuliolia kipindi cha mwendazake sasa ni wakati wa kucheka tu.

Tunataka mamalishe, machinga, wakulima & co wateseke kabisa maana ndiyo kubwa na hao ndiyo waliompa jeuri mwendazake.

Yako wapi sasa tuliwaambia wakashupaza shingo zao, acha sasa zivunjike.
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
47,888
2,000
Wanadeserve wanachokipata kwa kuwa wakati CCM inapora chaguzi walikenua meno.

Watulia hivyo hivyo sindano iingie vizuri hadi watakapopata akili ya kuikataa CCM na mambo yake yote.

Nashukuru sana Mungu kuwa leo wamepelekewa askari wa kikosi cha mbwa ambao wameenda kubomoa vile vibanda vyao ambavyo walikuwa wameshaanza kuvijenga jana.
Una uhakika kuwa hao wote walikenua hayo meno?
 
kijana13

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
1,696
2,000
Katika suala la soko kuungua hakuna kitu kinanisikitisha Kama mtu mtaji wake wote aliweka hapo kupotea ,hapo Kuna watu hawana kitu mfukoni then familia inamtegemea,Kodi, mikopo etc...Tuwaangalia watu kwa jicho la ubinadamu.. huwezi kuelewa Hadi yakukute..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom