Mpanda: Tundu Lissu ayalipua Maridhiano, Kingai, Byakanwa na Wambura Watajwa

Katika Muendelezo wa Mikutano ya hadhara inayoendelea kwenye Oparesheni 255 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) , ambayo sasa imeingia kwenye Mkoa wa Katavi , Tundu Lissu ameyataja mapungufu ya Maridhiano hadi sasa.

Akizungumza kwa kujiamini mbele ya Maelfu ya wananchi Lissu amesema kwamba , maana halisi ya maridhiano ni kuhakikisha kwamba Makandokando ya awali yaliyotokana na utawala wa kikatili wa awamu ya 5 yanaondolewa na kuanza ukurasa mpya.

Bali anashangazwa na kitendo cha washirika wa makandokando hayo kuendelea kupewa vyeo tena katikati ya naridhiano , Amemtaja IGP Camillius Wambura kama mpishi mkuu wa kesi zote za uongo zilizomkabili yeye mwenyewe , ambazo zimetupiliwa mbali mahakamani , anadai hakuna asiyejua upishi wa kesi za uongo wa Wambura , lakini aliteuliwa IGP

Tundu Lissu amefunguka kwamba Byakanwa ndiye aliyeharibu miundo mbinu ya Shamba la Kisasa la Freeman Mbowe , baada ya hapo akala shavu na kuwa RC wa Mtwara , na sasa ameteuliwa Balozi .

Lissu Amemtaja Ramadhan Kingai kama Mhalifu aliyetunga kila uongo kwenye kesi ya Ugaidi wa uongo iliyomkabili Mbowe , hata baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali Kingai akapandishwa Cheo , Lissu amedai kwamba katika wahalifu wa awamu ya 5 ni Sabaya Pekee aliyejaribu kushughulikiwa.

Tundu Lissu amependekeza Maridhiano ni lazima kweli yazingatie kuondoa matatizo pamoja na walioyaleta .
Kuna haja ya kuyafanyia kazi maneno yake hayo.....

Taifa letu ni moja....sisi ni wamoja....katika "reconciliation" kunahitajika sana kuelezana kinagaubaga......

Kwa haya simpingi mh.Tundu Lissu kwani mimi si mgonjwa wa "Mirembe"......

#SiempreJMT
 
Elimu imeshiba.....vilaza tu waliojaza ugali kichwani ndio watapinga
Honestly nchi haina social educator tangu nyerere na hii imepekekea jamii yetu kuwa hivi ilivyo katika historial nyerere pekee ndo aliiweza hii kazi sasa huyu bingwa binafsi nafurahia nondo zake .he is valued politician
 
Katika Muendelezo wa Mikutano ya hadhara inayoendelea kwenye Oparesheni 255 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , ambayo sasa imeingia kwenye Mkoa wa Katavi, Tundu Lissu ameyataja mapungufu ya Maridhiano hadi sasa.

Akizungumza kwa kujiamini mbele ya Maelfu ya wananchi Lissu amesema kwamba , maana halisi ya maridhiano ni kuhakikisha kwamba Makandokando ya awali yaliyotokana na utawala wa kikatili wa awamu ya 5 yanaondolewa na kuanza ukurasa mpya.

Bali anashangazwa na kitendo cha washirika wa makandokando hayo kuendelea kupewa vyeo tena katikati ya naridhiano , Amemtaja IGP Camillius Wambura kama mpishi mkuu wa kesi zote za uongo zilizomkabili yeye mwenyewe , ambazo zimetupiliwa mbali mahakamani , anadai hakuna asiyejua upishi wa kesi za uongo wa Wambura , lakini aliteuliwa IGP

Tundu Lissu amefunguka kwamba Byakanwa ndiye aliyeharibu miundo mbinu ya Shamba la Kisasa la Freeman Mbowe , baada ya hapo akala shavu na kuwa RC wa Mtwara , na sasa ameteuliwa Balozi .

Lissu Amemtaja Ramadhan Kingai kama Mhalifu aliyetunga kila uongo kwenye kesi ya Ugaidi wa uongo iliyomkabili Mbowe, hata baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali Kingai akapandishwa Cheo , Lissu amedai kwamba katika wahalifu wa awamu ya 5 ni Sabaya Pekee aliyejaribu kushughulikiwa.

Tundu Lissu amependekeza Maridhiano ni lazima kweli yazingatie kuondoa matatizo pamoja na walioyaleta .
",Mama anaupiga mwingi".

Simjui mwasisi wa msemo huu na maana aliyolenga kuiwasilisha kwa maneno hayo lakini ninakubaliana naye, kwa maana ninayoupa msemo wenyewe.

Kuna watu hudanganyika kiwepesi sana, hata bila ya kufikiri chochote juu ya wanachodanganywa juu yake. Lissu siyo mmoja wa watu wa aina hiyo.
 
Maridhiano ni pamoja na kusahau yaliyopia! Lissu hawezi na hana uwezo wowote wa kuwa kiongozi!

Maridhiano mazuri ni kuacha ya kale yapite ili ukurasa mpya uchukue hatua zake
Hao walioteuliwa ndio "ukurasa mpya"?

Hivi watu kwa nini hupenda kujitoa akili namna hii?

Hao walioteuliwa, wakiwa na shutuma za kusababisha mitafaruku, utawasahau vipi huku kila siku wakikukumbusha mabaya yaliyotendeka?

Unapojitambulisha kuwa wewe ni 'kisamv', jaribu kuonyesha tofauti kati ya uwezo wa akili yako na hicho kitoweo.
 
Reconciliation.....

"Reconciliation" ina mambo yake.....japo Tanzania haijawahi kutokea yaliyotokea Rwanda ila mahakama za jirani zetu "GACACA" zinaweza kutupa "akiba ya rejea" katika "suluhu" zetu.....

Mathalani katika hizo mahakama....WAHANGA NA NDUGU ZA WAHANGA WA PANDE ZOTE hawakuzuiwa "penting up"....kufunguka...kwa yaliyotokea....huwezi kuleta TIBA(healing) kwa kufichaficha baadhi ya mambo ilihali walioumia/kuumizwa bado wana vidonda.....

Hivyo ndivyo ilivyo "reconciliation"....GACACA inatupa mwanga mzuri tu......

#SiempreJMT
 
",Mama anaupiga mwingi".

Simjui mwasisi wa msemo huu na maana aliyolenga kuiwasilisha kwa maneno hayo lakini ninakubaliana naye, kwa maana ninayoupa msemo wenyewe.

Kuna watu hudanganyika kiwepesi sana, hata bila ya kufikiri chochote juu ya wanachodanganywa juu yake. Lissu siyo mmoja wa watu wa aina hiyo.
Mkuu Chadema ni akili kubwa , hii ni gane plan

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Hao walioteuliwa ndio "ukurasa mpya"?

Hivi watu kwa nini hupenda kujitoa akili namna hii?

Hao walioteuliwa, wakiwa na shutuma za kusababisha mitafaruku, utawasahau vipi huku kila siku wakikukumbusha mabaya yaliyotendeka?

Unapojitambulisha kuwa wewe ni 'kisamv', jaribu kuonyesha tofauti kati ya uwezo wa akili yako na hicho kitoweo.
, kumbuka kwamba majina huumba

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Mkuu Chadema ni akili kubwa , hii ni gane plan

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
Nimefikiria kumwanzishia huyu Bwana Lissu mada maalum kwenye ukumbi huu wa JF, lakini nasita.

Kuna watu ambao hata ufanye nini, huwezi kamwe kuwanyamazisha. Lissu ni mtu wa namna hiyo.

Kinyume chake, hivi sasa watu wangekuwa wanaulizana juu yake hukuyeye akiwa anasononeka huko alikojifichia kwa maumivu makubwa.

Mfano hapa, naweza kutoa mtu kama Dr Ulimboka. Kuna mtu yeyote anayemkumbuka tena? Ni kama aliuawa moja kwa moja, pamoja na kwamba naye alikuwa manusra.

Nchi nazo ziko hivyo hivyo. Kuna nchi ambazo zinatishwa tu, na kuufyata mkia na kushika adabu; na kuna nchi pia ambazo hata uwe na maguvu kiasi gani, huwezi kuwanyanyasa hata kama unayo maslaha chungu nzima.

Mfano mzuri hapa ni Vietnam. Vijamaa vilikataa kunyanyaswa, vikachakazwa hovyo hovyo, lakini vikaendelea kuuma meno hadi mwenye maguvu akasalimu amri. Leo hii nchi hiyo ya Vietnam inaendelea kwa kasi, kiasi kwamba nao sasa ni wawekezaji kwetu (Halotel).

Kwa hiyo, mtazame vizuri Tundu Lissu. Huyu ni kiongozi ambaye anazo sifa tofauti sana na viongozi wengine.

Acha nisikuchoshe. Lakini ninakutahadharisha, usianze kunivisha lebo ya uchawa. Ninao uwezo wa kugeuka haraka sana na kuwa koboko. EnHeeee Heeee!

Natamani sana angeanza kuzungumzia maswala ya msingi na ya muhimu zaidi, maswala yanayohusu hali mbovu za maisha ya wananchi wa hali duni, na hata hao wanaotulangua huko Kariakoo na kwingineko. Sote tunahitaji uongozi wenye dira kututoa hapa na kutusukuma mbele.

Ikikupendeza, tafadhali mfikishie ujumbe huu.
 
Katika Muendelezo wa Mikutano ya hadhara inayoendelea kwenye Oparesheni 255 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , ambayo sasa imeingia kwenye Mkoa wa Katavi, Tundu Lissu ameyataja mapungufu ya Maridhiano hadi sasa.

Akizungumza kwa kujiamini mbele ya Maelfu ya wananchi Lissu amesema kwamba , maana halisi ya maridhiano ni kuhakikisha kwamba Makandokando ya awali yaliyotokana na utawala wa kikatili wa awamu ya 5 yanaondolewa na kuanza ukurasa mpya.

Bali anashangazwa na kitendo cha washirika wa makandokando hayo kuendelea kupewa vyeo tena katikati ya naridhiano , Amemtaja IGP Camillius Wambura kama mpishi mkuu wa kesi zote za uongo zilizomkabili yeye mwenyewe , ambazo zimetupiliwa mbali mahakamani , anadai hakuna asiyejua upishi wa kesi za uongo wa Wambura , lakini aliteuliwa IGP

Tundu Lissu amefunguka kwamba Byakanwa ndiye aliyeharibu miundo mbinu ya Shamba la Kisasa la Freeman Mbowe , baada ya hapo akala shavu na kuwa RC wa Mtwara , na sasa ameteuliwa Balozi .

Lissu Amemtaja Ramadhan Kingai kama Mhalifu aliyetunga kila uongo kwenye kesi ya Ugaidi wa uongo iliyomkabili Mbowe, hata baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali Kingai akapandishwa Cheo , Lissu amedai kwamba katika wahalifu wa awamu ya 5 ni Sabaya Pekee aliyejaribu kushughulikiwa.

Tundu Lissu amependekeza Maridhiano ni lazima kweli yazingatie kuondoa matatizo pamoja na walioyaleta .
As usual, Mr Tundu is off the mark, badala ya kumsifia Rais kutetea maridhiano anamlaumu. Kesi zake Mr Tundu ni jambo binafsi huwezi kuliingiza kwenye Katiba wala kulipa tumehuru. Ni kweli alitoa matusi, ni kweli ni mchochezi, kila siku hadibleo anatoa uchochezi na matusi juu yaxwatu wengi tu, he is not above the law. Kesi ya uhaini ya Mheshimiwa Mbowe ni baraka kwake, kaponea chupuchupu angenyongwa. Ni kweli alikodisha makomandoo watatu na kuwalipa nauli na posho ili wakamuue Alexander Lengai Nurk ole Sabaya, DC wa Hai. Kampuni ya tigopesa ilitoa ushahidi kamilifu kuwa hela zilitumwa na kupokelewa. Afande Urio aliyetumwa kuwatafuta wauaji ushahidi wake haujakanushwa kwani maongezi yakwe yalinaswa. Makomandoo walikuwa safarini kwenda kumuua ole Sabaya wapumbafu wakaamua kupitia Club ya mbege kuchati na wahudumu pale Rau Madukani ushahidi uko. Wakiwa hapo ndipo wakakamatwa na Afande Jumanne kwa uongozi wa mpelelezi mkuu Kachero Ramadhani Kingai. Ndipo ikawa DC ole Sabaya amepona kuuliwa. Angeuliwa makamandoo wangekamatwa wangenyongwa naovwangemtaja Mheshimiwa Mbowe naye angenyongwa sawia. Katika yote haya sifa ni za Kachero Afande Kingai. Alichofanya Rais ni kufuta kesi kuona ole Sabaya amepona. Ni maridhiano makuu.
 
Wajitoe kwenye .maridhiano kama kweli wako serious
Nilikuwa naitafuta pointi hii bahati nzuri nimeipata kwako, nawashangaa sana wanavyozidi kupiga kelele kila siku halafu bado wako humo ndani, kisingizio ni maridhiano ya Mbowe na Samia..

Sasa kama Mbowe anawaburuza hivyo huko Chadema wamebaki wanafanya nini? kuna vitu vingine vinashangaza sana, kama sio kuchekesha, hawa vipofu wanatengeneza makundi ndani ya chama chao lakini hata hawaoni!.
 
Back
Top Bottom