Mpanda: Tundu Lissu ayalipua Maridhiano, Kingai, Byakanwa na Wambura Watajwa

Kama Lisu bado ana siasa za namna hii anafeli pakubwa sana,hizi siasa za lawama zimepitwa na wakati ,aseme atafanya nini tofauti na CCM ikiwa atakamata dola,aache porojo
Kama ni siasa mbaya na bado ana wafuasi wengi kiasi kile basi hizo siasa zake zinafaa
 
Katika Muendelezo wa Mikutano ya hadhara inayoendelea kwenye Oparesheni 255 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA ) , ambayo sasa imeingia kwenye Mkoa wa Katavi , Tundu Lissu ameyataja mapungufu ya Maridhiano hadi sasa.

Akizungumza kwa kujiamini mbele ya Maelfu ya wananchi Lissu amesema kwamba , maana halisi ya maridhiano ni kuhakikisha kwamba Makandokando ya awali yaliyotokana na utawala wa kikatili wa awamu ya 5 yanaondolewa na kuanza ukurasa mpya.

Bali anashangazwa na kitendo cha washirika wa makandokando hayo kuendelea kupewa vyeo tena katikati ya naridhiano , Amemtaja IGP Camillius Wambura kama mpishi mkuu wa kesi zote za uongo zilizomkabili yeye mwenyewe , ambazo zimetupiliwa mbali mahakamani , anadai hakuna asiyejua upishi wa kesi za uongo wa Wambura , lakini aliteuliwa IGP

Tundu Lissu amefunguka kwamba Byakanwa ndiye aliyeharibu miundo mbinu ya Shamba la Kisasa la Freeman Mbowe , baada ya hapo akala shavu na kuwa RC wa Mtwara , na sasa ameteuliwa Balozi .

Lissu Amemtaja Ramadhan Kingai kama Mhalifu aliyetunga kila uongo kwenye kesi ya Ugaidi wa uongo iliyomkabili Mbowe , hata baada ya kesi hiyo kutupiliwa mbali Kingai akapandishwa Cheo , Lissu amedai kwamba katika wahalifu wa awamu ya 5 ni Sabaya Pekee aliyejaribu kushughulikiwa.

Tundu Lissu amependekeza Maridhiano ni lazima kweli yazingatie kuondoa matatizo pamoja na walioyaleta .
Mh Tundu lisu fanyeni siasa safi zama zimebadilika sana hii mambo yakutaja majina italitesa Taifa bila sababu.
 
Maridhiano ni pamoja na kusahau yaliyopia! Lissu hawezi na hana uwezo wowote wa kuwa kiongozi!

Maridhiano mazuri ni kuacha ya kale yapite ili ukurasa mpya uchukue hatua zake
huyu Lisu si ndo yule aliwashauri chadema waingie mkataba hata na shetani (ambaye angemwaga makafara) alimradi tu wakamate nchi? kama ulisoma kitabu cha dr.slaa utaelewa. umeona watu waliokuzwa maisha ya kishirikina wanawaza ushetani all the time? tutaaminije sasa kama huko ulaya ambako walikuwa wanamtunza hajaingia mkataba na freemason akamate nchi ili aiuze mazima? manake yeye yupo tayari kwa lolote alimradi tu ashike nchi.
 
Uongo mtupu
 
Kama Lisu bado ana siasa za namna hii anafeli pakubwa sana,hizi siasa za lawama zimepitwa na wakati ,aseme atafanya nini tofauti na CCM ikiwa atakamata dola,aache porojo
Unadhani hayo tu ndio aliyoongea kwenye huo mkutano? Hiki ulichopewa hapa ni sehemu ndogo tu ya alichoongea.
 
Mh Tundu lisu fanyeni siasa safi zama zimebadilika sana hii mambo yakutaja majina italitesa Taifa bila sababu.
Kwasababu ww ulishiriki ule uovu, basi unataka watu wakae kimya bila kutaja majina ya hao waliokuwa wakiendesha uhayawani, ili huko mbeleni mrudie tena tabia hiyo.
 
huyu Lisu si ndo yule aliwashauri chadema waingie mkataba hata na shetani (ambaye angemwaga makafara) alimradi tu wakamate nchi? kama ulisoma kitabu cha dr.slaa utaelewa. umeona watu waliokuzwa maisha ya kishirikina wanawaza ushetani all the time? tutaaminije sasa kama huko ulaya ambako walikuwa wanamtunza hajaingia mkataba na freemason akamate nchi ili aiuze mazima? manake yeye yupo tayari kwa lolote alimradi tu ashike nchi.

Utamuuzia nani nchi masikini hii? Au unadhani hao wazungu wanaitaka sana nchi yetu?
 
Maridhiano ni pamoja na kusahau yaliyopia! Lissu hawezi na hana uwezo wowote wa kuwa kiongozi!

Maridhiano mazuri ni kuacha ya kale yapite ili ukurasa mpya uchukue hatua zake
Ulishawahi kupigwa japo kokoto lwa kutumia manati wewe ? Unaongea ukijigeuza kwenye sofa? Unataka mtu aliyeshambuliwa kwa risasi kama jambazi tena kwa kusema ukweli asamehe ?
 
uongo kwasababu hujasoma kitabu cha dr slaa au uongo kwasababu unaamua tu kusema ni uongo?
Kwani kitabu cha Dr. Slaa ni Qoran au Bible? Kitabu cha Dr.Slaa kitabu cha Dr.Slaa, kama unakiona ni kitabu cha maana hiyo ni kimpango wako.
 
Ulishawahi kupigwa japo kokoto lwa kutumia manati wewe ? Unaongea ukijigeuza kwenye sofa? Unataka mtu aliyeshambuliwa kwa risasi kama jambazi tena kwa kusema ukweli asamehe ?
Mkuu, asiposamehe ndo atarudi kama alivyokuwa?

Ni kweli haiwezekani kusahau, lakini utafanyeje sasa mkuu, ni kusamehe tuu ili maisha mengine yaendelee
 
32 Reactions
Reply
Back
Top Bottom