Mpambe wa Rais Magufuli abadilishwe

Mpambe wa Rais Magufuli abadilishwe

Kuna uzi moja ulianzishwa kipindi cha nyuma ukimuongelea huyu mpambe. Nilimtetea kwa kiasi kikubwa kwa kuzingatia kwamba Rais Magufuli ni Rais ambaye yupo tofauti kabisa na marais waliomtangulia. Yeye hana utulivu, lolote wakati wowote anapoana anapenda kulifanya anafanya. Mfano, amewaona wanakwaya, huyoo anaenda kuimba nao, mfano amewaona wapiga ngoma, huyoo anaenda kupiga ngoma.

Huyu mpambe wake kwa muda wote ambao amekuwa na Rais ameshidwa kuendana naye, ana uzubaifu kwa kiasi fulani, au pengine Rais yupo phisical fit zaidi yake yeye. Pengine anachoka na speed ya Rais ya kazi kazi. Dom-Arusha-eco bank- uganda.

Mfano wa picha hii, huyu mlinzi wa uganda amechukua position yake ambayo kimsingi kama ana jambo baya lolote, hapo ni shida.

View attachment 346675

=====================

Angalia vizuri kijana. Na huyo mpambe wa magufuli pia ameshika mwamvuli. Usikurupuke
 
Nilijibu kwa ufupi...Inaelekea unaleta mjadala ambao kwa maoni yangu hauna tija...Aide de camp ni aide de camp...ana majukumu yake na walinzi wana majukumu yao....lakini haina maana jambo baya likitokea yeye aangalie tu kwa kuwa eti ni aide de camp ndiyo maana wana sifa nyingine za ziada, wakati mwingine zikiwemo za ukomando na kadhalika...naona niishie hapo, mijadala ya aina hii ni useless, tunaingilia na kuongelea mambo yasiyotuhusu...
Useless wapi wewe wakati hapa wengine tunajifunza kitu
 
Watu mmemkomalia huyo ADC kuwa abadilishwe,akibadilishwa tunafaidika nn sijui, hayo mambo ya ulinzi na usalama tuwaachie wenye fani yao,,,,,kwanza huyo ADC kiukweli yupo fiti kuliko maelezo,

Rais ni Nyumba na ADC ni Earth Wire. Tafakari vizuri nilichokiandika na utapata jibu litakalokufanya uweze kufikiri vizuri humu kama Great Thinker.
 
Kwa Uganda usiwe na wasiwasi labda ingekuwa Rwanda ndiyo ningeshituka kidogo, museveni hawezi kuwasaliti JWTZ wakati alishirikiana nao kumtoa nduli idd amin kagera na hatimaye kumtoa Uganda ndiyo maana hata huyo JW amerelax kwa sababu anaona yupo nyumbani

Mkuu katika wadhifa wa usalama wa Raisi Ni kinyume Na mafundisho Yao kurelax Au kumuamini mtu yeyeto.Hata akiwa mzazi wako.
 
Useless wapi wewe wakati hapa wengine tunajifunza kitu

Samahani kwa kutumia neno 'useless'...ni kweli JF jukumu lake mojawapo ni kuelimishana, unisamehe kwa hilo, ila kuna mambo mengine siyo lazima tuingie kwa undani zaidi...unajua comrade, wako wengine ni wabishi mtu unamwambia majukumu ya aide de camp siyo ya ulinzi as such lakini anabisha tu...anataka watu wachokonoe hata yale mambo ya kiusalama kwa viongozi wetu, sasa hiyo siyo sahihi...ndiyo maana nikasema mijadala ya aina hii tuwaachie wenyewe wahusika watekeleze majukumu yao...
 
Rais ni Nyumba na ADC ni Earth Wire. Tafakari vizuri nilichokiandika na utapata jibu litakalokufanya uweze kufikiri vizuri humu kama Great Thinker.

We mnyarwanda mbona umekomalia Sana suala LA mlinzi wa prezidaa wetu, VP kwani,Una ajenda ya siri nini. Nahisi upo kikazi zaidi
 
We mnyarwanda mbona umekomalia Sana suala LA mlinzi wa prezidaa wetu, VP kwani,Una ajenda ya siri nini. Nahisi upo kikazi zaidi

Naona Kazi mliobaki sasa kunitajia kuwa ni yangu labda ni kuwa Mzibua Vyoo tu kwani mmeshanihisi vibaya na kunipachika Kazi ambazo binafsi naona SITHUBUTU hata kuzifanya. Halafu sijui kwanini ikitokea tu Mtu humu kaleta UZI wa Kijasusi na nikaleta PUA yangu humu Watu mtatoka huko maporomokoni mlipo na kuja kuanza kunishutumu kuwa Mimi ni AGENT na NATUMIKA. Nitawasumbueni sana na endeleeni hivyo hivyo kuhisi na kunipachika ajira mbalimbali.
 
Kama Angekuwa Hausili Na Maswala Ya Ulinzi Jibu Haya Maswali.
1. Kwanini ADC Lazima Awe Askari Na Si Raia?!.

2. Kwanini ADC Awe Askari Mwenye Mafunzo Maalumu Na Si Askari Yeyote?!.

3. Kwanini ADC Lazima Atoke JWTZ Na Si Jeshi Lingine Tz?!.

4. Kwanini Ni Lazima Awe Gazetted Officer Na Si Rank&File?!.

Stricker Na Deffender Wanacheza Uwanja Mmoja Lakn Position Tofauti. Licha Ya Kwamba Deffender Kapewa Kazi Ya Ulinzi Na Stricker Kapewa Kazi Ya Kufunga Lakn Bila Kujali Position Zao Uwanjani, Kila Mchezaji Kwa Position Yake Anajukumu La Kulinda Lango Lake/Kufunga Goli Pale Inapobidi Bila Kujali Position Alopangwa Na Kocha.

Nafikiri Umanielewa.
Nakukumbusha. Jukumu La Ulinzi Hata Yeye Analo Kwa Nafasi Yake Akishirikiana Na Walinzi Wengine.
Inaonekana unajaribu kuongelea jambo ambalo ama huna taaluma nalo ama hulifahamu vizuri. Mfano mzuri hapo nambari 3, unaweza kukumbuka wakati wa enzi za Mwalimu J.K.Nyerere alipokuwa Rais, Philemon Mgaya alikuwa ADC wake; huyu alitoka Jeshi gani?
 
Swali lako linahitaji majibu nyeti, sasa tunaogopa kumwaga kuku kwenye mchele mwingi.
 
Pole Sana Ndugu. Nafikiri Ulijibu Kitu Ambacho Hukijui Na Baada Ya Kukutana Na Majibu Yaloshiba Unakimbia Kwa Namna Yako.

Ulijibu "ADC Hausiki Na Ulinzi)
Mimi Sina Nia Ya Kuleta Mjadala Wewe Ndio Unauleta. Kama Ungekuwa Mwelevu Ungejibu Kifupi Tu Kwmb "Nimeelewa Au Nashukuru" Sasa Shida Yako Ni Kwmb Hutaki Kuonekana Kwmb Umekosea So Unatengeneza Excuse. Kwani Ukikiri Umekose Huwa Unaumia Sana Eeh?!, Basi Pole Ndugu Natumai Umenielewa.
Kwa jinsi nilivokusoma ww jamaa unapenda ligi za kitoto
 
sijafurahi huyo askari wa uganda anavyoonekana kuwa karibu zaidi na magufuli kuliko mlinzi wetu. sijapenda.
 
Inaonekana unajaribu kuongelea jambo ambalo ama huna taaluma nalo ama hulifahamu vizuri. Mfano mzuri hapo nambari 3, unaweza kukumbuka wakati wa enzi za Mwalimu J.K.Nyerere alipokuwa Rais, Philemon Mgaya alikuwa ADC wake; huyu alitoka Jeshi gani?
Ok Nimekuelewa Lakn Nashangaa Unaniita Si Mtaalamu Kwa Point1 Namba3 Nyingine Huzioni.

Unaloongea Sikatai Lakn Angalia Enzi Za Mwl Na Sasa Mambo Yamebadilika Sana.
Enzi Za Mwl Hata Wasomi Tz Walikuwa Wachache Sana.

Hata Hivyo Ni Vyema Ukasema Mwaka Gani Coz Mwl Kaongoza Hadi 1985 So Kwa Kipindi Chote Hicho Kabadilisha Ma ADC Kadhaa.

Kumbuka Pia Viongozi Wa Kipindi Kile Walikuwa Lazima Wapite JKT So Ni Product Ya JW Pia.
 
Ujinga wa mtu mmoja umenifanya na mimi kujua ambalo sikulijua, hata maana ya ADC sikuijua.
 
mleta mada umekurupuka..jifunze itifaki na mambo kama hayo
 
Back
Top Bottom