kwamtoro
JF-Expert Member
- Nov 15, 2010
- 4,922
- 3,236
Kuna uzi moja ulianzishwa kipindi cha nyuma ukimuongelea huyu mpambe. Nilimtetea kwa kiasi kikubwa kwa kuzingatia kwamba Rais Magufuli ni Rais ambaye yupo tofauti kabisa na marais waliomtangulia. Yeye hana utulivu, lolote wakati wowote anapoana anapenda kulifanya anafanya. Mfano, amewaona wanakwaya, huyoo anaenda kuimba nao, mfano amewaona wapiga ngoma, huyoo anaenda kupiga ngoma.
Huyu mpambe wake kwa muda wote ambao amekuwa na Rais ameshidwa kuendana naye, ana uzubaifu kwa kiasi fulani, au pengine Rais yupo phisical fit zaidi yake yeye. Pengine anachoka na speed ya Rais ya kazi kazi. Dom-Arusha-eco bank- uganda.
Mfano wa picha hii, huyu mlinzi wa uganda amechukua position yake ambayo kimsingi kama ana jambo baya lolote, hapo ni shida.
=====================

Ni hivi, Rais anapowasili nchi nyingine mpande wake anakuwa ni msaidizi kwa mafaili yake. Kuna kuwa na mpambe mwenyeji ambaye ndio anachukua jukumu kubwa wakati wa kumpokea na kwenye dhifa mbalimbali. Mfano angalia wakati rais Magufuli anakagua gwaride mpambe wake anakuwa mwenyeji na huyu anakuwa pembeni mbali. Mfano mwingine angalia wakati rais wa Vietnam alipokuja alipewa mpambe wake. Hivyo hiyo picha isikusumbue, suala la kumshikilia mwavuli rais lilikuwa la huyo mwenyeji. Nafikiri umenielewe kidogo.