Mpaka wasalimu amri; Hatutishwi tena! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpaka wasalimu amri; Hatutishwi tena!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 30, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Baada ya serikali ya CCM kuwalea na kuwadekeza wezi wa mali zetu; baada ya serikali hiyo kuremburiana macho na mafisadi kwa miongo kadhaa sasa; baada ya kuonesha woga na kutokujiamini mbele ya wale wanaotufanya tuwe duni mbele zao sasa nasema imetosha!

  Kama vile utungu wa mama kuzaa nchi yetu ndio imefika na wakati wa mwana kuzaliwa lazima iwe mwaka huu kwani hatuwezi kuendelea kupiga kambi kuzungumzia watu wale wale miaka mitatu sasa! Na wengine tumewazungumzia miaka 10 sasa.

  Kuna kundi la Wananchi ambao uzalendo wao ulishawatoka siku nyingi na kwa muda mrefu wamebakia kufurahia mali za nchi yetu. Kundi hili linaendelea kutaka kutawala bila kuhojia au kupigiwa kelele. Wanataka wawe kama yule anayekula kisicho chake na hata ukitaka kupiga kelele anakunyoshea kidole na kukuambia 'shssssssss' Kwamba wewe muibiwa usipike kelele badala yake umuombe aache kula!

  imetosha. Kuna kundi la watu ambao ni lazima wachukuliwe hatua au milele tunaweka kwenye notisi kuwa mbele zenu hatugwai na katika altare zenu za ufisadi hatupigi magoti. Tunawashuhudia wale ambao wanatetemeka mbele zenu ambao leo wanajitokeza kuwatetea ati kwa misingi ya "kufuata haki"! Je mlipovunja haki za wananchi wa tAifa hili kuishi katika neema mbona hamkutetea? Mlipogawiana mali ya wana na mabinti wa taifa hili kama urithi wa kizazi chenu mbona hamkupigiwa kelele! Sasa yatosha.

  Wafuatao nawatangaza daima kuwa ni maadui wa Tanzania na maslahi yake. Ni maadui wa maendeleo yetu na mmoja mmoja na kama kundi wanaleta mbele yetu hatari iliyo wazi na dhahiri. Kundi la watu hawa wanatakiwa waogopwe makampuni yao yasusiwe na miradi yao isusiwe daima!

  1. Benjamin William Mkapa
  2. Rostam Aziz
  3. Apson Mwang'onda
  4. Yusuph Manji
  5. Gen (mstaafu). Robert Mboma
  5. Vincent Mrisho
  6. Anna Mkapa
  7. Andy Chande
  8. Andrew Chenge
  9. Nimrod Mkono
  10. Yeyote anayewaunga mkono, kuwatetea, kuwasafisha au kuwaita ni watu safi!

  Na kutoka na kundi hilo ushirika wao wa uovu umetandaa kila kona na sekta ya nchi yetu. Ni kundi hili na makuwadi wao wanatufanya tuishi kama wageni katika nchi yetu na majina yao yatajwapo tunatakiwa kutetema kama mitete!

  Watu hawa na wale wengine ambao tayari wanajulikana ndio kwa kiwango cha juu kabisa wamefunya urithi wetu kuwa asili ya utajiri wao. Wametumia upole na ukimya wetu kututisha na sasa wanajiandaa kutumia nguvu ya dola ambayo wao wameitengeneza kulinda maslahi yao ili kututisha na kutunyamazisha.

  Mara moja na daima nakataa milele kutetemeka mbele ya kundi hili na wapambe wao. Nakataa kufumba macho mambo waliyoyafanya katika Taifa hili na kuogopa hata kuwataja majina ati kwa vile "ni viongozi fulani". Laana hiyo ya woga iwaendee makuwadi wao na uzao wao!

  I dare you to sue me!! Please do in any court.. here in the US or at home and I'll come on my own.. .. ukitaka kujua ni nani wa kumsuu.. give me your number I'll call you and give you all my information to assist you. You have to be one of the named siyo wapambe wao!
   
 2. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #2
  Apr 30, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Malizia na huyo wa kumi kabisa mkuu!!
   
 3. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #3
  Apr 30, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  10. Jk
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Apr 30, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  10. Sophia Simba
   
 5. MwanaHabari

  MwanaHabari JF-Expert Member

  #5
  Apr 30, 2009
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lowassa
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Apr 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  TANGANYIKA KUIFISADI ZANZIBAR --------- Kuna kundi la Wananchi ambao uzalendo wao ulishawatoka siku nyingi na kwa muda mrefu wamebakia kufurahia mali za nchi yetu. Kundi hili linaendelea kutaka kutawala bila kuhojia au kupigiwa kelele. Wanataka wawe kama yule anayekula kisicho chake na hata ukitaka kupiga kelele anakunyoshea kidole na kukuambia 'shssssssss' Kwamba wewe muibiwa usipike kelele badala yake umuombe aache kula!
  Mkuki kwa Nguluwe kwa Binadamu Mchungu - By Mwalimu Nyerere
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Apr 30, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Duuh! Kule Italy kuna freemasonry group ambalo linaitwa Propoganda 2 likiongozwa na Licio Gelli. Hili kundi lilihusika na kashfa nyingi na za kutisha nchini Italy na kwingineko.Hatimaye ilipelekea Licio Gelli kupata kifungo cha ndani mpaka hii leo. Moja ya sifa kubwa ya kundi hili ni umahili wake wa kuajiri majaji, wakubwa wa polisi na jeshi na any influencial figure waliomuona potential kwa manufaa yao.
  Nilikuwa nahisi hatuoni jinsi Sir Andy Chande alivyoweza kama kiongozi wa freemason Eats Africa kuwatumia viongozi wengi wakubwa wa nchi hii kwa manufaa yao.Huyu ndiye anayewalea watu wengi wanaoongoza kwa vituko nchini kwetu na nakupa hongera MMKJ kwa kuwa wakwanza kusema hadharani kuwa naye ametuuza big time. Alikuwa msimamiaji wa Viwanda na amesaidia sana kuuzwa kwa viwanda vingi vikaishia kuwa magodown ya wahindi TZ.
   
 8. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #8
  Apr 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Asante sana M.M.K kwa kuwa mkweli wa nafsi yako na Mtanzania mzalendo mwenye uchungu na mali za taifa hili. nakupongeza kwani kuna wengine hapa wapo peke yao lakini hata kuwaongelea hawa watu kuwa ni mafisadi wanaogopa utadhani ni Miungu yao vile au kwamba wao ndio wanaowaweka mijini kumbe ndio wanaowafilisi.

  i can add sum
  11. Daud Balali (marehemu hewa)
  12. Mgonja
  na wengineo wengi wafilisi na wabakaji wa Nchi yetu.

  nadhani hatutakiwi kukata tamaa kwani itafikia wakati watashindwa kufungua kesi za watu wanaosema ukweli kwa kuwataja kuwa wao ni mafisadi na wafilisi wa hii nchi, kwa kuwa huo ndio ukweli. Tungelikuwa na mahakama zenye kufuata sheria kama wenzetu, tungelianza kupata matumaini ya kuwafunga hawa watu katika hali iliyofikia hivi sasa.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  May 1, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Natumaini kuna gazeti litakubali kuchapa ninachoandika; hawa watu wachache hawawezi kamwe kuishikilia nchi yetu kama rehani! Ikibidi twende kwenye uchaguzi mwaka huu na twende lakini hatuwezi kuwaachia nchi hawa.
   
 10. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2009
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mbona umewaacha Edward Ngoyai Lowassa,Yusuph Makamba,Karamagi,Idris Rashid,Mramba,Yona,Mgonja na Frederick Sumaye?Anyway,I can understand,orodha ni ndefu sana ila naafikiana na hao uliowataja BILA KUSAHAU ANAYEWALEA NA KUWAPA JEURI
   
 11. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  JK nae pia yumo mimi naombea sana atokeee bingwa wa mutharika wa TZ ili awakomeshe woote hawa....hata kama baada ya miaka10 ijayo wote peleka mahakamani....
   
 12. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Ndahani kaandika vizuru sana kuhusu nguvu ya Licio Gelli hadi kuwaweka majaji na wakuu wa polisi ili kulinda maslahi ya genge lao. That's exactly what is happening in Tanzania. Ule waraka wa Rweyemamu kwa Rostam ni ushahidi tosha kuwa alipelekwa ikulu na hawa mafisadi. Nashawishika kuamini kuwa hata Mujuluza wa IMMMA ujaji wake ulipitia mkondo uleule!
   
 13. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Yes Mwnakijiji, this one tells every thing
   
 14. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2009
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180

  Siku mbili hizi mkuu naona unahasira sana kunaniii?
   
 15. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Safi sana Mkuu,

  Hii ni hatua nzuri sana na kuonesha ujasiri mkubwa sana. You can be asured of my support!
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Labda tunapaswa kuangalia nyuma ya majina... mfumo
   
 17. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Na tumeshaona ... wako very alergic na kutangazwa. They have no strength and any power of their own. Ukiwapasukia Live!!! Wanahaha Huamini ni wao. Nguvu na utulivu wao wa kutukuka ni Zawadi ya Ukimya wetu!

  So ?

  Jambo la kujifunza ni Moja.

  Si kuwatangaza tu!

  Bali?

  Ni kuwatangaza Kwa Namna ambayo hawakuwa wameitgemea hata kidogo. Alafu Ukae mbali uwaone wanavyo peperuka kama kuku aliyekatwa shingo na kuachiliwa.

  Very easy ...Hawana Nguvu kama tunavyowaona wakiwa hawajaguswa kwa namna Nzuri na priemtive!!

  Hakika ni Moja: Siku zao si nyingi na wao wameanza kuyaona haya!!
   
 18. M

  Mugo"The Great" JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2009
  Joined: Oct 7, 2007
  Messages: 263
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ujasiri huu ndio utakao-ikomboa Tanzania. Manake sioni kwanini tuendelee kuwa maskini katika nchi yenye utajiri wa asili. Ndiyo maana Bob Marley katika wimbo mmoja Rat race alisema " In the abundance of water, The fool is thirsty". Mapambano kama haya ndiyo yatatufanya tusiendelee kulalamika kuwa tuna "KIU" wakati maji yapo tele.
   
 19. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #19
  May 1, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Kama mahakama ziko corrupt, and on the side of the corrupt, suing the corrupt would be to entertain corruption itself!

  Dawa yao hawa watu ni kuichukua nchi kwa njia ya demokrasia. Even the so-called opposition is corrupt... CHADEMA, NCCR-MAGEUZI, TLP, UDP, DP, CUF, hawa wote ni CCM-B, C, D, E na F!

  Tunahitaji chama kipya, chenye fikra mpya na mbadala. Nchi ni yetu, nia tunayo, nguvu tunayo, uwezo tunao. Shime, tuunde chama kipya, tukaikomboe nchi yetu. La sivyo tusitegemee hawa watutetee.... akina Dr. Slaa ni wachache sana... peke yao hawawezi, sisi tuko huku, ukweli tunaujua, lakini tunaikalia politiki! Haitasaidia!

  Action now, talk is cheap! Tutakuja kulaaniwa na wajukuu wetu!
   
 20. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  CUF haina uswahiba na Sultani CCM ,wenye uswahiba ni wale waliogaiwa kiti cha ubunge huko Tanganyika katika uchaguzi wa 2005 kwa matokeo yaliopangwa na tume ya kushuhulikia na kupanga matokeo ya Uchaguzi ya Sultan CCM.
   
Loading...