Mpaka sasa Matokeo Ubaoni Vita ya Iran Vs Israel

Mpaka sasa Matokeo Ubaoni Vita ya Iran Vs Israel

Ile nguruwe ya USA imeufyata 😆😆
Kwa hali ya sasa ya vita kati ya Iran na Israel (na pia kuhusisha Marekani), ukweli ni huu:

1. Iran ndiyo imeathirika zaidi (kwa kiwango kikubwa)
Vifo na majeruhi ni wengi zaidi Iran
Miundombinu muhimu (kama mafuta, gesi, na kijeshi) imeharibiwa vibaya

Uchumi umeanguka:
Sarafu kushuka
Ajira kupotea
Vikwazo (sanctions) kuongezeka

Kwa kifupi: wananchi wa kawaida wa Iran ndiyo wanaoumia zaidi (kiuchumi + kibinadamu).

2. Israel imeathirika, lakini si kwa kiwango kikubwa kama Iran
Kuna mashambulizi ya makombora na baadhi ya vifo

Majeruhi na baadhi ya majengo yameharibiwa
Lakini:

Ina ulinzi mkali wa missile defense (Iron Dome n.k.)
Uchumi bado uko stable ukilinganisha na Iran

Hivyo imepata madhara, lakini imejilinda vizuri zaidi

3. Nchi nyingine (Middle East + dunia)
Hizi pia zinaathirika bila kupigana moja kwa moja:
Nchi za Ghuba (UAE, Kuwait n.k.) zimepigwa pia au kuathirika na vita
Bei ya mafuta imepanda duniani → inaathiri uchumi
Biashara na safari zimevurugika l

Hitimisho (jibu la moja kwa moja)

Aliyeathirika zaidi kwa sasa ni Iran, hasa:
Wananchi wake
Uchumi wake
Miundombinu yake

Israel imepata madhara, lakini si kwa kiwango sawa.

Dunia nzima pia inaathirika kidogo kupitia bei ya mafuta na uchumi.
Jibu hili hapa 👇 👇

View: https://www.instagram.com/reel/DXmsoWQjFbT/?igsh=MXUxdW12MTBzc2Q1ZQ==
 
All in all Watanzania wa kawaida tumeathirika zaidi ya Iran. Petroli, dizeli, nauli hadi viberiti vimepanda bei. Dada poa nao wamepandisha dau bila shaka ikizingatiwa nauli za bajaji na uber zimepanda.
 
Hii vita Ina milengo miwili
1~ kuwavuruga waarabu ktk sekta ya mafuta
2~ kutafuta superpower wa Mashariki ya Kati kwa kuipunguza nguvu Iran
3~USA kutaka kumyonga kiuchumi MCHINA kupitia mafuta.
4 - kuharibu nguvu ya kivita hasa kinyuklia ya Iran.
Lipi alilofanikiwà Huyo Muamerika na mwenzake Israel?
 
Lengo la kwanza la marekani na israel ilikuwa kuangusha utawala wa serekali ya kiislam ya Iran. Ndio maana siku ya kwanza ya mashambulizi wakamuua Ayatollah Khamenei na viongozi wengine wa juu wakifiki ndio watakuwa wamerahisisha kuiangusha serekali. Kumbe kuna utaratibu kabambe wa kurithishana uongozi.
Mojtaba Kwa sasa ndio kiongozi mkuu wa iran. (USA naIsrael hapa wamefeli vibaya)
Lengo la pili ni Iran iache kabisa na huu mpango wake wa kurutubisha nyuklia. Na kwa hali ilivyo kwa sasa Iran haitakubali kuacha huu mpango na itaendelea kurutubisha urenium. (Hapa nako USA na Israel wanaenda kufeli)
Marekani ambayo ilikuwa na kambi za kijeshi karibia nchi zote zilizoshambuliwa na Iran, Kuwait, Qatar, Saudia Arabia, Oman, nk ameshindwa kuwahakikishia usalama hizo nchi kwa kushindwa kuzilinda. (Hapa nako kafeli)
Israel kwa kumewaka moto. Hawakuzoea maisha ya kukaa mapangoni kama nguchiro. Japa taarifa zinafichwa lakini nao wameonja joto ya jiwe. (Iran hapa kafanikiwa. THAA na Iron Dome zimeshindwa kuwahakikishia ulinzi wananchi wa israel.
Kiuchumi. Tunapigika wote.
 
Mnashabikia vita kama michezo very senseless!
 
Yap hapa kidogo umeongea uhalisia, lakini china haathiriki moja Kwa moja, Bado yeye na Iran Wana Mbinu chafu na za Siri za kusafirishiana mafuta,pesa na baadhi teknolojia kutumia Bahari ya kaskazini mwa Iran,Caspian sea via Urusi,Uzebkistan,Azbeijan na kdgo Pakistani...
Lakini pamoja na hayo Ww kweli chizi maarifa, unaisema Iran wameshindwa vita, vipi wewe Mtanzania na Samia wenu mmeishinda vipi? Bei mafuta petroli,diesel,na ya kula ipoje saivi, vipi na baadhi za bidhaa na vyakula??
 
Back
Top Bottom