Sijawahi kuona Engineers wakiajiliwa wote katika nchi hii na hawalalamiki, walishajifunza kujiajiri na kutafuta ajira maeneo mbalimbali ya nchi na nje, kelele nyingi ni za walimu wanaomaliza makundi kwa makundi wakiwa wameahidiwa ajira za moja kwa moja, wengi wanamaliza hata na GPA mbovu kwani wanajua hakuna ushindani wao ni ku click button tu tayari wapo halimashauri , ubunifu wao mkubwa ni kutengeneza mazingira ya kubaki mjini na maeneo wanayoyapenda. Serikali inabeba lawama hizi kwani haikuwaanda vijana wengi kujiajiri na hata mazingira yenyewe sio rafiki kujiajiri.