Mpaka sasa hakuna fani ya Kuajiliwa moja kwa moja Serikalini

Good People

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
945
1,817
Imefika kipindi graduates tuwe wabunifu kwa sababu hadi sasa hakuna fani ya kuajiliwa moja kwa moja Vijana wengi walikua wamekimbilia Ualimu lakini nako kumeshajaa

Madaktari walikua wanaajiriwa moja kwa moja lakini Ummy Mwalimu nilimsikia akisema wanaomaliza ni zaidi ya 1,000 na uwezo wa Serikali kuajili ni madaktari 400 tuu kwa mwaka hapo kuna madaktari zaidi ya 600 watakua hawana ajira.
 
Sasa mkuu weka porojo pembeni, tujadiliane sasa huo ubunifu, tupe na mbinu zako ambazo wewe unatumia.
 
enzi za jk walimu madaktari na wengineo walio kada ya afya walikula shavu bila matatizo
 
enzi za jk walimu madaktari na wengineo walio kada ya afya walikula shavu bila matatizo
Enzi ya mwalimu kulikuwa na scarcity ya madaktari sababu graduates walikuwa wachache

Saizi kila mwaka mamia ya watu wana graduate ,ratio ni kubwa kuliko nafasi zilizopo
 
Enzi ya mwalimu kulikuwa na scarcity ya madaktari sababu graduates walikuwa wachache

Saizi kila mwaka mamia ya watu wana graduate ,ratio ni kubwa kuliko nafasi zilizopo
sasa si waajiri basi hizo zilizopo shida iko wapi?
 
Sijawahi kuona Engineers wakiajiliwa wote katika nchi hii na hawalalamiki, walishajifunza kujiajiri na kutafuta ajira maeneo mbalimbali ya nchi na nje, kelele nyingi ni za walimu wanaomaliza makundi kwa makundi wakiwa wameahidiwa ajira za moja kwa moja, wengi wanamaliza hata na GPA mbovu kwani wanajua hakuna ushindani wao ni ku click button tu tayari wapo halimashauri , ubunifu wao mkubwa ni kutengeneza mazingira ya kubaki mjini na maeneo wanayoyapenda. Serikali inabeba lawama hizi kwani haikuwaanda vijana wengi kujiajiri na hata mazingira yenyewe sio rafiki kujiajiri.
 
Imefika kipindi graduates tuwe wabunifu kwa sababu hadi sasa hakuna fani ya kuajiliwa moja kwa moja Vijana wengi walikua wamekimbilia Ualimu lakini nako kumeshajaa

Madaktari walikua wanaajiriwa moja kwa moja lakini Ummy Mwalimu nilimsikia akisema wanaomaliza ni zaidi ya 1,000 na uwezo wa Serikali kuajili ni madaktari 400 tuu kwa mwaka hapo kuna madaktari zaidi ya 600 watakua hawana ajira.

= kuajiriwa
= kuajiri

Wewe ukinikuta mimi nnaajiri basi ujuwe hutoipata hiyo ajira.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom