Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,059
- 79,412
Hamjambo wote!
1. Kwenye mambo ya Intelligence(ujasusi, ushushushu, unjangu) kuna kitu inaitwa Missing System/s.
2. Kitu hii ukikosa hata MTU binafsi mambo yako yanakuwa hatarini, usalama wako unakuwa mashakani.
3. Missing System ni uwepo wa ombwe la kimkakati, mfumo muhimu ambao unapaswa kuwepo ili kudhibiti, kutabiri, na kulinda nguvu za mamlaka, lakini mfumo huo haupo au haufanyi kazi.
4. Ni pale ambapo taasisi au chama kinaonekana kuwa na muundo kamili wa juu juu, lakini hakina mifumo ya ndani ya kusoma hatari, kupanga mustakabali, na kudhibiti mabadiliko ya mazingira ya kisiasa.
5. Kwa lugha ya kijasusi, Missing Systems ni akili ya mfumo iliyopotea, ndiyo maana nguvu huporomoka Siku hadi Siku.
6. Matumizi na utegemezi wa vyombo vya Dola katika siasa ni dalili nyingine inayoashiria kabisa kuwa kuna Ombwe la kimfumo, mkakati, mipango, mbinu ambalo CCM wanalo.
7. Ni kiashiria kwamba CCM imebakiwa na risasi ya mwisho.
8. Katika siasa za kidemokrasia, kulitegemea jeshi la polisi na vyombo vya Dola ni kuliingiza jeshi kwenye siasa. Ni kusema jeshi linafanya siasa.
9. Mtibeli najaribu kueleza kuwa, kisaikolojia, kitu unachokitegemea ndicho kinachokuongoza na kukutawala.
10. Kisiasa, Unapotegemea jeshi na vyombo vingine vya Dola, wewe inageuka kivuli tuu. Vyombo vya dola ndio vinakuwa vinatawala.
11. Kwamba CCM kama itategemea vyombo vya Dola tafsiri yake CCM sio chama tawala tena, isipokuwa Jeshi ndio linatawala.
12. Kwa sababu huwezi sema CCM inatawala wakati ikiletewa vyama vingine ili ipambane navyo inaanza kulialia na kupigia magoti jeshi ili lisapoti chama(CCM). Kwamba bila Jeshi CCM haiwezi kufutukuta. Na hapo ndipo Missing system katika chama inajitokeza waziwazi.
13. Jeshi sio chama cha siasa. Ukishaliingiza Jeshi au vyombo vya usalama lazima utaona viashiria vya kimabavu na uonevu kwa raia ukijitokeza. Na hapa nazungumzia raia waliopo kwenye vyama vya siasa vya upinzani, au hata waliopo CCM lakini wakaonekana mwiba ndani ya Chama.
14. Missing system iliyopo CCM iliyopelekea kulitegemea jeshi tija yake ni ipi? Je ni tija endelevu?
15. Iko hivi mahali popote unaposikia Uasi, mapinduzi, machafuko na taifa kugawanyika lazima uelewe kuna namna Jeshi liliingilia au kuingizwa kwenye Siasa.
16. Ukishaliingiza Jeshi kwenye siasa basi tegemea Uasi, mapinduzi, machafuko na mambo ya Aina hiyo.
17. Jeshi linafanya kazi kwa mujibu wa Sheria, na msingi wake Mkuu ni NIDHAMU. Lakini NIDHAMU inamipaka yake.
18. Jeshi litakuwa na nidhamu kama halitaingizwa katika mambo ya Siasa. Kutumika kama ngao ya chama Fulani.
Kutumika kama ngao ya chama Fulani hiyo haiwezi kuwa nidhamu tena. Itakuwa siasa, itakuwa ni maslahi.
19. Jeshi likiendeshwa kwa maslahi na sio nidhamu kazi inakuwa imekwisha. Hakuna jeshi hapo. Ule Wito WA kizalendo wa kutumikia taifa na wananchi utakuwa umekufa kifo cha asili.
Na hapo ndipo vurugu zinapoanzia.
20. Wanajeshi na Askari sio roboti au midoli ya AI(Artificial intelligence) kwamba wenyewe hawana akili za kufikiri. Nidhamu ni kwaajili ya taifa na nchi. Si kwaajili ya mambo ya kisiasa(maslahi) ya kikundi au chama Fulani.
21. CCM kama hawataziona gap na kuziziba. Wakiacha missing systems hizo ziendelee kuwepo. Sioni namna ya wao kuendelea kushika madaraka.
22. Kitu kimoja niweke wazi ambacho kitasaidia pande zote. Kadiri nguvu nyingi zinavyotumika ndivyo hata Yale mafanikio yaliyopo yanaharibiwa.
23. Unapomuona Gaddafi na watoto wake inaweza kuwa mfano mzuri katika kuyaendea mambo ya kisiasa na kushughulika na kuwaongoza watu.
24. Jeshi ni muhimu lakini watu ni muhimu zaidi. Kwa sababu jeshi hutoka kwa Watu.
25. Kwenye ujasusi kuna kitu kinaitwa Correction. Ambapo serikali au taasisi za kiusalama hutumia mbinu hiyo kufanya marekebisho na kufuta makosa unnotice na watu wa kawaida ili kurejesha Imani ya watu kwa serikali au chama Fulani.
26. Lengo la Correction ni kuondoa missing system, lakini pia kulinda maslahi ya taifa na future ya viongozi baada ya kustaafu.
27. CCM lazima iwe na mpango kabambe kwamba watawezaje kusimama bila kutegemea Vyombo vya Dola. Na sio kujivunia kwamba wao Wana dola. Hiyo ni dalili ya upungufu wa maarifa na kuhatarisha usalama wa chama na taifa kea ujumla.
28. Kitu kimoja cha uhakika. Huwezi tegemea jeshi Siku au miaka yote kama nyenzo ya kupata madaraka na kutawala.
29. Kiintelejensia kadiri unavyotegemea Jeshi ndivyo unavyokuwa hatarini, na unakuwa na mashaka zaidi.
Sababu kuu ni kuwa jeshi nidhamu yake hukoma pale linapoingiza maslahi mbele(siasa).
30. Na nidhamu ikikoma, basi mambo yanakuwa hayatabiriki, na kiusalama kutotabirika yafsiri yake hakuna usalama.
Mimi nimemaliza. Acha Nile makande.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam