Mpaka leo sijaijua thamani ya 'X'

Hahaa, tunatajirika tukiendesha magari mtumba toka Japan, nguo toka China, tukiumwa tunaenda India kutibiwa...!
 
Hayo mahesabu yanatumika kila siku katika maisha ila sema ni katika unconscious way pasipo kuelewa ni kama Yale ya darasani hii ni kwa sababu mahesabu yale ya darasani walifanya kuya modernize na kuyafanya yaonekane magumu yaani wameyafanya katika indirect way kiasi kwamba inapelekea mtu kushindwa kuyafananisha na yale anayotumia katika maisha halisi na kuona haya ya darasani ni magumu, hawakupoint moja kwa moja kama jinsi Leo tunavyoyatumia katika maisha huenda tungeyaelewa zaidi kwani ukweli mahesabu yanasaidia yanaongeza Uwezo wa kufikiri kufikiri kwa logic na pia yanasaidia kuwa nampangilio na faida nyingine kibao tu.
 
Niliwah kuwa na mawazo kama yako ndugu na niliipuuza sana Hesabu, ila nilivyoingia chuo nikakutana na TAX na QM lazima usome, na faida zake unaziona nje nje. Ikiwa ulitaka kuikimbia na ukafanikiwa bas ishi na upumbavu wako, usiambukize wanao tu kwani dunia tuliyonayo leo hii matajiri ni wasomi. Kaa hapo ukariri
 
Kwani thamani ya "x" ulikuwa ukiipata hivihivi kwa kuiangalia au ulifanya maneuvre kuitafuta. Bro acha kuota, tafuta njia ya kuipata thamani ya x. Cross multiply , gawa, zidisha, jumlisha, toa... utapata thamani ya "x".
Endelea kuingalia tu x ama utafeli mtihani.
 
Hahaa, tunatajirika tukiendesha magari mtumba toka Japan, nguo toka China, tukiumwa tunaenda India kutibiwa...!
Asante Himawari. Mdau anataka kila msomi atajirike na kama hajatajirika basi siyo msomi na elimu yake haijamsaidia. Kwa fikra kama hizi tutaendesha magari mtumba ya Japan, nguo toka China na kila siku matajiri wetu (...wasomi) watakuwa wanafia India na kuletwa katika masanduku milele. Wangekuwa wanautumia utajiri wao kwa faida ya jamii kama wanavyofanya akina Bill Gates, Warren Buffet, Zuckerberg na mabilionea wengine wa dunia angalau ningesema wasomi wetu wamefanikiwa. Mafanikio haya ya kujirundikia mali mwisho unafia India unaacha mabilioni yako yakiwa yamezagaa kwenye mabenki yakigawanwa na watoto wako wa kubambikiwa yana faida gani kwa jamii hii masikini? Hili ndilo lengo kuu la elimu? Ubinafsi wa kutisha na hiki ndicho kitambulisho cha mtu mweusi popote alipo hapa duniani. Halafu akina Trump wakitutukana kuwa weusi tuna matatizo hata katika mfumo wetu wa kufikiri tunaanza kulalamika na kuwaita wabaguzi. I say we deserve it!
 
Mathematics inasaidia kwenye kuongeza thinking capacity... hauwezi kuona tofauti until u know nothing.
 
Daa nimeipenda mada, kiuhalisia mtoa mada kachokoza watu kujitambua. Kiuhalisia hesabu zote zinamaana katika maisha. Zinakupa uwezo wa kukabiliana na changamoto, mfano wa logarithim unapewa kitabu four-figure kutoa majibu, utumiaji wa kitabu hicho na kufikia jibu inakupa uwezo wa kukabiliana na jambo na kufikia hitimisho kusudiwa.
Kuhusu thamani ya "X" haina jibu moja ila kila mtu anatafuta thamani ya "X" yake, hapa pia haijalishi umesoma au hujasoma ila jinsi unavyoyakabili mazingira yako ndio utaweza fanikisha thamani ya X yako.
Kuhusu kutajirika au la ni namna wewe binafsi unavyojituma na kujitoa mhanga "risk" kwa kile unachofanya, kwa aliyesoma huenda kwa tahadhari sana kwa project aliyoplan japo wakati mwingine huweka woga sana kwa huyu msomi na kukata tamaa, tofauti na asiyesoma huenda tuu mbele kwa mbele akikosa poa akifanikiwa pia kwake poa sana.

Pesa haiepukiki kufikia mafanikio whether ya kitaaluma au ya kijamii, nabaya zaidi mfumo wa elimu yetu hautoi mtu kujitafutia maarifa zaidi ya kuwa wa kutafutiwa maarifa, pili serikali zetu haziwapi nafasi ya kutosha wataalam wetu kuonesha ujizi walionao. Mifano ni mtaalam wa tiba ya Meno au Upasuaji unakuta kapewa wizara ya ulinzi au habari. So kiujumla wewe binafsi una X yako itafute .
 
Yaelekea we ngwini,ungekula vitu vya maana kama economics au engineering usingesema hujawah kuona applications za quadratic equation au logarithm.
For your info, nimesoma E.C.E
 
Ushahidi unagoma,... wasomi bado ni waajiriwa, mostly wa serikali.Entrepreneurs ndo matajiri, ambao mostly wako deep kwenye "knowledge" ambazo zinawasaidia ktk kazi zao moja kwa moja.Hawana mambo mengi kichwani.

Wasomi ndo wanaongoza kwa kuua makampuni, kufilisi mashirika n.k which makes me question the relevance of their education.

Nchi hii tuna wasomi kibao, bado wanahangaika mtaani na vyeti.. maskini wamekosa ajira ambazo ndizo walizoandaliwa ku-cover; hawakuandaliwa kujiajiri... wengine wamekimbilia siasa na kuacha profession zao, huko ndo wameenda kuwa matajiri.

Bado unanishawishi niamini elimu yetu iko sawa?? No, thank you.
 
Ofcourse nmesema sijaipata, which means naendelea kuitafuta.Siku nikiipata uwe na uhakika nitawasaidia wengi ambao pia bado wanaitafuta.

*X = Mafanikio.
 
Huna pesa huthaminiwi, hata usipokuwepo vikao vya familia vinaendelea... sasa pata pesa uone, hawafanyi kikao mpaka "mukubwa" ufike.

Look around you, kama huna kitu ukipata rafiki umefanikiwa kichizi.
Nimependa line 2 za mwisho umeweka na msingi wa Fid Q.
 
No Trump is selfish himself.

Wapo akina Mengi, Bakhresa, Ghalib Sallah & Mohammed (GSM) kwa mfano... wanatumia utajiri wao kusaidia jamii.Hawa ni matajiri ambao nisingependa kuwaweka katika kundi la wa wasomi, bali ni successful entrepreneurs.

Sasa... ukiona wasomi matajiri wa kitanzania wanashindwa kufanya kama hawa entrepreneurs, basi kubaliana na mimi kuwa MFUMO wetu wa elimu unahitaji mageuzi makubwa au la sivyo, Yesu arudi haraka iwezekanavyo kutusaidia.

Manaake ni kuwa, mfumo wetu unazalisha wasomi wasioweza kujitegemea pasipo kuajiriwa, na hata wakifanikiwa wanakuwa selfish!!

Sasa hapo ndo utasema algebra imewasaidia??? Thamani ya X waliyojifunza kutafuta, iko wapi???Am talking about the bigger picture here... dude!!
 
Mathematics inasaidia kwenye kuongeza thinking capacity... hauwezi kuona tofauti until u know nothing.
True, math's inaongeza thinking capacity. Wasi wasi wangu ni kuwa we're overloading.

Kichwa kimoja cha O-level kinasoma KISWAHILI, ENGLISH, BIOLOGY, CHEMISTRY, PHYSICS, MATH'S, CIVICS,GEOGRAPHY,HISTORY, COMMERCE... Halafu tunatarajia mtu huyu aje kuwa mvumbuzi kama Mark Zuckerberg????

Kwasabu kwa lundo la masomo hivyo manaake 99% wanakariri au wanasoma kwaajili ya mtihani na sio kwaajili ya kupata UJUZI.

Mwisho wa siku tuna wasomi ambao kwenye practical hamna kitu.Wana vyeti ila ukiwapa kazi wanachemsha...

Hence wasomi wamebaki kuwa watu wa kusubiri kuajiriwa.Na ukiajiriwa, kupata thamani ya X ni ngumu.... maanake ni kuwa neno "mafanikio" utakuwa unalisoma kwenye dictionary na kwenye magazeti.
 
Hatimaye nimepata kichwa tunachofikiri sawa.Siongezi wala kupunguza chochote mkuu.

Thank you!!!
 
Yale yote yalikuwa yanaongeza uwezo wa ubongo kufikiria kwa haraka. Ni problem solving skill muhimu katika maisha. Huwezi ona moja kwa moja lakini ubongo wako umepata uwezo wa kufikiria kwa kina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…