Moyo wangu una majonzi, yako wapi mapenzi ya dhati?

Moyo wangu una majonzi, yako wapi mapenzi ya dhati?

Ndu zangu wana jamvi....

Naomba nieleweke hivi, nimechoka, sijui tatizo langu ni kwamba napenda sana bila kiasi, nimepitia kwenye mahusiano kama matatu sasa toka nijue mapenzi ni nini, mwanamke wa kwanza aliniumiza sanaa, nililia mwanaume machozi ya kila aina, sikuwa tayari aniache, nilikuwa naona kam maisha yangu yatakuwa magumu sana nikiachana na huyo dada.
Niliteseka kwa zaidi ya mwaka mmoja nambembeleza turudiane, alinitesa mno, siwezi kuelezea. Siku moja nilijifungia chumbani kwangu saa 11 jioni hadi kesho yake, nilifunga simu, nikapiga magoti, nilisali sana, nilimlilia Mungu moyo wangu upate amani, nikamshi Mungu kama sio mapenzi yake amuweke mbali na mimi yule binti, kweli siku ya pili nilikuwa mwepesiii, sikuwa hata na hamu ya kumtafuta, nilimshukuru sana Mungu maisha yangu yanaanza kubadilika mwishowe nikafuta mpaka namba zake japo hata leo ninazo kichwani....

Nikaanza mahusiano mengine, nikaona picha ni zile zile, nilikimbia mapema nilivoona tabia za mwanamke wangu wa kwanza zimeanza kujirudia kwa mwanamke huyo wa pili....nikamuomba Mungu nisiingie tena kwenye mahusiano kama vinginevyo iwe ni mwanamke wangu alieniandalia, nilikaa kwa karibu mwaka mmoja na nusu bila kuwa na mahusiano ya serious......

Mwaka huu mwezi wa Tano nilikutana na Binti mmoja mrembo kweli, ni mzuri kuanzia kutembea kwake, kuongea kwake, anapenda sana kanisa, kila Jumapili yuko kanisani ibada ya kwanza. Binti huyu kwa mara ya kwanza alikuja kwenye eneo langu la kazi, alikuja kumtembelea rafiki yake ambae pia staff mwenzangu, nilivyomuona kiukweli nilimpenda, nikajaribu kumuuliza yule rafiki yake, akanipa briefing kidgo kuhusu huyo binti, nilimuomba appointment ya kutoka nao wote wawili ili atleast nipate picha halisi na kujuana nae kidogo. Kwenye hiyo out tulibadilishana mawazo kidogo, tukabadilishana na mawasiliano pia, nikaanza kujenga nae urafiki, tukafahamiana vizuri then nikaona ni mtu ambae yuko smart kweli, siku moja nikamuomba appointment ya kutoka nae somewhere for lunch, hakukataa alikuja then tukaongea sana then nikamruhusu aende nyumbani mapema ili awahi mapishi ya jioni. Yote tisa, kumi huyo binti nilianza nae mahusiano baada ya kila mmoja kumfaham mwenzake,,,,ni takriban miezi 5 sasa toka tumeanza mahusiano rasmi, professionaly yeye ni mwalimu, mimi ni Muhasibu, tumekuwa tukiwasiliana vizuri sana, kinachonipa wakati mgumu kwake ni majibu yake, mara nyingi nikichat nae huwa ana majibu mkato sana (shortcuts), unaweza ukawa unamuuliza kitu sensitive yeye akakujibu majibu ambayo like she dont care. Kingine huyu binti amekuwa mgumu sana kushare nae muda, kama mpenzi wangu muda mwingine naweza muomba lunch tule sehem moja lakini akakataa bila sababu, nikimuliza sababu nini atakujibu niko busy ... hii statement ya niko busy imekuwa ikini disappoint sana, ukimuuliza busy na nini atakujibu sorry niko busy. Guys nisaidieni mtu kama huyu kweli bado anaweza kuwa na mapenzi ya dhati kwako? Katika chatting yake mara nyingi tumevutana sana, huwa ni mtu mwenye majibu ambayo yanaonyesha hajali kabisaa,,,

Tukiachana na hayo yote , wiki iliyopita wakati napiga nae story kwenye simu alichomekea agenda yake kuwa anataka kurudi chuo kwa miaka 3 kuanzia mwaka ujao kwa hiyo nikimhitaji maswala ya ndoa nisubiri mwaka 2020. Hili jambo limenikatisha sana tamaa guys, yaani nikae mtaani nimsubiri yeye anaenda chuo kwa miaka minne kuanzia sasa....moyo wangu uliumia sana kiukweli, bado naendelea kuumia, muda mwingine nawaza na kumwambia Mungu kwanini unanipitisha kwenye majaribu magumu kiasi hiki? Kweli ni binti niliempenda sana ila yeye kutokuwa na care inanikatisha tamaa, majibu yake mara nyingi ni " Poa, sawa, K, P n.k.
Guys wenye experience naombeni ushari, naumia kweli maana tayari nilishaingia kwake miguu yote, dalili ya kuumia tena naiona.

Sio dhihaka , sio utani napitia kwenye wakati mgumu, ambao tayari mko kwenye ndoa naomba mtusaidie mlipitia katika wakati kama huu?
Muda mwingine huwa namwambia Mungu mapenzi ya kweli yale ya wazazi wetu yako wapi? Kiukweli vijana wa kiume tunapitia wakati mgumu sana pindi unapomtafuta binti wa kuwa nae kimaisha.

Naamin sipo mwenyewe, tusaidiane kwa ushauri na kufarijiana.
dawa 3.
1. tafuta pesa
2. tafuta pesa
3. tafuta pesa
 
Acha "Babe I love You" kwa saana.
Kila wakati au daily unataka uonane na demu wako. Huyo ameshagundua utakuwa unamganda sana na wivu mkali, hapo sasa demu anajikataa zake.
Kuna mdada hapo juu kakuambia love yourself hajakosea fuata ushauri wake.
 
Ukpend kwel utakufa kila ck mkuu we kama manta kazngua piga kmya ck ikpt ajaktaft poah wk ikpt mwez ukapt mahuxian yameish mtot wa kiume unachezew akil na mtot wa kike eb bdlika mkuu acha kulia
 
Acha "Babe I love You" kwa saana.
Kila wakati au daily unataka uonane na demu wako. Huyo ameshagundua utakuwa unamganda sana na wivu mkali, hapo sasa demu anajikataa zake.
Kuna mdada hapo juu kakuambia love yourself hajakosea fuata ushauri wake.
Sawa mkuu, kama nina hayo mapungufu nitarekebisha, but kumbuka sinaga time ya kumhitaji kila wakat maana huwa nakuwaga busy sana nikitaka kumeet nae kwa muda mchache tu, we sema najaribu kupambana kutenga muda mchache sana. Maana hadi weekend kazi yangu inanikeep busy
 
Ukiona demu anakujibu short sana akati ni ishu sensitive jua hapo umeliwaa...Majibu kama K..sijui P...!! Jua hapo hakuna kituu alafu pia na wew inaonekana upo busy sana so pale anapokuhitaji wew haupo na wew ukipata muda yeye anaigiza. Kuwa busy hata kama hayuko ili mradi na wew ufeel kile anafeel..!!

Mwanamke ukiona kakuganda na Anakupenda sio kwamba hajui unacheat ila jua kakupenda kwelii...
 
Pole sana mkuu ila huyo hakupendi anae mwingine anaempa majibu ya kubembeleza hadi mbingu zinatabasamu...kifupi achana nae kabla hujaanza kujifungia huku ukilia...!
 
Jamaniii mapenzi hayalazimishwi kama unaona haelekei kaa chonjo kwani ulizaliwa na MTU? Kuishi tunaishi Mara moja sasa wewe lialia ufe wenzio waendelee kufaidi mema ya nchi,.tulia,omba kwa bidii mkuu mkwe mwema anatoka kwa BWANA na hakuna awezaye kumuona isipokuwa yeye pekee ukilia lia na sisi ma baby gelo tufanyaje!??
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom