Moyo wangu umekufa ganzi naomeni Msaada

Moyo wangu umekufa ganzi naomeni Msaada

Kinachokuumiza zaidi ni nini??
unaona aibu kua na mama muathirika au unaona utapata jukumu la kumtunza kwa sana au hasa wewe kipi kinakusononesha??

Nimejudge kulingana na TONE yako uliyoitumia katika bandiko lako.
 
Hapana naumia kwa nini haya yameetokea?
 
Sina mengi ua kusema ila miezi 7 iliyopita nilipgiwa simu na mama yangu mzazi akiniambia maneno mazito na magumu sana nimeyabeba lakini naona yananishinda nawaza saana , naumia sana maneno yenyewe ndo haya"MWANANGU MIMI MAMA YAKO NIMEENDA KUPIMA NIKAAMBIWA NIMEATHIRIKA NINA UKIMWI KWA SASA NIMEANZA DOZI"
Ipo hivi mama yangu alizaa na baba yangu baadae wakaachana baba akanichkua nikwa nalelewa na baba mpaka nikafikia utu uzima. mama yangu kule aliolewa akabahatika kupata watoto wawili ila mme wake alifariki kwa huo ugonjwa.
TRULY I GOT PAINFULLY
nashindwa kukubali Matokeo naombeni Ushauri wana Jf ili niweze kukubali kuwa ni kweli mama yangu ni Muathirika.
Kila siku tunafundisha namna ya kufanya tahajudi mnapita kama vile hamuoni hiyo post. Shauri yako! Fanya tahajudi tu utaona mambo yote kawaida!
 
Najuani ngumu boss. Ni ngumu sana kuukubsli ukweli haswa kwa swala kama hilo. Chamsingi kapime na ww uhakikishe kama unao au lah. Maana inaweza kuta hauna ila nduguzo ndio wanao
mimi sinaga mkuu
 
Sina mengi ua kusema ila miezi 7 iliyopita nilipgiwa simu na mama yangu mzazi akiniambia maneno mazito na magumu sana nimeyabeba lakini naona yananishinda nawaza saana , naumia sana maneno yenyewe ndo haya"MWANANGU MIMI MAMA YAKO NIMEENDA KUPIMA NIKAAMBIWA NIMEATHIRIKA NINA UKIMWI KWA SASA NIMEANZA DOZI"
Ipo hivi mama yangu alizaa na baba yangu baadae wakaachana baba akanichkua nikwa nalelewa na baba mpaka nikafikia utu uzima. mama yangu kule aliolewa akabahatika kupata watoto wawili ila mme wake alifariki kwa huo ugonjwa.
TRULY I GOT PAINFULLY
nashindwa kukubali Matokeo naombeni Ushauri wana Jf ili niweze kukubali kuwa ni kweli mama yangu ni Muathirika.

Inaelekea hukuwa na ukaribu na mama yako angehakuambiaga zamani sana. anyway siwezi jua sababu ila ni mapito tu. na kwa umri wa mama yako I hope anamlingana Muumba wake.
 
Hapana naumia kwa nini haya yameetokea?
Hupaswi kuumia, UKIMWI sio mwisho wa maisha ni Upungufu wa Kinga Mwilini ili arudishe na kuimarisha kinga zake basi anapaswa kula mlo kamili, afanye mazoezi sio mpk aende Gym kutembea kama km 2 na kurudi kila siku ni zoezi tosha, arelax asiwaze waze sababu kuwaza husababisha kinga ya mwili kushuka na magonjwa nyemelezi ndio hujitokeza, atengeneze unga wa lishe awe anatumia kila siku.

Ukiwa poa wewe na yeye atakua poa lakini kama ukianza kuwaza waza atajisikia unyonge anaweza hata kupoteza maisha kwa kujidhuru.
 
unaweza ukafa ukamuacha huyo mama yake akaishi miaka mingine 20 mbele baada ya wewe kudanja.
 
Kila jambo baya kama halijakupata utaliona la kawaida sana. Ila likikutokea huwa linakuwa zito zaidi kwa mhusika.

Nimejaribu kuvaa uhusika wako, kwa kauli uliyoipokea kutoka kwa mama mzazi, nimeishia kutokwa na chozi.

Mama anahitaji msaada wa dawa, chakula na zaidi ya yote anahitaji msaada wa Kiroho.
Cha msingi uwe karibu naye kwa mawasiliano.
 
Alichokosea ni kuanza kutumia dozi.alaf mbna inshu ndogo hiyo inakumaliza ganzi ya mwili..ukimwi sio kifo..ana mategemeo ya kuishi miaka zaidi ya kumi akijilinda na akibadilisha life style..tena wanawake ndo hawafagi kbsa kwa ukimwi..ondoa shaka kua nae karibu muondoe hofu.na hadi yeye kukubali kuanza dozi ni kwamba kakubaliana na hali.ukiwa down wewe utamkatisha tamaa mapema..ukiwa nae act kama ni kitu cha kawaida sana utaona mambo fresh kbsa..

Arv sio nzuri,chakula kizuri ni bora zaidi ya arv
 
Ki nina dada yangu alikwaa ngoma mwaka 2000 bado yupo fresh kabisa na anachapa dozi. Afterall mama kashakubaliana na hali hii inamoa nafasi yabkujipanga na kuishi maisha yake safi kabisa. Muhimu jitahidi kama unanafasi kumtumia tumia pesa kidogo ili asikose chakula. Zile dawa zinaraka msisi chief, Acha woga ndugu inaonekana kupata sio ticket ya kifo
 
Kila jambo baya kama halijakupata utaliona la kawaida sana. Ila likikutokea huwa linakuwa zito zaidi kwa mhusika.

Nimejaribu kuvaa uhusika wako, kwa kauli uliyoipokea kutoka kwa mama mzazi, nimeishia kutokwa na chozi.

Mama anahitaji msaada wa dawa, chakula na zaidi ya yote anahitaji msaada wa Kiroho.
Cha msingi uwe karibu naye kwa mawasiliano.
well said mkuu watu wanaona ni jambo la kawaida sana kumbe haipo hivo mkuu.
inaumaa
 
Wew siyo wa kwanza hata mimi pia hali km hiyo ilishanikuta miaka mingi iliyopita na mpaka sasa maisha yanaendelea ni lazima kukabiliana na hiyo hali baadae utakuwa sawa. Mwanzo mgumu ila mm nililaumu sana kwann aliniambia vile, mpk leo sijapata jibu. Jipe moyo ila mtie moyo kweny mambo yake sana.
 
Pole zidi kumtia moyo na kumwomyesha upendo na Mungu atakubariki wewe ndio tegemeo lake mpaka kakujulisha hivyo jipe moyo na omba Mungu akutoe huo uchungu na majonzi chukulia kama malaria tu
 
Kubali matokeo utakuwa sawa ila usipokubali matokeo utapata tabu sanaaaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom