Moyo wangu umekufa ganzi naomeni Msaada

Moyo wangu umekufa ganzi naomeni Msaada

Pole sana Mkuu!! Najaribu kuvaa viatu vyako hakina Inasikitisha na kuumiza sana
 
Pole sana Mkuu!! Najaribu kuvaa viatu vyako hakika Inasikitisha na kuumiza sana
 
Najuani ngumu boss. Ni ngumu sana kuukubsli ukweli haswa kwa swala kama hilo. Chamsingi kapime na ww uhakikishe kama unao au lah. Maana inaweza kuta hauna ila nduguzo ndio wanao
nashindwa kukubali mkuu nimejitahidi but nimeshindwa
 
Pole sana mkuu.
Hali ilivyo kwa sasa karibia kila familia kuna mgonjwa. Hilo ni janga la kitaifa.
 
Ukimwi ilikua miaka ya tisini kwa sasa mbona kawaida sana. Usiwaze kijana mama ataishi miaka mingi sana muhimu azingatie matumizi sahihi ya dawa na lishe ONLY that!
 
Sina mengi ua kusema ila miezi 7 iliyopita nilipgiwa simu na mama yangu mzazi akiniambia maneno mazito na magumu sana nimeyabeba lakini naona yananishinda nawaza saana , naumia sana maneno yenyewe ndo haya"MWANANGU MIMI MAMA YAKO NIMEENDA KUPIMA NIKAAMBIWA NIMEATHIRIKA NINA UKIMWI KWA SASA NIMEANZA DOZI"
Ipo hivi mama yangu alizaa na baba yangu baadae wakaachana baba akanichkua nikwa nalelewa na baba mpaka nikafikia utu uzima. mama yangu kule aliolewa akabahatika kupata watoto wawili ila mme wake alifariki kwa huo ugonjwa.
TRULY I GOT PAINFULLY
nashindwa kukubali Matokeo naombeni Ushauri wana Jf ili niweze kukubali kuwa ni kweli mama yangu ni Muathirika.
Hako ka kiingereza kako kamenifurahisha... "Truly I got painfully"

BTW mama yako sio wa kwanza na hatakuwa wa mwisho kuambukizwa. Mwambie afuate masharti na maelekezo ya matabibu. Atakufa uzeeni mwake au wewe utakufa umwache na nguvu zake.

Cha msingi hivi sasa jitahidi na uombe Mungu sana ili na wewe usipate maambukizi.
 
Akipata mlo sahihi,ukimuonyesha upendo na kumtia moyo ana uwezo wa kuishi hata miaka 100!
 
Mpende tu mama yako my friend na kubaliana na hali.
I have been in your shoes.yes it pains! But accept it kuwa karibu na mama kila kitu kitakuwa good.
 
Sina mengi ua kusema ila miezi 7 iliyopita nilipgiwa simu na mama yangu mzazi akiniambia maneno mazito na magumu sana nimeyabeba lakini naona yananishinda nawaza saana , naumia sana maneno yenyewe ndo haya"MWANANGU MIMI MAMA YAKO NIMEENDA KUPIMA NIKAAMBIWA NIMEATHIRIKA NINA UKIMWI KWA SASA NIMEANZA DOZI"
Ipo hivi mama yangu alizaa na baba yangu baadae wakaachana baba akanichkua nikwa nalelewa na baba mpaka nikafikia utu uzima. mama yangu kule aliolewa akabahatika kupata watoto wawili ila mme wake alifariki kwa huo ugonjwa.
TRULY I GOT PAINFULLY
nashindwa kukubali Matokeo naombeni Ushauri wana Jf ili niweze kukubali kuwa ni kweli mama yangu ni Muathirika.
Pole mkuu.

Ni jambo la kusikiyisha lakini jipe moyo, msisitize atumie dawa na afuate masharti

We ni mama yako, kuna wengine ni mama, baba na yeye wote waathirika

Kuna wengine wazazi wana Kansa

Ni ngumu kukubali, lakini lazima ukubali na uwe imara kwa ajili ya mama yako
 
ch

christian
Inaonekana hawakufunga ndoa na baba yako!
Pia upo uwezekano alikuwa chanzo cha kuondoka kwa baba yako (kukorofishana) ikasababisha umelelewa na baba huku mama akikuachia mtihani wa maswali mengi bila idadi lakini msingi wa maswali hayo ni kumhusu baba yako (akijaribu kum prove wrong babiyo)

Maumivu yako yanakuwa makubwa sana kwa kuzingatia kuwa hujalelewa na mama, una kiu ya malezi ya mama na unaiona nafasi hiyo ikizidi kuyoyoma ikitokomea kusikojulikana.

Hapo juu nimeandika dibaji.

Sasa unatakiwa kusonga, UNASONGAJE.

1. Acha kuishi kwenye anga la kufikirika.
2. Acha kutafuta mchawi wa tatizo lililopo.
3. Ivue na kuitupa mbali sura ya huzuni na hofu unapomfikiria mama na vvu.

Usimdhanie kakosea hata amepata maambukizi, kwa maana namna alivyo/anavyoendesha maisha yake ipo nje kabisa ya mamlaka yako.

Timiza wajibu wako kama mtoto kwa upendo uliopitiliza kwenye kipindi hiki cha mashaka makuu kwa mama.

Hatakufa ataishi.
 
mkuu nashukuru saaana kwa ushauri wako hakika Jamii forum Idumu milele.
Mkuu nitajithidi sana kusahau najua siku nitasahau
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom