Moyo wangu umekufa ganzi naomeni Msaada

Moyo wangu umekufa ganzi naomeni Msaada

Quan Lup

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2016
Posts
710
Reaction score
1,011
Sina mengi ua kusema ila miezi 7 iliyopita nilipgiwa simu na mama yangu mzazi akiniambia maneno mazito na magumu sana nimeyabeba lakini naona yananishinda nawaza saana , naumia sana maneno yenyewe ndo haya"MWANANGU MIMI MAMA YAKO NIMEENDA KUPIMA NIKAAMBIWA NIMEATHIRIKA NINA UKIMWI KWA SASA NIMEANZA DOZI"
Ipo hivi mama yangu alizaa na baba yangu baadae wakaachana baba akanichkua nikwa nalelewa na baba mpaka nikafikia utu uzima. mama yangu kule aliolewa akabahatika kupata watoto wawili ila mme wake alifariki kwa huo ugonjwa.
TRULY I GOT PAINFULLY
nashindwa kukubali Matokeo naombeni Ushauri wana Jf ili niweze kukubali kuwa ni kweli mama yangu ni Muathirika.
 
Mkuu pole sana,cha msingi pambana apate mlo sahihi.
We ni dini gani??
 
Ukimwi ni ugonjwa tu kama mengine mkuu. Sema tu jamii huwa inawachukulia waathirika kama vile sijui ni wadhambi wa namna gani. Kitu ambacho sio sahihi.

Cha muhimu mlee mama yako mpe matunzo mazuri ale vizuri na dose vizuri.

Mbona maisha yanaenda tu mkuu.
 
Pole Sana ndugu mambo ya kawaida Sana shukuru Ana Hiv.... Angekwambia cancer c ndo ungekufa presha? Kila kitu kinatokea kwa sababu...relax Mungu yu pamoja nanyi! Hakuna kubwa hapo
 
Pambana Bro
Usikate tamaa wala kuhuzunika sana
Mama kwasasa,anamtegemea Mungu kisha ww

Basi,usisababishe tatizo likawa kubwa kwa huzuni yako ana msongo wa mawazo
Ni wakati wako sasa,wakuwa karibu na Mama kimawazo na maliwazo,
Mama anakuhitaji sana kuliko unavyofikiria kwasasa
Pambana mpaka dakika yako ya mwisho,katika kumpa matumaini mazuri na huku akimjalia kwa Dawa,Chakula n.k.

Ni nani kama Mama?!!
Inauma kweli
Tumuombe Mola wetu,ampe ponyo la kweli na kumuondolea kila aina ya tatizo
 
Asan
Ukimwi ni ugonjwa tu kama mengine mkuu. Sema tu jamii huwa inawachukulia waathirika kama vile sijui ni wadhambi wa namna gani. Kitu ambacho sio sahihi.

Cha muhimu mlee mama yako mpe matunzo mazuri ale vizuri na dose vizuri.

Mbona maisha yanaenda tu mkuu.
asante sana kwa Ushauri Mzurii
 
s
Pambana Bro
Usikate tamaa wala kuhuzunika sana
Mama kwasasa,anamtegemea Mungu kisha ww

Basi,usisababishe tatizo likawa kubwa kwa huzuni yako ana msongo wa mawazo
Ni wakati wako sasa,wakuwa karibu na Mama kimawazo na maliwazo,
Mama anakuhitaji sana kuliko unavyofikiria kwasasa
Pambana mpaka dakika yako ya mwisho,katika kumpa matumaini mazuri na huku akimjalia kwa Dawa,Chakula n.k.

Ni nani kama Mama?!!
Inauma kweli
Tumuombe Mola wetu,ampe ponyo la kweli na kumuondolea kila aina ya tatizo
Shukrani saana MKuuu kweli nampambania saaana tena Saaana.
 
Mwambie " pole mama , usijali Mungu yupo na wewe. Kuna magonjwa hatari zaidi ya hayo. ...( unamtolea na mfano)"

Ili mama afarijike huku wewe unaendelea kuumia kimya kimya. Maana akiona huzuni yako utamfanya ahuzunike zaidi.

Pole mkuu.
 
asante sana
 
pole sanaa kijana mwenzangu cha msingi mama asiwe na stress na wewe usiwe nazo ale chakula vizurii mazoezi kwa sana atafika miaka mingi hadi utashangaa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom